Muziki wa taarabu....!!

Dark City

JF-Expert Member
Oct 18, 2008
16,253
11,598
Mimi binafsi si mpenzi wa muziki wa taarabu lakini nimekuwa nikiufuatilia kwa muda sasa...Kitu kinachonivutia ni lugha ya picha ambayo inavutia sana endapo mtu unapata nafasi ya kuitafakari!!

Nimejaribu kuvuta kumbukumbu zangu, na kukutana na baadhi ya miziki ambayo kweli inavutia!! Naweka hii hapa chini na natumai wadau watanisaidia kutukumbusha nyimbo nyingine na ikiwezekana kutuwekea baadhi ya mashairi na nukuu ambazo zili/zinawakuna!

1. Wrong namba
2. Y 2 K
3. Zumbukuku
4. Kuna waimbo fulani siukumbuki jina ila ulikuwa unasema kwamba, "manahodha wa mashua kwa nini muwe nyuma, chombo kikienda mrama nani alaumiwe"?
5. Njiwa (Patricia Hilal)
6. Asu (Abdul Misambano.....my favourite song)!!
7.

Waimbaji mahiri: Najua wako wengi ila naweza kuwakumbuka baadhi tu....
1. Shakila
2. Issa Matona
3. Khadija Kopa
4. Nasma Khamis
5. Mzee Yusufu
6.......

Hata hivyo baadhi ya nukuu ambazo nimekutana nazo hivi karibuni ni kama hizi,

"Ukiona nanga inatupwa kwenye maji, ujue jahazi limefika. Ndimu changa haina maji na bamia ikikomaa sana inapoteza thamani"....by Khadija Mohamedi!!!

Naomba michango yenu wandau kwani naanza kuvutiwa zaidi na kutamani kuufahamu zaidi huu muziki!!
 
Kasikilize "TX Nipasue"
 
Mimi najiuliza jinsi 'gay culture' ilivyo popular na muziki wa taarabu
na jnsi vikundi hivyo vinavyo shirikisha wanasiasa
na sasa wanakuja juu walipoambiwa na david cameroon 'waheshimu haki za gays'

isnt it funny??????
 
Kasikilize "TX Nipasue"

Duuhhhhhh,

Umenikumbusha mbali sana mkuu,

Enzi ile ya miaka ya tisini huu wimbo ulivuma sana iseeee!!!!

"TX nipasue, ondoa maradhi yote ya ndani....""

Haki ya nani watunzi wengine ni vichwa kweli kweli,

I am sure huu unaweza kuimbuka kuwa muziki wangu, hata kama una dalili za kulalia kwenye ngono ngono katika mistari yake""
 
Mimi najiuliza jinsi 'gay culture' ilivyo popular na muziki wa taarabu
na jnsi vikundi hivyo vinavyo shirikisha wanasiasa
na sasa wanakuja juu walipoambiwa na david cameroon 'waheshimu haki za gays'

isnt it funny??????

Kweli mkuu???

Naomba usinifanye niwaombe wahusika wanifungie hii thread!
 
kuna wimbo kaimba Issa Matona kuhusu nyuki, sijui unaitwajwe lakini maneno yake yanauliza uhalali wa asali kwa sababu hata kwenye mzoga wa nyani, nyuki hupata material za kutengeneza asali...unaitwaje huu wimbo?
 
hata mashairi yao tu ni utata...
na all the gays in dar 'wanajaa' kwenye taarabu tu..

But usiombe waifunge thread. taarab is bigger than that....hiko ni kisehemu tu..
so sisemi taarabu ni gay music no..
taarab ni music na culture kubwa tu....na marijali ni wengi kuliko hao gays...
 
Dah! Nimeusikiliza huu wimbo wote na kumkumbuka Mzee Issa Matona jinsi alivyokuwa na kipaji cha kuzichangamsha harusi mbali mbali alizoalikwa kutumbuiza. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi~AMEN.
 
Bahati mbaya hii miziki haipo kwenye you tube...Ngoja wadau waje watusaidie,

Ila ukweli utabaki pale pale kwamba huyu babu alikuwa ni jabali la muziki wa Taarabu,
 
Ahsante mkuu,

Umenirudishia amani yangu...Nimeshusha pumzi utadhani nimemwagiwa maji ya baridi saaana!

Tuendelee kukumbushana!!
 
Dah! Nimeusikiliza huu wimbo wote na kumkumbuka Mzee Issa Matona jinsi alivyokuwa na kipaji cha kuzichangamsha harusi mbali mbali alizoalikwa kutumbuiza. Mwenyezi Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi~AMEN.

Kweli mkuu...Huu wimbo ulikuwa popular sana katika harusi za miaka ya 90 na kikundi chote cha mzee Matona kilijizolea umaarufu sana enzi hizo. Nakumbuka kuona (kwenye VHS) jinsi walivyokuwa wanapagawisha watu kwenye harusi!
 
Bahati mbaya hii miziki haipo kwenye you tube...Ngoja wadau waje watusaidie,

Ila ukweli utabaki pale pale kwamba huyu babu alikuwa ni jabali la muziki wa Taarabu,

Upo mkuu

Ila mie leo nna ujumbe huu " Mbuzi isiyo na meno itaikunaje nazi"

Last edited by a moderator:
UTAIKUNAJE NAZI MBUZI HUNA MENO.....mashallah!!

bure utafurukuta ujiumize mikono atii....
 
Karibu sana Teacher,

Nilishaanza kusikitika kwamba Muziki ambao unaonekana kuwa wetu kwa kila kitu hauna wadau!

Nitasikiliza kwa makini choice yako!! Nikikutana na mistari migumu nitakuja kuomba msaada, ....sawa teacher!!

Babu DC
 
Wadau tupo tulikuwa mbali tu

"utakuna kutwa kichwa, kwa ndole na visigino
nazi haitoki chicha, japo bingwa wa mikuno..."

Bee aseme kama tumtafsirie hiyo part ...lolz
 
  • Thanks
Reactions: bht
Wadau tupo tulikuwa mbali tu

"utakuna kutwa kichwa, kwa ndole na visigino
nazi haitoki chicha, japo bingwa wa mikuno..."

Bee aseme kama tumtafsirie hiyo part ...lolz

Ama kweli,

Lugha ya huu muziki si kama ile ya ubongo wa fleva!!

Hivi under 18 huwa wanaelewa kweli?

Na uzee wangu bado nahitaji msaada hapa na pale!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom