kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 17,930
- 17,356
Hongera Mr. Kassim Said Kassim kwa kutunukiwa nishani na Rais kwa 'ushujaa" wako uliouonyesha wa kulidhibiti "jambazi" kwa chepe. Bila shaka kuanzia sasa vijana wengine wataanza kuyawinda majambazi yenye bastola kwa kutumia silaha duni kama vile machepe, miko ya kusongea, bakora, mapanga, michi, marungu na vijinga vya moto ili wapate bahati kama yako ya kukanyaga Ikulu . Wasiwasi yangu ni kwamba nishani hii ya muuza chips inaweza kusababisha maafa makubwa kwa vijana watakao jaribu kumuiga muuza chips huyu kama alivyofanya yeye kwa kupambana na mtu mwenye silaha ya moto (iga ufe).
Wasiwasi wangu mwingine ni kuwa vijana wapenda misifa na nishani wanaweza kufanya hivyo kwa kuwawinda "majambazi feki" wasiokuwa na hatia kwa kuwasingizia kuwa walitaka kupora fedha au chips zao. Hivyo, maelezo lazima yatolewe kwa jamii ili kufahamu sifa za mtu jambazi (case definition) ili raia wema wasije wakadhibitiwa na watu watakaotamani kupewa nishani na Rais.
Wasiwasi wangu ya tatu ni kuwa utoaji wa nishani kama hizi utakuwa endelevu kwa vijana wote waliofanya na watakaofanya matukio ya kijasiri kama haya?. Matukio yanayostahili nishani na vigezo vyake lazima vifahamike kwa wananchi.
Je, kwa kitendo hicho Kassim Said Kassim amepatiwa ulinzi gani na serikali dhidi ya ndugu, marafiki na washirika wa jambazi alilolipiga chepe? bado anaishi Buguruni na kazi yake ileile ya kukaaga chips?
Hongera sana Kassim.