Kimbunga
Platinum Member
- Oct 4, 2007
- 14,941
- 9,947
Hilo tukio sitakaa nilishau, aliposhushwa toka kwenye stage, jamaa walianza kumshindilia mangumi na mateke. Mimi nilikuwa fresher enzi hizo, niliogopa sana maana nilijua atauwawa--alikuwa anapigwa kama kibaka---namuona live mbele yangu. Bahati yake, watu waliokuwa mbali walianza kutupia viti kumpiga, makamandoo wa FOE wakamuachia wakiogopa kupigwa viti--ndio mwanya wa maswahiba wake kumnyakua na kumkimbiza. Nilivyoona, ile ilikuwa kifo chake aisee! He is very lucky!
Duh mkuu TzPride kumbe nawe ulikuwepo? Kumbe ulikuwa fresher? Haya maneno unayosema kwamba ulioogopa kuna mtu nilimsikia anayaongea pale hall five, nadhani ni wewe! Mimi enzi hizo nilikuwa mwaka wa tano pale chuoni! Baada ya hapo ikaja ile adhabu ya INTIMIDATION basi watu wengine wakasimamishwa! Kuna watu walisoma FOE miaka 6.
Last edited by a moderator: