Muziki wa taarabu....!!

Muziki wa taarabu....!!

This one is soooooo cute. Ilivyo hit nilikuwa mdogo hata sikuwa naelewa wanasema nini.....lolz

Wazazi wanazungumza na mtoto wao kwa vile anahama kwao, anaolewa

Mazuri twakutakia, japo tunateketea
Twajua unahamia, ugeni hukuzowea
Jambo tunalokwambia, uende ukirejea
Muhimu kuzingatia, malezi tulokulea

Last edited by a moderator:
Tenda wema wende zako usingoje shukurani
Viumbe roho ngoeko, fadhila hawana kwani
Mradi wavile vyako, vya tunu vya kilindoni
Hawajali wema wako, dhaifu wa ihsani
Mlipaji Mola wako, inshallah pindi mwakani
Kwako wema hauozi, wala hauna kaburi

Wako wema hauozi, wema hauna kaburi
Atakulipa Mwenyezi, endelea kusubiri

Wanadamu wana choyo, mfanyie wema gani
Umchangie chajio, pia hatokuthamini
'Memkinai mwenzio, ndie huyo firauni
Atakuendea mbio, akutie kisimani
Lakini usife moyo, mlipaji Rahmani
Mwenda tenzi na omo, umsubiri ngamani

Wako wema hauozi, wema hauna kaburi
Atakulipa mwenyezi, endelea kusubiri

Last edited by a moderator:
Hivi Teacher,

Ina maana hayo mashairi yako kwa kichwa au???

Haya bwana....kwa hilo tu,.....nimekuvulia kofia!!
 
yako kichwani eee......yawepo wapi 😛

Hivi hayo ma ujuzi hayomo kwenye ile package ya kizuri ukile na mwenzio (sharing is caring)??

Nitajaribu jaribu ingawa kichwa sasa kimesha-jam!
 
Hivi hayo ma ujuzi hayomo kwenye ile package ya kizuri ukile na mwenzio (sharing is caring)??

Nitajaribu jaribu ingawa kichwa sasa kimesha-jam!

Si hivi tuna share ...:]

Unajua inakuja natural, ukiwa na utaratibu wa kusikiliza, mwezi mwingi na wewe unaanza kutushushia mistari
 
DC mambo ya vidole juu sio???

Mie nakumbuka wimbo mmoja aliimba nani sijui "Natanga na njia nahangaika ooohhh" Naupenda sana huu wimbo
 
Nimesafi nia ...by Mohammed Ilyas

"moyoni sina nafasi, kuweka nongwa na chuki
wala si weki visasi, kufanya hivyo sitaki
kugombana nnakhisi, napotoka siongoki

ila ntavumilia, wala khasama siweki
nguzo nilotegemea, ya mola haitenguki

Last edited by a moderator:
DC mambo ya vidole juu sio???

Mie nakumbuka wimbo mmoja aliimba nani sijui "Natanga na njia nahangaika ooohhh" Naupenda sana huu wimbo

Duh ....kwa hapo pekee sijaujua, hebu ongeza mistari kidogo.
 
Duh ....kwa hapo pekee sijaujua, hebu ongeza mistari kidogo.

Gaijin bana mie mistari siijui.

But nakumbuka aliimba mwanaume eeehhh nimekumbuka jina kama sijakosea anaitwa Ali Star wakati akiwa na TOT nafikiri aahh bana kumbukumbu ziro
 
DC mambo ya vidole juu sio???

Mie nakumbuka wimbo mmoja aliimba nani sijui "Natanga na njia nahangaika ooohhh" Naupenda sana huu wimbo

natanga na njia eee, natanga na njia nahangaika yoyoyooooo
nashinda na njaa eeeh, nalala na njaa nahangaikaaaaa
lakini Mungu yupooo....
 
Gaijin bana mie mistari siijui.

But nakumbuka aliimba mwanaume eeehhh nimekumbuka jina kama sijakosea anaitwa Ali Star wakati akiwa na TOT nafikiri aahh bana kumbukumbu ziro

hahahaaa lol...
Dena umechoka??? au njaa??
 
hahahaaa lol...
Dena umechoka??? au njaa??

Ha!! We nae kunisema hadharani ndo nini?? Sijaishika mistari bana

Asante Gaijin atakuwa ameuelewa sasa watu wengine kuimba hatujui bana
 
Ha!! We nae kunisema hadharani ndo nini?? Sijaishika mistari bana

Asante Gaijin atakuwa ameuelewa sasa watu wengine kuimba hatujui bana

Nausaka kwanza sijauona.Nikiuona tu nakuwekea uburudike roho yako :]
 
Ha!! We nae kunisema hadharani ndo nini?? Sijaishika mistari bana

Asante Gaijin atakuwa ameuelewa sasa watu wengine kuimba hatujui bana

aah hata bafuni bibie weye waoga bila kijiwimbo?? akhaa hebu usiniangushe kwani wewe unataka kuimba sauti ka Bi Malika???
jipe raha mwenyewe bana imba hata 'flat' tu
 
aah hata bafuni bibie weye waoga bila kijiwimbo?? akhaa hebu usiniangushe kwani wewe unataka kuimba sauti ka Bi Malika???
jipe raha mwenyewe bana imba hata 'flat' tu

Bee mwambie huyo kuwa ukizowea kuimba hizi hata sauti inakuwa inajifanyia automatic tuning......inageuka nyororoooooo lolz

Unaosha vyombo huku na "fanya wema wende zako singojee shukurani"

ushajifunza pia hahaha
 
Ha ha ha we kweli kiboko mistari imekaa mahala pake sikuwezi.........

Haya ngoja nijifunze kuimba sauti ya1, 2, 3, 4 kwa pamoja
 
aah hata bafuni bibie weye waoga bila kijiwimbo?? akhaa hebu usiniangushe kwani wewe unataka kuimba sauti ka Bi Malika???
jipe raha mwenyewe bana imba hata 'flat' tu

Haya nimekusoma mkuu nitaimba sauti zote
 
Back
Top Bottom