Muungano wetu: Ujumbe huu kwenye bango la Timu ya Taifa Zanzibar unamaanisha nini?

Jamani naomba anayefahamu faida za huu muungano kwa Tanzania bara au Tanganyika anifahamishe,mm uelewa wangu ni mdogo Kila nikijaribu kutafuta faida za muungano sizioni
Kwanza uasisi wake tu ni magumashi, LISSU aliwahi kuuchambua bungeni kiundani saana huu muungano namna ulivyoasisiwa na jinsi gani ulivyo batili, hiyo video ipo Youtube.

Ilikuwa ni kamati ya maridhiano ya muundo wa katiba mpya, kamati ilikuwa chini ya Jaji Warioba na Spika wa kipindi hiko alikuwa Samwel Sitta.
 
Na wapo sahihi kabisa, mimi nikimuona mtu anajifananisha na Kenya namuona ni kama mwehu, wale wana akili kweli wala hawatuonei.

Tuna ardhu ya kutosha kwa kilimo, tuna madini takriban yote, tuna bandari, mbuga za kutosha, gas, mito ya kutosha n.k na bado hatujawafikia kiuchumi, Je hizi rasilimali wangekuwa nazo wao je au hata Kagame?

Tukubali tu kuwa sisi Watanzania CCM wameiua nchi na kutufanya tubaki hapa kwenye shimo la umasikini.
Sio kweli kuwa wao Wana akili kuliko watanzania,jambo kubwa ni uongozi tulionao lakini pia historia ya afrika mashariki kuwa nchi moja chini ya ukoloni,Kenya ilifwnywa nyumbani kwa wakoloni hivyo paliwekezwa viwanda vingi na miundo mbinu
 
Kuwepo na Serikali 3, yaani Serikali ya Tangayika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano ama kama hayo hayawezekani basi Muungano uvunjike
 
Mkuu, sisi huku akili ni nzito. Mpaka sasa embu tazama hata Demokrasia kati ya Tz na Kenye ni wapi iliyo juu? Si juzi tu hapo 2020 tukaamua kuua upinzani na mpaka sasa nchi upinzani?

Sio sisi ambao kwenye rasilimali za msingi za nchi tunaamua kuziua na kujadili hatutaki? Anza mikataba ya gas, mikataba ya madini n.k

Si ni Tanzania bandari imeshindwa kujiendesha yenyewe? Sehemu ambayo inachukua namba 2 sijui 3 kuchangia pato la Taifa, tumeona vyema aje mwekezaji aendeshe?

Si hapa hapa Tanzania sukari gharama za vyakula kila siku zinapanda juu while ni moja ya nchi yenye ardhi nzuri ya kilimo Afrika? Tuondoe ushabiki na tuwe wawazi, leo unasema wakoloni walianzisha viwanda vingi na miundombinu Kenya, upo sahihi kabisa.

Je, unajua kuwa Mwinyi aliua viwanda vingi sana ambayo Mwalimu alianzisha kwa sehemu? Kwa rasilimali ambazo tunazo, sisi tumeshindwa kuanzisha viwanda vya kwetu?
 
Kuwepo na Serikali 3, yaani Serikali ya Tangayika, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Muungano ama kama hayo hayawezekani basi Muungano uvunjike
Sidhani kama tunapaswa kuwa na options, huu muungano ni ufe tu moja kwa moja, ila kubwa zaidi hapo ni suala la kiusalama, ile nchi itaenda kuwa kitovu cha ugaidi Afrika Mashariki.

Naam, Zanzibar itakuwa ni kitovu cha ugaidi.
 
Kwanza uasisi wake tu ni magumashi, LISSU aliwahi kuuchambua bungeni kiundani saana huu muungano namna ulivyoasisiwa na jinsi gani ulivyo batili, hiyo video ipo Youtube.

Ilikuwa ni kamati ya maridhiano ya muundo wa katiba mpya, kamati ilikuwa chini ya Jaji Warioba na Spika wa kipindi hiko alikuwa Samwel Sitta.
Ahsante
 
Wazanzibar wana akili ndio maana wanapata maendeleo na projects kubwa ,huku pesa zote zinapelekwa Dodoma..

Miji mingine hovyo hakuna hata majengo ya maana yote yanajengwa Dodoma na Arusha.
 
Sioni kosa lo lote! Tujifunze UK!
Wales, England, Scotland, nadhani kama sikosei kila moja ina Uachama wa FIFA! Na kwa miaka mingi zimekuwa zikishiriki makombe mbali mbali mfano Euro, World Cup pamoja na kwamba ziko ndani United Kingdom!
Nadhani angalau kwenye michezo Koti la Muungano lilegezwe wajitegemee!
 
Brother nafahamu mwingiliano wa hayo makabila ila ukweli ni kwamba wakenya wanawadharau watanzania,wanaona ni watu wasio na elimu,akili na watu maskini pia hawapo proud kuwa na ukaribu wa kimahusiano na watanzania,tafiti Hilo swala mkuu
Kwani uongo? Kitendo cha CCM kuendelea kua madarakani ni inductor number moja ya ujinga wa watanzania
 
Timu ya Taifa ya Zanzibar maarufu kwa jina la Zanzibar Heroes imebeba bango lenye logo ya CAF likiwa na ujumbe huu;

"Zanzibar should be restored as the 55th member state. Its time now to take us seriously" ~ "Zanzibar inapaswa kurudishwa kama mwanachama wa 55. Ni wakati sasa wa kutuchukua kwa uzito"

Ujumbe huu unamaanisha nini?

Kwa kuwa huu ujumbe umo katika nembo ya CAF na wala sio nembo ya Umoja wa Afrika, iko wazi kuwa Zanzibar Heroes au Timu ya Taifa ya Zanzibar, inachoomba hapa ni uanachama wa CAF. Mimi badala ya kuutafsiri ujumbe huu kuwa ni "uhaini" kama mmoja alivyodai huko chini, ninaona kama ni "uchochezi uchwara" kwa kupindisha lengo la ujumbe kutoka kwenye mpira hadi shutuma za kutaka kuvunja Muungano.
Naomba hapa tujadili iwapo Zanzibar ina haki ya kuwa mwanachama wa CAF au la. Ikiwa Wana haki au hawana, ni kwa nini na kwa maslahi ya nani.
 
CAF nao hawajielewi wamewaruhusu nusunusu. Wameruhusu Vilabu, basi waruhusu na timu yao ya Taifa.
 
Mboga mboga sijui ni kwa nini Wana ka ng'ang'ania kale kasehemu na wakati hakana faida yoyote zaidi ya hasara tuu,

Ugaidi,sunajua pale conditions zote za ugaidi zipo ni vile tu majeshi ya tanganyika bado yananguvu huko.
 
Kwa kuwa huu ujumbe umo katika nembo ya CAF na wala sio nembo ya Umoja wa Afrika, iko wazi kuwa Zanzibar Heroes au Timu ya Taifa ya Zanzibar, inachoomba hapa ni uanachama wa CAF. Mimi badala ya kuutafsiri ujumbe huu kuwa ni "uhaini" kama mmoja alivyodai huko chini, ninaona kama ni "uchochezi uchwara" kwa kupindisha lengo la ujumbe kutoka kwenye mpira hadi shutuma za kutaka kuvunja Muungano.
Naomba hapa tujadili iwapo Zanzibar ina haki ya kuwa mwanachama wa CAF au la. Ikiwa Wana haki au hawana, ni kwa nini na kwa maslahi ya nani.
Hio kitu imepigwa two in one
 
Ugaidi,sunajua pale conditions zote za ugaidi zipo ni vile tu majeshi ya tanganyika bado yananguvu huko.
Kuendelea kuwakumbatia ni kuendelea kuiletea nchi hasara tuu wakiharibu vya watu huko Tanzania ndio inalipa na wao hawachangii chochote kwenye Tanzania na niwa baguzi Sana wale jamaa
 
Brother nafahamu mwingiliano wa hayo makabila ila ukweli ni kwamba wakenya wanawadharau watanzania,wanaona ni watu wasio na elimu,akili na watu maskini pia hawapo proud kuwa na ukaribu wa kimahusiano na watanzania,tafiti Hilo swala mkuu
Mimi nipo karibu sana na wakenya na ninaishi nao vizuri tu ingawa huwa tunabishana mambo ya uchumi na utalii. Wakenya ukiishi nao nje ya Africa wanakuwa karibu sana na watanzania kuliko hata waganda na waafrica wengine.
Tunacheza nao mpaka upatu, na pia wakenya wa jinsia nyingine ni mteremko sana kwa waTz.

Sasa kuhusu experience yako, hapo siwezi kukubishia but from my experience, tukiwa nje ya nchi zetu huwa tunahesabiana kama tupo karibu ukilinganisha na watu kutoka mataifa mengine.
 
Mi jana nimebaki mdomo wazi. Nilidhani naujua huu muungano ila kiukweli bado kuna vingi si vijui ila nadhani ni kwa kuwa pia havieleweki hata uwe mfuatiliaji kiasi gani.

Hivi ni muungano gani ambao upande mmoja una bendera, wimbo wa taifa na rais?

Hawa wachezaji waliozaliwa ughaibuni wanaoshawishiwa kuja kucheza huku kwa siku za karibuni ni kigezo au sheria gani inawafanya wachezee huku na sio Zanzibar heroes. Mfano michuano ambayo Zanzibar heroes wanaenda independently from Tanzania je hawa kina Kawawa wanaruhusiwa kucheza upamde wa Zanzibar heroes au Kilimanjaro stars?

Hili bango wangelishika Kilimanjaro stars wakihitaji Tanganyika itambuliwe hali ingekuwaje?

Hivi huu ni muungano kweli au ni nchi moja ina ilea nchi nyingine hadi hapo nchi inayolelewa itakapo kuwa na uwezo wa kujitawala itapewa uhuru wake kama ilivokuwa Tanganyika na Waingereza?

Hivi huu ndo muungano aliouunda Nyerere au kuna mambo yalikuja badilishwa yeye akiwa hajui, mbona kama alikuwa vizuri upstairs ila hii kazi ya mikono yake haieleweki kabisa?
 
Back
Top Bottom