Mutungirehi: mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?

Mutungirehi: mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?

Ilikuwa ni October 1994 ndipo Mutungirehi alipogaragazwa pale Nkrumah Hall. Soma headline ifuatayo: [UDSM wanaamriwa kuondoka kurudi makwao: {UHURU: November 07, 1994, pg. 1}].

Walioongoza kumtwanga Mutungirehi pale Jukwaani ni kweli mmemtaja Harold Mushi alikuwa Engineering. Mwingine ni Gasper Tracers aliyekuwa 3rd year Electrical Engineering. Huyu ninajua kuwa hadi 1998 alikuwa ni Engineer pale ITV ingawa sasa sijui yuko wapi.

Ila kuna moja wengi mnalisahau na hamlisemi. Wakati Mutungirehi anasulubiwa katibu wake wa DARUSO alikuwa Godwin Ngwilimi. Godwin alipoona Mutungirehi kaparamiwa na kuangushwa chini akachukua kiti na kumponda Harold Mushi ndipo fujo ikazidi...

Baada ya hapo wale vijana wa FOE second year wakati huo wakaenda mbele kufanya fujo...Umenikumbusha mbali sanaaaa.
 
Mkuu Royals tumekumbuka mbali kweli kweli! Naona Mutungi kaamua kuwa mfanyabiashara manake alikutana na Lyatonga akafanyiwa kitu mbaya!

Kimbunga kumbe tulikuwa pamoja, mnenikumbusha hiyo siku mambo tuliyofanya na jinsi kunji lilivyoendelea. Unamkumbuka Selestine Mushi? Naona siku hizi kawa mkurugenzi wizarani
 
Last edited by a moderator:
Baada ya hapo wale vijana wa FOE second year wakati huo wakaenda mbele kufanya fujo...Umenikumbusha mbali sanaaaa.

Yaani kuna vijana walioshiriki kumshusha huyo jamaa na kule FOE kaanza kumuita MUTUNGILAHELA aka Mnyamrenge..Siku hizi wengi ni Ma senior Engineers ukiwakumbusha wancheka sanaaaaa...kama John Peter...JP nk
 
Nakumbuka alimlaani mrema, wakati mrema anamfukuza uanacham kuwa "nakulaani ewe mrema, utaondoka tlp ukiwa ndani ya jeneza!
 
Bwana kajunju nashukuru kwa kufatilia habari za kyerwa kwa karibu , ninachotofautiana na wewe ni kuwa Mtungirehi kapita pengi siyo ubunge wa kyerwa tu . Huko madudu yake huyaongelei. Ni si sahihi kuwa watu wa kyerwa kuwa wanapenda pombe ndo wampigie kura mtu maana mara ya kwanza kashinda ubunge akiwa masikini zaidi kuliko alipogombea 2005 kama ingekuwa pombe asingepata hata hizo kura za kumpa ushindi maana uwezo huo hakuwa nao. kwenye Lugha hasa kinyambo ,kingereza na kifaransa anaweza sana na mie ningempigia kura kama uchaguzi ungenikuta katika eneo lolote kama tu anagombea na katagira

Isingiro! Dah! Salimia familia ya mzee Kahatano bana! bila kusahau kijana mtukutu Max! very long time! Ile ni Very potential location lakini ndio hivyo tena Magambas yameng'ang'ania 50yrs!
 
Mkuu Royals tumekumbuka mbali kweli kweli! Naona Mutungi kaamua kuwa mfanyabiashara manake alikutana na Lyatonga akafanyiwa kitu mbaya!

Benedicto Mutungirehi alisoma O Level Kahororo sekondari na kisha Milambo, KLF. Huko pia alishakuwa Kiranja Mkuu, na siku moja katika Mkutano na Mkuu wa shule, Mzee Msemakweli, akichangia hoja ilokuwa inapigwa danadana akasema: "Mama mmoja huko kwetu alikuwa analima shambani, akakaona kanyoka kadogo, Mume wake akamwambia waaue lakini Mama yule akasema wakaache maana ni kadogo hakana makosa ya Wazazi wake wanaowauma. Basi wakati wanavuna mazao msimu huo, huku kakiwa kamekua, kakamuuma Yule Mama kwenye kisigino. Akafa!" Hapa Mutungi alikuwa anasisitiza haja ya kumaliza matatizo yakiwa hayajachelewa. Toka siku hiyo wanafunzi wote walimfahamuna kweli alikuwa ni MPIGANAJI!
 
Huyu jamaa aliuzwa na MREMA kabla ya uchaguzi wa mwaka 2005,uongozi mzima wa chama chake TLP ulijiuzulu na kuingia CHADEMA Mrema kwa kuwa alikuwa anamuhitaji sana aliamua kupiga kambi na kuhakikisha anaharibu mpango wa yeye kuungana na wenzake hasa MWL Deus aliyekuwa mwenyekiti wake na Diwani,akiahidiwa na Mrema kumuachia uenyekiti wa TLP na kwa kuwa enzi hizo alikuwa level za kitaifa akaamua kucheza pata potea na kweli akapotea.Wengi naona wanakumbuka matukio ya DARUSO ila kuna siku Bungeni aliwahi kusema Ikulu inanuka kutokana na soko la feri kuna maneno alitumia kujenga hoja nadhani zingelikuwa zama za bunge hili tungesikia ''MUTUNGIREHI WALK OUT''
Kuhusu siasa bado ana nafasi kubwa sana katika siasa za Kyerwa hasa kutokana na udhaifu wa mbunge aliyepo tatizo la Ben kwa sasa ni kwamba alikumbwa na msukosuko wa uchumi hadi kupelekea kukosa kujiamini mbele ya jamii,ni moja ya wabunge walioingia bungeni wakiwa masikini nakuondoka wakiwa masikini vilevile.
 
JF kiboko,

Kuna mtu kanikumbusha habari za Mwl. Msemakweli wa Milambo High School. That school!
 
Isingiro! Dah! Salimia familia ya mzee Kahatano bana! bila kusahau kijana mtukutu Max! very long time! Ile ni Very potential location lakini ndio hivyo tena Magambas yameng'ang'ania 50yrs!

Salamu zimefika ,Max ni mwana CDM mzuri sana na ana cheo hapa .Isingiro ni wazima japo inarudi nyuma kiasi fulani
 
Hivi inamaana hajawa mwana JF? au ndo Kajunju?
 
Salamu zimefika ,Max ni mwana CDM mzuri sana na ana cheo hapa .Isingiro ni wazima japo inarudi nyuma kiasi fulani

Ngoja tujipange kuizindua Kaisho mpaka Murongo kamanda nimefurahi tunae mtu kutoka Kaisho akiwakilisha hapa JF direct from there! Utakuwa chemchem ya mabadiliko Kaisho.pamoja sana kamanda.
 
Hivi inamaana hajawa mwana JF? au ndo Kajunju?

si kweli kuwa mimi ni mtungireh,mawasiliano na mtungireh niliyapata kwa mtu waliyesoma nae. Karagwe nimefanyia kaz. Najua vijiji vyote ukianza na chamchuzi,kitwechenkura,igurwa,katanda nk.huyu jamaa nilikuwa napata story zake kwa jamaa waliesoma nae milambo..hasa mgomo aliouhasisi.nafikiri tusiwe wavivu wa maneno mengi.hebu mpigie cmu na atakalokwambia lilete hapa. Nawasilisha
 
Leo kaibukia kwenye lile Coalition kubwa la Ukawa kupitia Chadema.
 
Namtakia kila la Kheri Kamanda Mtungireh ... Zama zake sisi wengine tulikuwa bado O level pale Ilboru, Namkumbuka sana Advocate Kamara alivyokuwa anatusimulia manjonjo ya huyo kamanda... Well, zama zile bado System ilikuwa ya mfumo wa chama kimoja Zaidi, haki za binaadamu zilikuwa hazilindwi sana ... bado hajachelewa, ananafasi ya kuweka tofauti kwa jamii yake ya kitanzania ....
 
RockSpider,
Kazi hapa ni kwa wapiga kura wake kama wanajua kuwa huyu jamaa ni kifaa kweli.
 
Back
Top Bottom