Father of All
JF-Expert Member
- Feb 26, 2012
- 6,376
- 6,720
Kwa wanaojua kanuni za uharibifu, huwa hauachii mahali au kwenye kitu kimoja.
Nyerere aliwahi kuulinganisha na kula nyama ya binadamu. Ailaye haachi. Sijui ukweli wa dhana hii.
Hata hivyo, ukiwasikia wanaohanikiza tuvunje muungano, unapata wasiwasi nao.
Mfano, juzi mtu mmoja aitwaye Jussa alisikika akisema tuuvunje na kugawana mbao. Haya ni mawazo mafupi hasa kwa upande wa visiwani ambao watu wengi hujidanganya kuwa muungano ukivunjika watakuwa kama Dubai kwa vile wameonja harufu ya mafuta. Ni uchoyo na upofu mtupu.
Muungano ukivunjika, yafuatayo yanaweza kutokea:
Mosi, wapemba nao watataka kujitenga na waswahili weusi ili wawe karibu na ndugu zao waarabu ambao huwa wanawaabudia japo waarabu wanawaona kama watumwa wa kawaida.
Pili, Tanganyika italazimika kuwatimua wazenj wote ili warejee kwao na Zenj itajibu mapigo japo hatua hii itazua tatizo jingine.
Tatu, kama idadi ya Wazenji wote walioko bara watatimuliwa, Zanzibar haitakuwa na uwezo wa kuwatosheleza kimaisha hata kama ingekuwa na hayo mafuta ambayo haina uzoefu wa kuya-manage sawa na nchi nyingine za kiafrika.
Nne, Zenj itakumbwa na tishio la mapinduzi toka kwa migawanyiko yake ya asili baina ya waliofanya mapinduzi na waliopinduliwa ambavyo kimsingi, ndiyo sababu kuu iliyoisukuma kuungana na Bara.
Tano, Zenj itakuwa na tishio la usalama kutokana na kutokuwa na jeshi lake na vyombo vingine vya ulinzi. Hivyo, italazimika kuendelea kutegemea Tanganyika hata kama ni kinafiki.
Sita na mwisho, Zenj itatumia fedha nyingi kuagiza bidhaa toka Tanganyika katika fedha za kigeni jambo ambalo litaathiri vibaya uchumi wake.
Unaweza kuongeza madhara mengine na faida kama zipo.