Muuza chips atunukiwa nishani na Prof. Kikwete

Muuza chips atunukiwa nishani na Prof. Kikwete

Nakuunga mkono hoja yako mkuu! ila kwanza aje Pasco

Imeandikwa "Mtu hata ishi kwa mkate tuu!", vivyo hivyo, mtu hataishi kwa nishani za kutazamana usoni!, nishani ya kweli ni ile iliyo ndani ya mioyo ya watu!.

Kwa EL kunyimwa nishani mbona haya ni madogo tuu, nini nishani?!, subirieni kushuhudia jinsi lile "jiwe walilolikataa waashi, litakavyofanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Pasco.
 
Kama vipi na yeye aanze kutembea na chepe labda atakutana na jambazi mwenye chamoto akimpiga atapewa ya ushupavu kama dogo Kassim
 
  • Thanks
Reactions: 4GB
Imeandikwa "Mtu hata ishi kwa mkate tuu!", vivyo hivyo, mtu hataishi kwa nishani za kutazamana usoni!, nishani ya kweli ni ile iliyo ndani ya mioyo ya watu!.

Kwa EL kunyimwa nishani mbona haya ni madogo tuu, nini nishani?!, subirieni kushuhudia jinsi lile "jiwe walilolikataa waashi, litakavyofanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Pasco.

Niliwaambia subirini aje , mmemsomaa?Eti lowasa ni jiwe la msingi la kwenye kona, ya kweli haya??Kwani nchi hii haina watu mpaka Rais awe lowasa na makandokando yake yoooote!??
 
quote_icon.png
By 4GB
Baba yangu hajawahi kuwa Waziri Mkuu na akajiuzulu kwa aibu kutokana na ubadhirifu, Mume wangu hajawahi kuwa Waziri wa Maji na akajisifu kwamba amevuta maji kutoka ziwa Victoria huku akijua fika kwamba ni uongo, na mke wangu hajawahi kushikwa na wivu kiasi kwamba anajua mimi ni Baba wa familia na akataka anipindue. Madaraka yake kama mke yanamtosha, anajua mipaka yake. Sifa za kijinga hataki.



Mkuu 4GB, umeniacha hoi hapo. Loudly thinking, ina maana Lowasa alijaribu kumpindu JK...kwa maana hiyo hata kashfa ya Richmond ilipikwa ili tu wamwondea mhaini? Hebu tusaidie bwana, unajua kama hilo ndilo lilimwondoa Lowasa, then nchi iko hatarini sana, maana roho ya mapinduzi haifi..na tusishangae Lowasa akampindua JK kwa ticktack hapo 2015, si kwa mtutu bali kwa kumzidi maarifa tu! Na hapo ikitokea..ya Chiluba ni madogo!!!​


  • UKIONA MTU MLIKUWA WASHKAJI M[PAKA MNAGONGEANA MADEMU ....SIKU MKI CHANGIANA NI JAHU KWELIKWELI...
    KAMA MTU SI MNAFIKI SIASA ITAKUWA NGUMU KWAKO
 
Amentimwa au hajapata? Tuache siasa uchwara humu zenye propaganda za uchochezi na ufitini. We leta sera watu wapambue siyo oooh kanyimwa ohh amefanya sijui kitu gani. Hadi sasa Lowasa hana sifa za kuwa Rais
 
Kati ya Sitta na Lowassa nani mwenye historia na nchi hii? You got to be kiddin me!
sitta atakumbukwa daima kwa unafiki wake, hamna mtanzania mwenye unafiki wa SITTA
 
Imeandikwa "Mtu hata ishi kwa mkate tuu!", vivyo hivyo, mtu hataishi kwa nishani za kutazamana usoni!, nishani ya kweli ni ile iliyo ndani ya mioyo ya watu!.

Kwa EL kunyimwa nishani mbona haya ni madogo tuu, nini nishani?!, subirieni kushuhudia jinsi lile "jiwe walilolikataa waashi, litakavyofanywa kuwa jiwe kuu la pembeni!".

Pasco.
nyerere kabla ya kuwa rais alikuwa na nishaaaaaaaaani ipi? nishani mbona mpaka makinda na sitta wamechotewa wameifanyia nini hii nchii?

LOWASSA haitaji nishani ili kuonesha kukubalika , LOWASSA anajulikana kwa maamuzi magumu na spidi ya utendani.
kwa CCM hamna anayeuzika uraiani kama Lowassa
watu wa kanda ya ziwa tutamkumbuka daima alivyotuletea maji from victoria na kuvunja mkataba wa kijinga wa MISRI KUWA MTUMIAJI PEKEE YA MAJI YA VICTORIA
 
Ingekuwa kuna nishani ya ufisadi Lowasa angekuwa wa kwanza kupewa
 
Chenge Mzee wa Visenti naye atapewa lini ............................ Hebu, subirini nishani za mwisho za Kikwete za 26 April 2015, ndiyo uje na huo usemi wako!!!
 
Chenge Mzee wa Visenti naye atapewa lini ............................ Hebu, subirini nishani za mwisho za Kikwete za 26 April 2015, ndiyo uje na huo usemi wako!!!
Naye Chenge angekuwa wa pili kupewa nishani ya ufisadi
 
Bandiko lako limejamejaa hoja nzito lakini sitachangia mpaka mkuu Pasco atoe maoni yake kwanza.
 
Last edited by a moderator:
lowassa anawatesa watu sana yeye ametulia anakula maisha yake wengine wenye njaa wana angaika kwenye mitandao kumchafua......tanzania ni nchi ya ajabu sana..watu badala ya kupiga kazi wao ni kufuatilia maisha ya watu
 
Wabongo bana...yaani hata nishani mnatumia kupambana na Lowassa..jamaa kakaa kimya nyie mnawiraaaaa...kwa taarifa yenu tu ni kua huyu jamaa anakubalika kuliko maelezo..jpo mnamuandama kila siku.tulieni tu mfikirie pa kukimbilia jamaa akiingia magogoni manake apa mchofanya na kumuongezea hasira tu
 
Mwinyi alijiuzulu kwa tuhuma tu.....hao wengine mpaka wameundiwa tume na chunguzi mbalimbali ndio wakajiuzulu kwa shingo upande
 
mkuu nilikuwa silijui hili. asante kwa kuongeza kitu kipya kichwani mwangu.

mkuu unadhani kwann mkapa alikubali kupanda mahakamani na kumtetea na kwann kapewa ukuu wa chuo chao kule bagamoyo
 
LOWASSA ATOSWA NISHANI KWA MARA NYINGINE! APITWA NA MUUZA CHIPSI!

Mwaka 2011 wakati taifa likisherehekea miaka 50 ya Uhuru Rais Jakaya Kikwete aliwatunuku nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili wanasiasa mbalimbali waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu na Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania, huku akiwatosa Edward Lowassa, John Malecela na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambao nao, waliwahi kutumikia nafasi hizo.

Katika sherehe hizo Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Aprili 2014 wakati wa sherehe za Muungano ukawa neema kwa Jaji Josepha Sinde Warioba aliyepewa nishani ya daraja la kwanza katika kulinda Muungano pamoja na wenzake wengine kama Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Aman Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk Salmin Amour Juma. Wengine ni Omar Ali Juma na Idrissa Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.

Wengine walioanza kupata tuzo na nishani hizo katika sikukuu ya Muungano ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume (wote ni marehemu) na walioendeleza ambao ni Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wengine waliopewa tuzo ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama akiwemo Mkuu wa Jenshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa akiwemo, Jenerali Mirisho Sarakikya na Jenerali David Musuguri.

Katika nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne lilikuwa na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano. Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi mwezi huo wa Aprili alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.

SITTA, MUUZA CHIPSI WAMPIKU

Kwa nishani zilizotolewa juzi tarehe 9 Desemba katika sherehe za Uhuru Rais Kikwete aliendelea na zoezi lake la kuwatunuku nishani viongozi mbali mbali waandamizi wa serikali ikiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Paul Rupiah, Spika Chief Adam Sapi Mkwawa (marehemu), Mzee Kingunge, Mama Anna Abdallah, Balozi Dk. Augustine Mahiga (Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa mstaafu), Spika Samuel Sitta na aliyekuwa kivutio kikubwa kuliko wote kijana Kassim Said Kassim (muuza chipsi wa Buguruni malapa aliyezaliwa mwaka 1986) alivikwa nishani ya ushujaa kwa kujitolea mhanga na kumdhibiti jambazi aliyekuwa na silaha ya moto ambaye angeleta madhara makubwa. Hii imewafanya wadau mpaka kujiuliza, je mzee wa ‘maamuzi magumu’ aliachwa wapi? Au ni kwamba nchi hii haitambui michango yake ambayo amekuwa akijikweza kama ni yakishujaa?

LOWASSA KUTOSWA

Kwa upande wake Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 2005 hadi Februari mwaka 2008, katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete ni Waziri Mkuu pekee yake aliyestaafu ama kujiuzulu ambaye bado hajatunukiwa Nishani yeyote na taasisi kuu ya Rais ukiachilia mbali ya hulka yake ya kutamblika kama mzee wa ‘maamuzi magumu’. Lowassa ambaye ni mshirika wa siku nyingi kisiasa wa Rais Kikwete, alijiuzulu kufuatia kashfa ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Miaka ya hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, Lowassa alijaribu kujitetea dhidi ya kashfa hiyo lakini hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema bado hajawa safi mbele ya serikali inayoongozwa na swahiba wake Rais Kikwete. Lowassa alisema hakuhusika moja kwa moja katika hilo lakini alilazimika kujiuzulu kwa sababu waliozembea na maofisa walioko chini yake.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa dhamira yake ilikuwa kuvunja mkataba wa Richmond jambo alilomjulisha pia mkubwa wake (Rais Kikwete) kwa simu akiwa nje ya nchi, lakini Rais alimwambia asubiri kwanza kwani alipata ushauri kutoka kwa makatibu wakuu kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu ndani ya serikali wenye nafasi zao nyeti wanasema utetezi wa Lowassa bado haujakidhi kumfanya awe safi, ndio maana hakuweza na hajawahi kutunukiwa tuzo yeyote ile hadi sasa. Walitoa mfano kwamba kwenye sherehe za miaka 50 ya Uhuru, Rais Kikwete alimtunuku Nishani ya Juu ya Julius Kambarage Nyerere na Rais wa

Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ingawa naye aliwahi kujiuzulu kutokana na kashfa ya mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Mwalimu Nyerere. Kwa uwajibikaji huo, Rais Kikwete aliutaja kuwa ni moja ya mambo ambayo yalionyesha kuwa Mwinyi ni mwadilifu.

Wachunguzi wa mambo haya ya siasa wanadai kitendo cha Mzee Mwinyi kujiuzulu na leo anatunukiwa nishani hiyo ni changamoto muhimu kwa Lowassa kutambua kuwa pamoja na maelezo yake ndani ya NEC, bado usafi kwa kashfa zinazomwandama unatia shaka, kwani yeye alijiuzulu baada ya Bunge kuunda tume iliyochunguza na kutoa mapendelezo ya ‘kupima’ lakini Mzee Mwinyi alipima mwenyewe uzito wa tukio na kuamua kuachia ngazi.

NJIA KUELEKEA 2015 BADO NI NGUMU KWA LOWASSA, NADHANI IMEFIKA WAKATI WA YEYE ‘KUPIMA’ KWA MARA NYINGINE KABLA HAJAKUTANA NA DHORUBA KUU! LOWASSA HASAFISHIKI!


Chanzo: Mwisho wa Lami



Kama simu yako ya mkononi haikatiki kiganjani mwako muda wowote, inaweza ikawa inaharibu uhusiano wako na umpendaye. Wanasaikolojia wamesema kuwa watu wengi kwa sasa wanalazimika kushindana na smartphone za wapenzi wao kupata attention.

Utafiti uliofanywa, umebaini kuwa robo tatu ya wanawake wanaona kuwa smartphones zinaingilia maisha yao ya mapenzi na kupunguza muda ambao wangetumia kuzungumza au kuwa karibu na wapenzi wao. Wanasayansi wamedai kile walichokiita ‘technoference’ kina madhara makubwa kama migogoro mingi, kupunguza quality ya uhusiano, kupunguza mridhisho wa maisha na hatari kubwa ya msongo wa mawazo.

Utafiti huo ulifanywa na mwanafunzi wa chuo kikuu cha jimbo la Pennsylvania, Marekani na mwingine wa chuo kikuu Brigman Young University cha Utah na kuhusisha wanawake 143.

Asilimia 62 walisema teknolojia imeingilia muda waliotumia pamoja na wapenzi wao na theluthi moja wakisema boyfriend zao waliangalia smartphone wakati wakizungumza.

Wanasayansi hao wameshauri kuweka simu silent na kutokuwa nazo muda wote ili kuwa na muda wa kufocus kwa mpenzi wako. “Kama unataka kuangalia kitu muhimu, toa maelezo kwanza na kisha angalia simu yako.

Na pia usijitetee pale mpenzi wako akionesha kukerwa na tabia yako ya kuangalia sms au kucheza games mara kwa mara – ni njia ya yeye kusema kuwa angetaka kuconnect na wewe moja kwa moja,” wamesema.



linda ndoa yako achana na kukariri kukaa na simu muda wote ni dili
 
Back
Top Bottom