Mutungirehi: mwanasiasa mahiri kazimikia wapi?

Royals

JF-Expert Member
Nov 19, 2011
1,466
378
Bandugu bapenzi,

Yule mwanasiasa mahiri na machachari katika upinzani wa kwanza kwanza yuko hai na kama yu hai yuko wapi kwa sasa na anajishughulisha na kitu gani?

Maana wakati ule alikuwa maarufu sana wakishirikana na kamanda Wilfred Rwakatare ambaye sasa yuko M4C.

Bandugu; Wenye kujua taarifa zake wazimwage hapa jamvini na walio na mawasiliano naye wamwambie siasa sasa ni M4C na kama anataka kurudi ulingoni basa amfuate Rwakatare kwenye chama makini.

#NYONGEZA #

HAKI YA MUNGU, MUNGU NI MKUBWA. 12.4.2015.
Wana jukwaa.
Leo furaha yangu ni kuona huyu bwana Benedicto amejitokeza tena baada ya kuwa mafichoni kwa muda mrefu.

Zaidi nafurahi sana kwa kuwa kaibukia akiwa kwenye Coalition kubwa ya Ukawa kupitia Chadema. Hii inaonesha jinsi ambayo jukwaa hili linavyoweza kujenga na kuimarisha mambo hata yaliyo na yasiyo kwenda sawa sawa.

Ni matumaini yangu kuwa ataibukia Bungeni tena kwa kupitia kwa wa piga kura wake na kwa uwezo wa Mungu.

Mungu ibariki Tanzania. Mungu ubariki Ukawa na Mungu ibariki Chadema.
 
Jamaa alikua kichwa sana, alikua alisoma linguistic. Moja ya vituko vyake, alisha uliza swali kwa makamu mkuu wa chuo UDSM enzi izo kwa kutumia mbwembwe na utaalamu wake wa lugha ya kiingereza. Mkuu wa chuo akashindwa kujibu na kulalamika muuza swali katumia vocabulary zisizoeleweka.
 
Nakumbuka kuna makala kwenye gazeti la Rai ilimhoji kuhusu Kikwete wakati wa kampeni za uraisi 2005 nanukuu maneno yake

'wakati mwingine ikiandikwa inakuwa kama ilivyoandikwa ,nimefuatilia sana historia ya Kikwete kuanzia utendaji wake au hata pengine kuna hotuba aliyowahi kutoa iliyofurahisha watu sana,sijaiona.

Ninachokiona ni kwamba Kikwete atakuwa Raisi wetu basi'.

Nayakumbuka sana haya maneno yake Mtungirei.
 
Jamaa alikua kichwa sana, alikua alisoma linguistic. Moja ya vituko vyake, alisha uliza swali kwa makamu mkuu wa chuo UDSM enzi izo kwa kutumia mbwembwe na utaalamu wake wa lugha ya kiingereza. Mkuu wa chuo akashindwa kujibu na kulalamika muuza swali katumia vocabulary zisizoeleweka.
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.
 
toka atenguliwe kapotea kabisa. unaweza ukadhani wamemtengua mpaka kichwa!
 
Unakumbuka alipotolewa
high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana,
watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye
stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.

ilikuwa 1994!
 
alibishana na mrema,,akidhan siasa za vyuon ni sawa na za jukwaan mtaan,,,mrema alimbeba akapata ubunge,,akajaa kichwa,,,akaanza kung,ang,ania siasa za kitaifa hali hana mizizi imzra jimboni,,,,hili limewakumba wengi sana,,,wengine wamefufukia cdm ,,lakini bado ni ngumu ukisha haribu japo waweza kujipanga,,,,hata cdm,,,wanatakiwa wawajenge vijana kuwa na mizizi si tu kulipukia mihemko ya siasa za kitaifa,,,zinaleta kiburi na kuanza kupimana ubavu,,,na manguli,,,ukidondoka husimami tena,,,,vyema kuwa mjuzi wa kuzisoma alama za nyakati,,,na kuepa mihemko,,,,,,jazba,,na ujuaji,,,,,,busara ,,hekima,,,tahadhari zen kanyaga twende,,,,:pray2:
 
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.

Hilo tukio sitakaa nilishau, aliposhushwa toka kwenye stage, jamaa walianza kumshindilia mangumi na mateke. Mimi nilikuwa fresher enzi hizo, niliogopa sana maana nilijua atauwawa--alikuwa anapigwa kama kibaka---namuona live mbele yangu. Bahati yake, watu waliokuwa mbali walianza kutupia viti kumpiga, makamandoo wa FOE wakamuachia wakiogopa kupigwa viti--ndio mwanya wa maswahiba wake kumnyakua na kumkimbiza. Nilivyoona, ile ilikuwa kifo chake aisee! He is very lucky!
 
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.

Ilikuwa mwaka wa masomo 1994/1995. Alivutwa TAI, nusura imdhuru. Na kuanzia hapo mtu akikabwa tai watu husema "Tumemtungirehi"! Yaani MTUNGIREHI inakuwa KITENZI!
Alishawahi kuwa Mbunge wa Kyerwa na alikuwa mchangiaji hodari wa hoja sana Bungeni!
 
Duh mmenikumbusha hiki kichwa.niliongea nae sept 2007. Aliniambia kuwa" kikwete lilikuwa chaguo la mungu,watu walioteshwa kuwa,kuwa huyu ndie atakuwa rais wa kupeleka nch wananch wanapopataka.licha wa wana wa israel kuwa mazinifu kwa mungu. Mungu alimtuma musa awaongoze toka utumwani" maneno kwa tafsiri yake alisema kikwete na ccm yake kuwa mafisad, jk ndie ataleta mpasuko mkubwa ccm atimae watoke madarakani. Kuhusu mrema,alisema mara nying huwa hajui kupanga la kuongea linalokuja ndilo anaropoka. Kwa sasa ameokoka. Ameshawishiwa sana kujiunga cdm naskia bado amegoma ingawa wanasema ata yeye anakubali cdm wana strategy kali. Jimbon kyerwa niliwai kwenda na kuongea na wananchi wa kule. Wanamkubali sana ila unavyojua watz wengi wanamhusudu mtu anayewaibia. Kahawa zao zinanunuliwa na mbunge wao.waliniambia eti anawajengea chuo cha ualimu.nilivyouliza kama watasoma bure?walibaki midomo wazi. Ni mtu muhim wa kuleta mabadiriko ila sasa kinachomsubilisha mimi na wewe hatujui
 
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.
Ni mwaka 1993 kwa uhakika maana ndio kwanza najiunga chuo nikakutana na hzo siasa za Daruso hali iliyopelekea chuo kufungwa
 
Unakumbuka alipotolewa high table Nkrumah hadi akupoteza kiatu, jamaa alikuwa mkorofi sana, watu wanamvuta aondoke yeye akashikilia meza kidogo aanguke nayo kwenye stage, i think it was 1991 or 92 kama sikosei.

Duh mkuu Feedback huko umeenda mbali. Ilikuwa first term ya academic year ya 1994/95! Tulimpandia pale juu na kumvua tai. Baada ya kutawanyika akaja na press Release ikiwa na maneno maarufu yaliyosema ".... it will cost you nothing to be procedural.."

Alipokuwa Mbunge nilikutana naye Dodoma alikuwa mlevi wa hovyo mno. Tuliongea kwa kina alikuwa na maono kuhusu jimbo lake la sijui kyelwa!
 
Last edited by a moderator:
Bandugu,
Wachangiaji wote ni wsle waliosoma naye zamani. Ambaye ameonana nayee karibini ni Kajunju 2007. Je hskuna waliye karibu naye ili wamstue kusoma uzi huu ili ajibu hoja hapa kueleza yuko wapi na nini mustakabari wake kisiasa?. Maana ninavyomfahamu ksma angekutana na bunge la sasa basi ingekuwa ni hatari kwa msgamba maana timu ya upinzani ingekuwa nk moto wa kuotea mbaali.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom