Kwa wanangara na Tanzania kwa ujumla

mjsimon

Member
May 11, 2009
5
1
Usifanye makosa katika uchaguzi huu, wa serikali za mitaa

Ndugu zangu watanzania, awali ya yote napenda kuwasalimu, wakubwa Shikamoo na wadogo habari gani. Kwa wale ninaowazidi, watakuwa wameniamkia. Kwanza napenda kumshukuru Mungu muweza wa yote kwa kutufikisha siku ya leo ninapoongea na wewe kupitia maandishi haya.

Ama baada ya salamu hizo, naomba niongelee moja kwa moja hoja yangu juu ya uchaguzi wa Serikali za mitaa ambao utafanyika Jumapili tarehe 14/12/2014. Sasa leo bila woga wala kupepesa macho na bila kijali itikakadi ya chama chako, nimekuandikia maneno haya ili yawe msaada kwako na yakusaidie kufanya maamuzi sahihi siku hiyo ya uchaguzi na usiunge mkono chama cha mapinduzi. Maelezo haya yanawahusu watu wafuatao:-

1. Wapenda haki wote,
2. Wacha Mungu wote na mwisho,
3. Wapenda maendeleo wote wa nchi hii

Nakuomba usichague mgombea yeyote wa Chama Cha Mapinduzi kwa sababu zifuatazo:-

Mosi, kwa wapenda haki; Mpenda haki ni mtu apendaye haki itendeke kwenye jamii, hapendi kuona au hata kusikia mtu anaonewa, anadhulumiwa haki yake, anadhalilishwa, anafanywa duni na kubwa zaidi mpenda haki huyu hataki kushuhudia au hata kuambiwa kuwa binadamu mwingine amedhulumiwa uhai wake! Kwa maelezo hayo hapo juu CCM inakosa haiba na uhalali kwa wapenda haki kwani hakuna hata moja kati ya hayo ambayo CCM imeyafanyia kazi!

Uonevu, kama wewe ni mtanzania usiye na chembe ya unafiki utakubaliana na mimi kuwa chama hiki kimekuwa kikionea watu kwa kiwango cha kutisha na kusikitisha. Chama hiki na serikali yake vimekuwa mstari wa mbele kumdhibiti mtanzania wa kawaida asipate hata kupumua, kila akigeuka huku anakutana nao kwa namna nyingine. Wakati wao wakijimilikisha mali za umma na kujifanya miungu watu, mtanzania wa kawaida haruhusiwi hata kuuza juisi barabarani. Kwa mfano katika wilaya yetu ya Ngara, wananchi wengi wameonewa na serikali ya CCM imewaonea kwa kuwanyanyasa kwa kuwaita warundi, wengine wamepigwa mabomu kama huko Murukulazo, wengine wamekamatwa na kuwekwa ndani bila sababu yoyote, wengine wameuawa kama kule Mrubanga kata ya Mrusagamba. Wananchi wengi wameonewa kwenye kuchangishwa pesa eti ni kuchangia ujenzi wa maabala wakati pesa zilizoibwa na viongozi wa CCM na kutajwa na mkaguzi wa hesabu za serikali zilikuwa zinatosha kujenga maabala nchi nzima na kujaza vifaa muhimu bila kuchangisha wananchi ambao nao ni maskini.

Dhuluma, nani asiyejua kuwa CCM kwa kutumia kivuli chake chenye jina "serikali" ndiyo imekuwa mstali wa mbele kudhulumu haki za watu? Uporaji wa ardhi ya watanzania na kuwapatia wazungu, kwa kisingizio cha upanuzi wa miji na uwekezaji, Ubomoaji wa makazi ya watu bila hata ya taarifa na pia bila hata fidia. Ukiukwaji wa haki za binadamu, kama vile ubambikiziaji wa kesi bila sababu ya msingi, kuua raia wasio na hatia kama mwangosi na wengine wengi!

Udhalilishaji, nani anayepinga kuwa CCM na serikali yake haina udhalilishaji? Mfano mdogo tu ni namna halmashauri inapoenda kukusanya ushuru na kodi za leseni kwa mtutu wa bunduki madukani, wamachinga na mamalishe kukamatwa na kunyang'anywa mali zao. Mfano mzuri kwa Ngara wakati wa opereation ya kurudisha wahamiaji haramu, CCM iliwadhalilisha wananchi wengi ndugu zetu hasa wa upinzani kwa kuwaita wahamiaji haramu. Ndugu zetu wengi waliumizwa na kudhalilishwa vya kutosha.

Wote tunamfahamu mzee wetu Warioba aliyeteuliwa asimamie zoezi la kukusanya maoni ya wananchi ya kuandika rasimu, alipofanya hivyo aliishia kutukanwa matusi (siwezi kuyaandika hapa) kama mtoto mdogo na kuambiwa ni mnafiki na msaliti. Sasa jiulize kama wameweza kumdhalilisha Jaji mstaafu (mwanasheria mahiri) na waziri mkuu mstaafu, vipi kuhusu mimi na wewe?

Kama kweli wewe mtanzania ni mpenda haki basi kwa mifano hiyo michache utakuwa umeshajua ni kwa nini si busara kuchagua mgombea aliyepitishwa na CCM sababu ataendeleza uonevu, dhuruma na udhalilishaji.

Pili, kwa wacha Mungu; Mcha Mungu ni mtu ambaye anatenda mapenzi ya Mungu na kushika yale Mungu anayotaka yafuatwe. Huyu anatabia ya kutetea haki, ikiwa ni sehemu ya maadili ya imani yake. Ila yeye anakuwa na vitu zaidi ambavyo mpenda haki anaweza asiwe navyo, mfano mcha Mungu haamini katika ushirikiana anaamini katika Nguvu ya Mungu aliye hai. Haamini katika kulipiza kisasi, anaamini katika msamaha. Mcha Mungu anaamini katika kutenda mema na kuepuka kila jambo linalovuruga uhusiano wake na Mungu pia anapenda kuwa chanzo cha amani katika maisha ya watu. Kwa ujumla ni mtu mwenye hofu ya Mungu katika moyo wake.

Ushirikina, nani asiyejua kuwa CCM ni washirikina namba moja hapa nchini? Kwani hamkuona au kusikia wakati CCM ikiwaita wapiga ramli wote Mwanza ili kukinusuru chama baada ya kukataliwa na wananchi? Je hajawahi kutokea mganga wa jadi aliyedai kuwa yeye ndiye anayemlinda Rais bila bunduki na Rais hakukanusha? Lakini si hayo tu kwa mcha Mungu, licha ya kutoamini katika ushirikina pia yeye naye anachukia haki kutotendeka, uonevu, dhuruma na udhalilishaji! Ni mcha Mungu gani, Askof, Padre, Mchungaji, Mwinjilist, Shehe au ustadhi anayeweza kumpendeza Mungu kwa kuiba kura, kuwekea pingamizi za uongo, kushiriki katika kuhujumu uchaguzi usiwe huru na haki? Ni mcha Mungu gani atakubaliana na rushwa?

Hapa nataka pia nikufahamishe kuwa wachungaji, mashehe, mapadri, katekista na viongozi wote wa dini kuwa katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania haiwazuii kushiriki katika siasa na kuwaelimisha wananchi kuchagua viongozi watalaotenda haki wanaozuiwa kwa mijibu wa katyiba na sheria za nchi ni hawa. "Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ibara ya 113A inatamka wazi kuwa Itakuwa ni marufuku kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Jaji wa Mahakama Kuu, Hakimu wa ngazi yoyote kujiunga na chama chochote cha Siasa, isipokuwa tu kwamba atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii".

Pia watu wengine wanaotajwa kutoshiriki siasa ni katika ibara ya 147 (3) Itakuwa ni marufuku kwa mwanajeshi yeyote kujiunga na chama chohote cha siasa, isipokuwa atakuwa na haki ya kupiga kura iliyotajwa katika ibara ya 5 ya Katiba hii.

Hapo naamini pia umeelewa kuwa kama wewe ni mcha Mungu bila kujali dini yako na unataka kumpendeza Mungu, jiepushe na kuunga mkono CCM ambayo ndiyo chimbuko la dhuruma za kila namna hapa Tanzania.


Tatu, mpenda maendeleo; Mpenda maendeleo ni mtu anayetaka kuona jamiia yake ikibadilika kutoka katika hali duni ya maisha kuja kwenye mafanikio, kutoka kwenye uchache kuja kwenye wingi, kutoka kwenye unyonge kuja kwenye nguvu, kutoka kwenye umaskini kuja kwenye utajiri,nk. Mtu huyu hupenda aone rasilimali za nchi zikitumika vyema kwa manufaa ya umma. Huchukia ubadhirifu wa mali ya umma, rushwa na matumizi mabaya ya madaraka.

Ubadhilifu wa mali ya uma, nani asiyejua kuwa CCM ndiyo mama wa wabadhirifu wa mali ya umma? Richmond, EPA Meremeta, Buzwagi, Escrow, wanyama hai kupandishwa ndege, Meno ya tembo kwenda na ndege ya rais wa china. Kujimilikisha misitu kama ile ya Goyagoya na maeneo mengine. Pesa ambazo zingetumika kulipa walimu, waganga na watumishi wengine ili wawahudumie wananchi vizuri, zinachotwa na kutumiwa na wachache huku wakigawana mapesa ya umma kwa kuyabeba katika viroba, magunia, Rambo na rumbesa, pesa hizo za umma umma wa watanzania we=angezifaidi kama zingenunulia madawa hosptalini.

Rushwa, wapi kwenye serikali hii ya ccm utakwenda upate huduma bila kuzunguka mbuyu? Ofisi ya mtaa, kitongoji, kijiji, wilaya mkoa hadi taifa rushwa imetamalaki! Hata polisi, kuna msemo kuwa polisi unaingia bure lakini kutoka ni pesa. Rushwa imeenea kila mahali hata mahakamani, haki inanunuliwa.

Matumizi mabaya ya madaraka, mfano waziri mkuu kusema watu wapigwe tu, watoto wa vigogo kujazana kwenye taasisi za kiserikali ikiwemo benki kuu, kufungulia watu kesi za ugaidi ambazo si za kweli mfano Wilfred Rwakatare, kubambikizia watu kesi, hata wilayani kwetu Ngara, wananchi wengi wamefunguliwa kesi lukuki za kubambikiwa.

Sasa basi ndugu zangu watanzania kwa maelezo ya hapo juu, kama wewe ni mpenda haki, au mpenda maendeleo au mcha Mungu wa kweli hutadhubutu kuipigia kura mgombea yeyote wa CCM maana ataendeleza udharimu, uonevu, dhuruma na udhalilishaji. Kwa maneno yangu haya naamini kuwa CCM itapata kura za wasiopenda haki, wasiomcha Mungu (wacha shetani) na wale wasiopenda maendeleo.

Chakufanya: Siku ya Jumapili, Ukienda kuchagua kiongozi, piga kura ya ndiyo kwa mgombea wa CHADEMA au CUF au NCCR Mageuzi. Kama vyama hivyo havina mgombea hapo, mwone kiongozi wa Chadema wa eneo husika kwa maelekezo zaidi.

Ukimaliza kupiga kura, usiende nyumbani kulala, tembea umbali wa mita 100 kutoka kwenye kituo ulipopigia kura, subili matokeo. Usisahau kuwa CCM wamejipanga kuchakachua kura yako na kutangaza kuwa mgombea wao wa CCM ndiye ameshinda kumbe ni wizi mtupu.

Hitimisho. Usiichague CCM kwa manufaa na ya umma! CCM ni janga la kitaifa!

Mungu ibariki Tanzania, Mungu Ibariki CHADEMA, Mungu ibariki UKAWA.

Ahsanteni

Imeandikwa na John Malanilo, Bukiriro.
 

Attachments

  • Usifanye makosa katika uchaguzi huu kuchagua CCM.pdf
    343 KB · Views: 214
Uchaguzi ukishamalizika tu na matokeo kutangazwa operation kimbunga ya kutimua wahamiaji haramu waliobaki baada ya lile zoezi itafuata.nadhani wahusika wanajijua akiwemo mwandishi wa hili bandiko
 
Back
Top Bottom