Reality of gender logic and emotional dynamics

Reality of gender logic and emotional dynamics

Zemanda

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2021
Posts
10,999
Reaction score
23,499
Katika umri mdogo kijana anamtamkia binti maneno anayoumba kutoka katika akili yake na majibu ya binti yatashtua mapigo ya moyo ya kijana aidha kwa wasi wasi au mahaba.

Wakati wa umri mdogo kijana anaitazama ulimwengu kwa namna ya matarajio na kwasababu anakuwa mgeni na maisha huwa anajawa na hofu na wasi wasi kuanza safari ya Maisha pekee yake ndio maana huhitaji sana apate rafiki wa kudumu wa maisha.

Kama atapata wa kumuamini ambaye atamtamkia maneno kwa mfano" Jana niliota ndoto ya kutisha sana niliota dunia imesambaratika na haipo kama ilivyo sasa, uraia wote umefutika na dunia imekuwa kama imeanza upya kabisa, kitu cha kwanza nikajiuliza ni wewe upo wapi sababu nilishindwa kufikiria maisha bila wewe kwenye huo ulimwengu uliosambaratika nitaweza kuishi vipi". Maneno haya yakijibiwa na kauli kutoka moyoni kwa mfano "kweli umeota hivyo, ulifanyaje sasa? Usihofu hiyo ilikuwa ni ndoto tu katika haya maisha sitakuacha wala hata iweje wewe ni nusu yangu".

Kisha akaja kijana mwingine kumtongoza huyu binti na akamjibu si kwa ubaya ila kwa taarifa kuwa yeye kwasasa amechumbiwa tayari na yupo na anayempenda kuliko wakisubiria kuanza maisha pamoja kwa ridhaa ya wazazi hapo ndipo mwanzo wa furaha ya milele labda huyu kijana ageuke akili yake na kumuumiza huyu binti kwa uongo wa maneno yake.

Ndipo binti atakwenda kwa mwingine na mwingine na sipopata wa kumtuliza basi atageuka kuwa na moyo wenye machungu utakaowanenea mabinti wadogo historia ya maumivu ambayo itakuja kugeuka hukumu ya kusomewa vijana watangaza nia ya mapenzi ya dhati wasio na hatia wala madoa ya usaliti kwa mabinti wachanga wasiolijua wasemalo ila tu kusimamia ushuhuda wa historia za maumivu za waliowatangulia enzi na enzi kipindi maneno ya mapenzi yalidhaniwa kuwa na uhalali wa kuaminiwa pale yalipotamkwa kwa mara ya kwanza.

Na hawa vijana watabakia kuwa wahanga wa kuuliza ni wapi wamedanganya hatimae akili zao zinajaa maumivu ya kukataliwa na kujikuta wakisaliti adhima yao ya kuzaliwa nayo ya kuwajali na kuwapenda mabinti kwa lengo la kuambata nao maishani wakiwapa uhakika wa faraja ya kudumu maishani. Na sasa akili zao zitasikiliza mioyo yao ya maumivu ambayo itaziambia akili kujiandaa na maumivu zaidi kuliko upendo na mbinu ni kuwa kisirani kama sio mshambuliaji asiye na huruma kwa mabinti wachanga wasio na ufahamu kwa kutumia mbinu za kimkakati za kurubuni na kupumbaza akili hata isijue inalengwa kupelekwa wapi kwa raha za muda zinazofananushwa na faraja ya milele.

Maumivu huzaa maumivu, uongo huzaa kiza cha upofu wa uelekeo, maswali yasiyo na majibu hutengeneza majibu batili ya kujijibu katika upotofu. Mwishowe ni kuogopana sababu vijana na mabinti hawajuani, hawajuani sababu hawaelewani, hawaelewani sababu hawasikikizani, hawasikilizani sababu hakuna anayemhurumia mwenzake kwanza, hawahurumiani kwasababu kijana ameacha kumwambia binti ndoto yake ya upweke na ya kuogofya ya maisha yakusambaratika na hakujua binti yupo wapi hivyo akapatwa na hofu iliyochanganyika na simanzi na upweke. Na binti hajasikia hii story muda mrefu hadi amehisi kwenye huu uhalisia wa Maisha hakuna kijana anayemuota wala kuwazia upweke wa maisha bila yeye.

Can we heal and start over? [emoji25][emoji25][emoji25]
 
Of course we can heal and commence again our love journey.
 
Back
Top Bottom