Haaaaa haaaa! JK ni msanii, alikuwa anatest zari! Kama ana nia njema asingepeleka watoto kuuchapa usingizi ili kukaba nafasi za watu wengine wakati wa kuchangia Muswada wa Katiba Mpya! Sasa hivi atakuja kivingine, mtapinga kisha anaondoa hoja tena, mara 2015 hii hapa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inachakachua matokeo, then hadi 2020!
Hata kama wamejaribu kupima joto lakini hilo la kuchelewesha mchakato wa kupata Katiba mpya ndio katika mbinu zao...kuchelewa kupatikana katiba yenye kukubalika na wananchi na kila mbia ni tija kwa CCM.
Wanaofurahia muswada kuondolewa wana haki ya furaha yao, muswada ni mbovu. lakini pia hatupaswi kusahau hii janja ya kuchelewesha mchakato. Na kila muda unavyoyoyoma, 2015 inakaribia. Tunaweza kuingia uchaguzi mwengine bila ya katiba mpya na bila Muundo mpya wa Muungano.
CCM ni wazuri kwa kufunga magoli, Upinzani ni wazuri kwa kupiga chenga!!!