Muuaji wa Mwangosi na kafara za kisiasa

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,782
699,224
Kijana mdogo aliyekuwa anaanza maisha yake akiwa na matumani na ndoto nyingi za kimaisha

Mke mzuri watoto wanaomjua Mungu nyumba gari na mali nyingine
Kwenye harakati hizo za kuyatafuta haya anaingia kwenye kazi ya upolisi, inawezekana kabisa halikuwa chaguo lake lakini ugumu wa ajira na njia ya kutimiza ndoto zake anakuwa hana jinsi

Misuguano ya kisiasa , utawala usio zingatia sheria kulindana, Ubabe wa mamlaka, kukosa weledi na amri za kukurupuka, visasi na rohombaya vimesabibisha
.Mauaji ya kijana mwanataaluma, baba wa familia
.Yatima
.Ujane
.Nguvu kazi ya Taifa kupotea

Lakini pia kwa maumivu mengi yenye kuumiza hisia yamemsababishia kijana aliyetekeleza mauaji kifungo cha miaka 15 jela ukiacha 4 ya kukaa mahabusu...Je kuna aliyeyakumbuka maumivu yake haya?

Wote waliomsababishia haya wako mtaani wanapeta huku wengine wakipandishwa vyeo YANI MIMI NIENDE JELA HALAFU WEWE UPANDE CHEO?
Visasi huwa na historia ndefu sana
 
Majuto aliyonayo anayajua Mungu tu nahisi anawaza kuanzia alipoingia depo ccp siku ya kwanza Na mabegi Yake anaimba Mimi kuruta Mimi kuruta anajisemea mwenyewe kwa nini nilichagua hii kazi kwa nini niwe Mimi kwa nini peke yangu kwa nini kwa nini zinakuwa nyingi katika maisha Yake maumivu aliyonayo Na majuto ni mengi sana. Kwenye maisha Mungu utumia matatizo kutufundisha Na kuwafundisha wengine Mungu anaweza kukuchagua wewe uwe katika matatizo ili wenzako wajifunze kutoka kwako. Naamini vijana wengi kama yeye kwenye taasisi mbali mbali watatumia hili tatizo lake kama somo jiepusheni Na miemko ya viongozi wenu kutaka kuonekana wanafanya kazi kwa kutumia mgongo wenu. Tujihadhari kufanywa kafara katika kazi zetu ili mabosi wapate sifa
 
Kipindi huyu kijana amekamatwa mlisimama kidete, achukuliwe hatua kali, Leo mnajifnya na HURUMA nae. Mngeazisha thread za huruma kipindi kile, kipindi mlileta picha za ushaid ili achukuliwe hatua

Tatizo ni watoa amri, sio watekelezaji! hili hulijui? ndio tulilalamika hatua zichukuliwe kwa watoa amri, huyo kaonewa.Hata wewe unajua.
 
ImageUploadedByJamiiForums1469682245.864280.jpg
 
Majuto aliyonayo anayajua Mungu tu nahisi anawaza kuanzia alipoingia depo ccp siku ya kwanza Na mabegi Yake anaimba Mimi kuruta Mimi kuruta anajisemea mwenyewe kwa nini nilichagua hii kazi kwa nini niwe Mimi kwa nini peke yangu kwa nini kwa nini zinakuwa nyingi katika maisha Yake maumivu aliyonayo Na majuto ni mengi sana. Kwenye maisha Mungu utumia matatizo kutufundisha Na kuwafundisha wengine Mungu anaweza kukuchagua wewe uwe katika matatizo ili wenzako wajifunze kutoka kwako. Naamini vijana wengi kama yeye kwenye taasisi mbali mbali watatumia hili tatizo lake kama somo jiepusheni Na miemko ya viongozi wenu kutaka kuonekana wanafanya kazi kwa kutumia mgongo wenu. Tujihadhari kufanywa kafara katika kazi zetu ili mabosi wapate sifa
Well said!!
 
Tatizo ni watoa amri, sio watekelezaji! hili hulijui? ndio tulilalamika hatua zichukuliwe kwa watoa amri, huyo kaonewa.Hata wewe unajua.
Eti kaonewa....!!! Amekuwa mbwa yeye kusema hana akiri ya jema na baya...
 
Nimeskia yule mpiga picha wa ile picha ya mnato ikionesha kuuwawa kwa Daid mwangosi nae amefariki,sijui kuna ukweli
 
Back
Top Bottom