Muuza chips atunukiwa nishani na Prof. Kikwete

Muuza chips atunukiwa nishani na Prof. Kikwete

.. Elli buku7 saba walustahili nishani nao vp hawajapewa au
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tayari keshajulikana na watu usishangae keshokutwa ukamkuta ni askari. Apart from that kila mkazi wa buguruni aliyesikia hiyo habari atapenda kula bandani kwake ili amfahamu zaidi.

ok labda mkuu but it is so indirect. Angemfanyia kitu ambacho kingebadilisha maisha ya uyo jamaa-ata aboreshe biashara yake
 
Watanzania tuna tabia ya kupiga makofi tu bila kupima athari ya kitendo kilichofanyika, kuna ujasiri gani kumvaa mtu mwenye silaha, je alikuwa na uhakika gani kama hana wenzake amekuja nao wapo nje? Je kama hao wakitokea kumsaidia mwenzao wakiwa na silaha? kingetokea nini? Ushujaa ni kutii amri wanazotoa hao majambazi uwape wanachotaka kama pesa,saa,simu NK. Huyo mnaomsifu angeweka maisha yake na ya watu wengine hatarini, unapaswa kuchukua hatua kama hiyo kama huna budi umeshaona jambazi ameanza kuuwa au unaona anatishia kweli maisha ya watu, lakini hawa mara nyingi tunawaona na kusikia wanakuja kwasababu ya njaa zao wanaonyesha silaha zao katika mabaa na kutaka wapewe pesa au simu na mkiwapa wanaondoka zao. Kushabikia mambo kama haya ipo siku kuna mtu ataingia sehemu na atatokea kijana ajifanye mbabe atake nae kutunikiwa nishani kama huyu hapo, inaweza tokea akasababisha kuumia au kuuwawa kwa wananchi na kuyahatarisha maisha yake pia.Hayo mambo ya usalama yanataka yashughulikiwe na polisi waliopitia mafunzo na ni kazi zao. Kama ni self defence wakati huna budi sawa, lakini siyo kitendo kama hichi hakikuwa unahitaji ujihami risk yake ilikuwa kubwa ukichukua uamuzi wa kutumia nguvu. Tunatakiwa tuwaelimishe wananchi jinsi ya kukwepa kuweka maisha yao hatarini linapotokea jambo kama hili na sio kushangilia kwa jazba.
 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete juzi, ametunuku Nishani ya Ushupavu kwa mfanyabiashara ya kukaanga na kuuza viazi (chips) wa Dare s Salaam , Bwana Kassim Saidi Kassim, kwa kitendo chake cha kuokoa wananchi dhidi ya jambazi.

Bwana Kassim Saidi Kassim alikuwa mmoja wa watunukiwa 28 wa nishani mbali mbali ambazo Rais Kikwete alitunuku ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Miaka 53 ya Uhuru.

Katika sherehe ya kutunuku nishani iliyofanyika kwenye Bustani za Ikulu, Rais Kikwete alieleza kuwa amemtunuku Bwana Kassim Nishani hiyo kwa sababu ya kitendo cha ushupavu alichokionyesha cha kujitoa mhanga kukabiliana na jambazi mwenye silaha ambaye angeleta madhara makubwa.

Katika maelezo yaliyosomwa kabla ya Rais Kikwete kumtunuku Nishani hiyo, ilielezwa kuwa mnamo Julai 7, mwaka jana, 2013, majira ya saa 3:15 usiku, Bwana Kassim akiwa katika eneo lake la biashara, alitokea jambazi akiwa na silaha aina ya bastola na kuanza kuwashambulia wateja kwa kuwapiga makofi na kuwapora mali zao na fedha zao.

Na “Kwa ushupavu mkubwa ulichukua chepe na kumpiga jambazi huyo mara mbili kichwani, kipigo kilichosababisha aanguke na kupoteza fahamu. Kitendo hicho kilifanikisha kukamatwa kwa bastola aina ya Globe ambayo nambari zake zilikuwa zimefutwa ikiwa na risasi tano ndani yake na hivyo kuepusha madhara ambayo yangeweza kusababishwa na matumizi mabaya ya silaha hiyo.”

Bwana Kassim anakuwa muuza chips wa kwanza katika historia ya Tanzania kutunukiwa Nishani ya Ushapavu na Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Bwana Kassim mwenye umri wa miaka 28 alizaliwa katika Kijiji cha Namwinyu, Wilaya ya Tunduru, Mkoa wa Ruvuma mwaka 1986. Alisoma na kumaliza elimu yake ya msingi mwaka 2002 katika Shule ya Msingi ya Ilala, iliyoko Wilaya ya Ilala, Dar Es Salaam.

Baada ya kumaliza elimu ya msingi, alianza kujishughulisha na biashara ya kukaaga na kuuza viazi (chips) katika eneo la Buguruni Malapa.
 
LOWASSA ATOSWA NISHANI KWA MARA NYINGINE! APITWA NA MUUZA CHIPSI!

Mwaka 2011 wakati taifa likisherehekea miaka 50 ya Uhuru Rais Jakaya Kikwete aliwatunuku nishani ya Mwenge wa Uhuru Daraja la Pili wanasiasa mbalimbali waliowahi kushika nyadhifa za Uwaziri Mkuu na Makamu Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Muungano wa Tanzania, huku akiwatosa Edward Lowassa, John Malecela na Mzee Aboud Jumbe Mwinyi ambao nao, waliwahi kutumikia nafasi hizo.

Katika sherehe hizo Kikwete aliweka wazi kwamba, nishani hizo zimetolewa kwa Makamu Rais na Mawaziri Wakuu wastaafu walio hai ama waliokufa, walioondoka madarakani bila kashfa na hata baada ya kuondoka kwao madaraka, wameendelea kuwa na maadili mema na kuishi kwa heshima na maadili ya ofisi yao.

Aprili 2014 wakati wa sherehe za Muungano ukawa neema kwa Jaji Josepha Sinde Warioba aliyepewa nishani ya daraja la kwanza katika kulinda Muungano pamoja na wenzake wengine kama Aboud Jumbe Mwinyi aliyekuwa Rais wa Pili wa Zanzibar, Aman Karume, John Malecela, Cleopa Msuya na Dk Salmin Amour Juma. Wengine ni Omar Ali Juma na Idrissa Abdul Wakil, ambao sasa ni marehemu.

Wengine walioanza kupata tuzo na nishani hizo katika sikukuu ya Muungano ni waasisi wa Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Karume (wote ni marehemu) na walioendeleza ambao ni Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa.

Wengine waliopewa tuzo ni pamoja na viongozi wa majeshi ya ulinzi na usalama akiwemo Mkuu wa Jenshi la Wananchi (JWTZ), Jenerali Davis Mwamunyange na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Ernest Mangu. Wakuu wa JWTZ wastaafu pia walikumbukwa akiwemo, Jenerali Mirisho Sarakikya na Jenerali David Musuguri.

Katika nishani ya kumbukumbu ya miaka 50 ya Muungano daraja la nne lilikuwa na Mama Maria Nyerere na Mama Fatma Karume, Bendi ya Msondo Ngoma pia ilipewa tuzo kwa kuuenzi Muungano. Naye Mwenyekiti Mtendaji wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi mwezi huo wa Aprili alipewa tuzo maalumu akiwa raia wa Tanzania aliyetoa mchango muhimu katika huduma za jamii.

SITTA, MUUZA CHIPSI WAMPIKU

Kwa nishani zilizotolewa juzi tarehe 9 Desemba katika sherehe za Uhuru Rais Kikwete aliendelea na zoezi lake la kuwatunuku nishani viongozi mbali mbali waandamizi wa serikali ikiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu Balozi Paul Rupiah, Spika Chief Adam Sapi Mkwawa (marehemu), Mzee Kingunge, Mama Anna Abdallah, Balozi Dk. Augustine Mahiga (Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa mstaafu), Spika Samuel Sitta na aliyekuwa kivutio kikubwa kuliko wote kijana Kassim Said Kassim (muuza chipsi wa Buguruni malapa aliyezaliwa mwaka 1986) alivikwa nishani ya ushujaa kwa kujitolea mhanga na kumdhibiti jambazi aliyekuwa na silaha ya moto ambaye angeleta madhara makubwa. Hii imewafanya wadau mpaka kujiuliza, je mzee wa ‘maamuzi magumu' aliachwa wapi? Au ni kwamba nchi hii haitambui michango yake ambayo amekuwa akijikweza kama ni yakishujaa?

LOWASSA KUTOSWA

Kwa upande wake Lowasa aliyekuwa Waziri Mkuu tangu mwaka 2005 hadi Februari mwaka 2008, katika Serikali ya Awamu ya Nne, chini ya Rais Jakaya Kikwete ni Waziri Mkuu pekee yake aliyestaafu ama kujiuzulu ambaye bado hajatunukiwa Nishani yeyote na taasisi kuu ya Rais ukiachilia mbali ya hulka yake ya kutamblika kama mzee wa ‘maamuzi magumu'. Lowassa ambaye ni mshirika wa siku nyingi kisiasa wa Rais Kikwete, alijiuzulu kufuatia kashfa ya utoaji zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa kampuni tata ya Richmond Development LCC.

Miaka ya hivi karibuni kwenye kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, kilichofanyika mjini Dodoma, Lowassa alijaribu kujitetea dhidi ya kashfa hiyo lakini hata hivyo wachunguzi wa mambo wanasema bado hajawa safi mbele ya serikali inayoongozwa na swahiba wake Rais Kikwete. Lowassa alisema hakuhusika moja kwa moja katika hilo lakini alilazimika kujiuzulu kwa sababu waliozembea na maofisa walioko chini yake.

Alikwenda mbali zaidi na kueleza kuwa dhamira yake ilikuwa kuvunja mkataba wa Richmond jambo alilomjulisha pia mkubwa wake (Rais Kikwete) kwa simu akiwa nje ya nchi, lakini Rais alimwambia asubiri kwanza kwani alipata ushauri kutoka kwa makatibu wakuu kuhusu jambo hilo. Baadhi ya watu ndani ya serikali wenye nafasi zao nyeti wanasema utetezi wa Lowassa bado haujakidhi kumfanya awe safi, ndio maana hakuweza na hajawahi kutunukiwa tuzo yeyote ile hadi sasa. Walitoa mfano kwamba kwenye sherehe za miaka 50 ya Uhuru, Rais Kikwete alimtunuku Nishani ya Juu ya Julius Kambarage Nyerere na Rais wa

Awamu ya Pili, Ali Hassan Mwinyi ingawa naye aliwahi kujiuzulu kutokana na kashfa ya mauaji ya vikongwe mkoani Shinyanga wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani katika Serikali ya Mwalimu Nyerere. Kwa uwajibikaji huo, Rais Kikwete aliutaja kuwa ni moja ya mambo ambayo yalionyesha kuwa Mwinyi ni mwadilifu.

Wachunguzi wa mambo haya ya siasa wanadai kitendo cha Mzee Mwinyi kujiuzulu na leo anatunukiwa nishani hiyo ni changamoto muhimu kwa Lowassa kutambua kuwa pamoja na maelezo yake ndani ya NEC, bado usafi kwa kashfa zinazomwandama unatia shaka, kwani yeye alijiuzulu baada ya Bunge kuunda tume iliyochunguza na kutoa mapendelezo ya ‘kupima' lakini Mzee Mwinyi alipima mwenyewe uzito wa tukio na kuamua kuachia ngazi.

NJIA KUELEKEA 2015 BADO NI NGUMU KWA LOWASSA, NADHANI IMEFIKA WAKATI WA YEYE ‘KUPIMA' KWA MARA NYINGINE KABLA HAJAKUTANA NA DHORUBA KUU! LOWASSA HASAFISHIKI!


Chanzo: Mwisho wa Lami
 
sawa tumekuskia asimpatie nishani tu.....ampe hela ili aongeze mtaji wake wa chips......
alijitoa mhanga huyo kassim
 
sub heading "sita na muuza chips" kinanifanya nikupe nishani ya uzalendo daraja kwanza, hi ni category sahisi kabisa kwa bwana sita.
 
  • Thanks
Reactions: 4GB
Lowasa kaonewa, na pia chenge alipaswa kupewa nishani ya ukwapuaji mabilioni ya umma kila kashfa!
 
  • Thanks
Reactions: 4GB
Back
Top Bottom