Muswada wa Katiba waondolewa kinyemela!

Haaaaa haaaa! JK ni msanii, alikuwa anatest zari! Kama ana nia njema asingepeleka watoto kuuchapa usingizi ili kukaba nafasi za watu wengine wakati wa kuchangia Muswada wa Katiba Mpya! Sasa hivi atakuja kivingine, mtapinga kisha anaondoa hoja tena, mara 2015 hii hapa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inachakachua matokeo, then hadi 2020!

Hata kama wamejaribu kupima joto lakini hilo la kuchelewesha mchakato wa kupata Katiba mpya ndio katika mbinu zao...kuchelewa kupatikana katiba yenye kukubalika na wananchi na kila mbia ni tija kwa CCM.

Wanaofurahia muswada kuondolewa wana haki ya furaha yao, muswada ni mbovu. lakini pia hatupaswi kusahau hii janja ya kuchelewesha mchakato. Na kila muda unavyoyoyoma, 2015 inakaribia. Tunaweza kuingia uchaguzi mwengine bila ya katiba mpya na bila Muundo mpya wa Muungano.

CCM ni wazuri kwa kufunga magoli, Upinzani ni wazuri kwa kupiga chenga!!!
 
Watanzania ni wa ajabu sana , yani nyie hamuoni sasa kibao kimegeuka yani yani ya kwamba serikali ndo wanahitaji katiba na wananchi wanaipinga.? teh teh teh

sina mbavu kwa kweli.
 
Wana bodi,

Hatimaye serikali imeuondoa kinyemela ule muswada Tata wa uundaji wa tume ya kukusanya maoni kuhusiana na katiba mpya. Muswada huo sasa hautawasilishwa tena kama ulivyopangwa awali na badala yake, utawasilishwa kikao cha mwezi Juni.

Habari hizi ni kwa mujibu wa souce ya 'kuaminika'

Hata hivyo 'source' huyo hakunipa sababu za serikali kuuondoa muswada huo ila kwa maoni yangu,

  1. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu, hivyo imesikia kilio cha waliokwisha toa maoni na ikakubali kuyazingatia.
  2. Hivyo muswada umerudishwa ili kufanyiwa marekebisho ya muhimu kiwemo kujumuisha michango ya wadau
  3. Utakapoletwa tena hiyo mwezi Juni, utakuwa ni kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
  4. Hii inamaanisha hata zile siku mbili za bunge kuendelea kukutana mjini Dodoma, siku ya Jumatatu na Jumanne ijayo kwa ajili ya kupokea maoni ya waheshimiwa wabunge, sasa hazitakuwepo, hivyo kikao hiki cha bunge kitamalizika rasmi siku ya Ijumaa.
  5. Pia kunauwezekano serikali imesoma dalili za nyakati kwa kuangalia kama maoni ya watu wa kawaida yametoa cheche vile, jee hayo ya wabunge si ndio yangewasha kabisa moto na hata kuulipua ukumbi wa bunge?!.
  6. Uthibitisho wa kuondolewa kwa muswada huu, utawajia soon!
Pasco.

watavua magamba mpaka watapakiza mifupa!!!
 
unampongeza kwa lipi?ebu weka hapa JF wapi anastahili pongezi?kwa kusingizia udini huku akijua ufisadi ndio uliompa ile 61% iliyochakachulika?
JK hana nia ya TZ kuwa na katiba mpya inayokidhi haja za makundi yote.Hapa kabanwa na hasa anakimbia kivuli cha CDM

Naungana na wewe merytina, sioni kama jk anastahili kupongezwa kwa lolote atakalofanya sasa hivi, hii ni kwa sababu anayoyafanya alitakiwa kuwa ameyafanya siku nyingi tu huko nyuma, isistoshe hayafanyi kwa sababu anapenda kuyafanya, anafanya kwa sababu hana option. Ni msukumo kutoka kwa wananchi, mbona huo mswada alishaona poa tu? kama sio reaction ya peoples power watu wangepeta na ingekuwa business as usual.

halafu niwakumbushe, jk hayuko hapo kujifunza kazi, yuko hapo kutimiza yale aliyoahidi kufanya pindi akipewa ridhaa na wananchi (ambayo hakupewa, aliipora) kwa hiyo acheni kumpongeza, mara ooh amefanya maamuzi magumu!! mnamsifia mtu kwa kutimiza wajibu wake tena baada kusukumwa sana. he has waisted a lot of our time, and he is too late as well.
 
Kama ni kweli, naipongeza Serikali, hasa Mh. Kikwete: kimsingi Rais anayelipenda Taifa lake hutazama mbele (miaka 200) zaidi na wala si miaka miwili. Dunia ya leo hakuna haja ya kuficha mambo.Tuwaache watu waamue namna wanavyotaka taifa lao liwe.

Boss, Mkuu pasko hapa si ametuambia umeondolewa kinyemela meaning kimya kimya...huo uwazi unaoongelea uko wapi? eti miaka 200...a serious joke...huyu jamaa hata wiki moja mbele haoni chochote we waongelea 200yrs! Na kama anaona mbali hakuona huo mswada mbovu ever na akaukacha juu kwa juu. Ona sasa ulivyo waumbua, tena si kuwaumbua tu but umbua BIG TIME! Vitu kama hivi ndo vinawacost then baadae wanakuja kulalamika ni Jamii forums ndo wabaya.
 
Ni vigumu kujua kama wameutoa au haukuwepo kwenye ratiba kwani hii ndiyo taarifa pekee iliyotolewa na Bunge bila ratiba
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
BUNGE LA TANZANIA
__________
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
_____________
Katibu wa Bunge anautangazia umma kuwa,
Mkutano wa Tatu wa Bunge la Kumi utaanza
tarehe 5 Aprili, 2011 Mjini Dodoma.
Imetolewa na:
Idara ya Habari, Elimu kwa Umma
na Uhusiano wa Kimataifa
DAR ES SALAAM
1 Aprili, 2011
 
Kama umeondolewa si kwa sababu hizo Pasco; Ila hizi zifuatazo:

a. Maandamano ya kitaifa ya Chadema ya tarehe 16 yangeporomosha juhudi zote za kujivua gamba
b. Wametambua kuwa mswada huu ulikuwa ni miongoni mwa miswada mibovu kabisa kuwahi kuandikwa na watu wenye akili. Na binafsi naamini unapita kwa ubovu ule mswada wa gharama za uchaguzi ambao wengine tulipinga na wengine wakajaribu kuutetea.

Vyovyote vile ile ilivyo wamesoma alama za nyakati ..

Heshima yako Mzee, I salute sana...nilitaka kuongeza hapo, c muswada wa gharama za uchaguzi tu, unakumbuka juu ya ule muswada wa Baraza la Usalama uliokataliwa mwaka jana bunge la Februari...ulipingwa takribani na wabunge wote makini huku wakifuatwa na wabunge wengi wengine 'wabovu'. Nakumbuka mchangiaji wa kwanza alikuwa Brigedia General Hassan Ngwilizi, akapiga vibaya sana kuwa muswada wa hovyo watu wanandaa kikundi kinachoweza kumpindua rais.

Waziri mhusika by then alikuwa msema hovyo, mama wa mipasho, Sofia Simba. Kwa kujua kuwa muswada wa hovyo, hawakuupitisha katika kamati husika ya ulinzi, usalama na mambo ya nje, ambako kulikuwa na wataalam ambao wangeweza kushauri mabadiliko ya msingi kwani ulihusu usalama na ulinzi.

Wakaupeleka kamati ya katiba, sheria na utawala chini ya G. Lubeleje, ambaye nilimshuhudia nje ya ukumbi wa bunge akiwayawaya tu baada ya muswada kukataliwa naye akisema hajui kwa nini uliletwa katika kamati yake. Baadae ilikuja semekana kuwa (bada ya kukataliwa bungeni na kurudishwa serikalini, ufanyiwe marekebisho makubwa, ikishauriwa sasa upelekwe katika kamati inayaohusu) haukupelekwa kule kwa sababu 'kulikuwa na wabunge wajuaji'

Ulikuwa muswada wa hovyo sana pia kuwahi kuandikwa pia kupitishwa katika ngazi zote mbili za watu wenye akili, technical commitee ya makatibu wakuu na baraza la mawaziri ambalo mwkiti wake ni rais...baada ya kuandikwa na wataalam wa sheria katika kitendo cha uandishi wa miswada katika ofisi ya CAG.
 
Ngoja niende zangu jukwaa la chini kabisa. Maana nimechoka kusikia habari za JK.... zinaudhi na kuchusha.
 
Hata kam wameuondoa maandamano yako palepale jumamosi,sababu ziko nyingi
1.Katika sarakasi yao ya kujivua gamba wamekiri kwamba kuna mafisadi ndani ya chama chao,umefika wakati sasa tushinikize serikali iwafungulie mashitaka hao waliokubaliana nasi kuwa ni mafisadi,kama ni wasafi mahakama ndio itadhihirisha hilo
2.Maisha bado ni magumu kwa kila mtanzania hivyo tushinikize hatua mahusi zichuliwe.
3.Watuthibitishie kama Al-hadaiwi kama wanamlipa au la.Waseme wazi,mi nafahamu wameogopa peoplez power.Wananchi tuna nguvu bana tumewabania kujilipa chama chao hela zetu.Hatudanganyiki.MAANDAMANO YAKO PALEPALE,
 
Pasco nadhani hujawahi kuwa katika maandamano ya Chadema. The anger from umma is greater than kumbukumbu ya risasi. Serikali isingethubutu kuwanyika kibali kwa sababu wanajua madhara ambayo yangetokea. Na chadema wasingeacha kuandamana eti kwa sababu wamenyimwa kibali

On a broader look, usisahau kwamba mabadiliko yanayotokea sasa hivi ya serikali kutii amri ya wananchi siyo kwa sababu wanapenda kuonekana wasikivu bali kwa sababu bakuli linatembezwa barabarani kwa ajili ya bajeti ijayo. Anayetembeza anarudisha bakuli jioni likiwa tupu au pungufu na walivyozoea miaka iliyopita.

Remember my words wafadhili watakapotangaza mchango wao kwenye bajeti ijayo. Impact ya Arusha is more than we think of, iko kwenye bajeti, kwenye mabadiliko yanayotokea sasa hivi ccm na serikalini, n.k
muhosni, hii connecting the dots ya maandamano na bakuli, ndio naipata kwako!. Inawezekana kila jema litakalofanyika kwa sasa, ni kubembelea bakuli!
 
kwenye website ya CCM wameandika haya:

KUHUSU MUSWADA WA SHERIA YA KUREKEBISHA KATIBA

Halmashauri Kuu ya Taifa, katika kikao chake ilipata fursa ya kupewa maelezo juu ya yaliyomo ndani ya Muswada wa Sheria ya Kuanzisha Tume ya Kuratibu Mchakato wa Mabadiliko ya Katiba na kuazimia yafuatayo:-

(i) Wananchi waelimishwe kuhusu madhumuni halisi ya muswada huu, kwamba madhumuni yake ni kuweka taratibu zitakazotumika katika kukusanya maoni ya wananchi juu Katiba wanayoitaka. Huu si Muswada wa Katiba yenyewe.
(ii) Muswada huo utafsiriwe kwa lugha ya Kiswahili ili kuwawezesha wananchi wengi kuuelewa na hivyo kuwa katika nafasi nzuri ya kutoa maoni.
 
Kama umeondolewa si kwa sababu hizo Pasco; Ila hizi zifuatazo:

a. Maandamano ya kitaifa ya Chadema ya tarehe 16 yangeporomosha juhudi zote za kujivua gamba
b. Wametambua kuwa mswada huu ulikuwa ni miongoni mwa miswada mibovu kabisa kuwahi kuandikwa na watu wenye akili. Na binafsi naamini unapita kwa ubovu ule mswada wa gharama za uchaguzi ambao wengine tulipinga na wengine wakajaribu kuutetea.

Vyovyote vile ile ilivyo wamesoma alama za nyakati ..

Nakubaliana na wewe huenda wamesoma, alama za nyakati na kujikuta hawajajua cha kufanya na hivyo kujipa muda kuweza kuzielewa zaidi. Tutathibisha hilo pale watakapoandika mswada mwingine na kuuleta. Ila kama wamefanya hivi ili kuutafsiri kwa kiswahili lakini contents zikawa zilezile basi wajue kuwa ni bora kukaa kimya kuliko kuliingia hili likitu huku moyoni hawalitaki, na kwa kuwa wameishayavulia nguo hawana budi kuayaoga sasa. Liwike lisiwike kutakucha tu. Walijaribu ku-test water depth na kujituta wanazidi kudidimia bila kujua mwisho wa kina ni upi, wameamua kutoka bila kuwa na majibu kamili.

Last edited by a moderator:
Wana bodi,

Hatimaye serikali imeuondoa kinyemela ule muswada Tata wa uundaji wa tume ya kukusanya maoni kuhusiana na katiba mpya. Muswada huo sasa hautawasilishwa tena kama ulivyopangwa awali na badala yake, utawasilishwa kikao cha mwezi Juni.

Habari hizi ni kwa mujibu wa souce ya 'kuaminika'

Hata hivyo 'source' huyo hakunipa sababu za serikali kuuondoa muswada huo ila kwa maoni yangu,

  1. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu, hivyo imesikia kilio cha waliokwisha toa maoni na ikakubali kuyazingatia.
  2. Hivyo muswada umerudishwa ili kufanyiwa marekebisho ya muhimu kiwemo kujumuisha michango ya wadau
  3. Utakapoletwa tena hiyo mwezi Juni, utakuwa ni kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
  4. Hii inamaanisha hata zile siku mbili za bunge kuendelea kukutana mjini Dodoma, siku ya Jumatatu na Jumanne ijayo kwa ajili ya kupokea maoni ya waheshimiwa wabunge, sasa hazitakuwepo, hivyo kikao hiki cha bunge kitamalizika rasmi siku ya Ijumaa.
  5. Pia kunauwezekano serikali imesoma dalili za nyakati kwa kuangalia kama maoni ya watu wa kawaida yametoa cheche vile, jee hayo ya wabunge si ndio yangewasha kabisa moto na hata kuulipua ukumbi wa bunge?!.
  6. Uthibitisho wa kuondolewa kwa muswada huu, utawajia soon!
Pasco.

Hapo kwenye red, vijana wenzangu kooote nchini hadi hapo kusimama kwetu kidete kumezaa matunda. Na hata tarehe ikisogezwa vipi SUALA LA KATIBA MPYA wala tusiilazie damu hata tone hivyo bado nasi tuendelee na ule ule mpango wa kuelimishana pamoja na vijana wenzetu ha kule vijijini ili kila mmoja wetu aelewe haki yake kuongoza na kuamua mambo ya kuundwa kwa katiba mpya bila serikali kutuingilia kwa namna yoyote isipokua tu serikali kazi yake itabakia tu ya ku-facilitate mchakato mzima kifedha na ulinzi n usalama basi!!!.
 
nimeamini JK anaendesha nchi kwa kuogopa kivuli cha CDM
wanainchi chochote tunachotaka kwa sasa tunaweza JK hana ubavu wa kukataa.

Tukidhamiria kwa dhati hata Spika wa BUNGE ataambiwa na JK ajiuzuli.

JK ANANIACHA HOI, kwa sasa ameweka wazi ni ufisadi uliompa 61% na sio udini kama alivyowadanganya jamaa zake -(alikuwa akimjibu Sofia Simba :source Raia mwema.)
dada naona haujui mshind wa uraic ktk uchaguzi ulopita
 
Kama umeondolewa si kwa sababu hizo Pasco; Ila hizi zifuatazo:

a. Maandamano ya kitaifa ya Chadema ya tarehe 16 yangeporomosha juhudi zote za kujivua gamba
b. Wametambua kuwa mswada huu ulikuwa ni miongoni mwa miswada mibovu kabisa kuwahi kuandikwa na watu wenye akili. Na binafsi naamini unapita kwa ubovu ule mswada wa gharama za uchaguzi ambao wengine tulipinga na wengine wakajaribu kuutetea.

Vyovyote vile ile ilivyo wamesoma alama za nyakati ..

Mnachezewa akili tu,mswada wa tume ya katiba na hati ya dharura wapi na wapi....wameshapima upepo na upepo umepimika...wanajifanya wajuaji sana hawa,ila this time kila engo tuwe nao tu
 
CDM sasa ndio inayoongoza nchi tunachotaka ndicho Serikali ndicho itakacho fanya hakuna mjadala ktk hilo.
Kama ZNB walidiliki kuuchana mbele ya mwakilishi wa rais (Waziri 6) na mwakilishi wa tume ya kukusanya maoni ni dalili tosha kuwa mambo mbele ni magumu
 
Kitu pekee ninachoweza kusema ni kuwa "Sikio la Kufa Halisikii dawa." Ukweli ni kuwa CCM imechoka, au ni wachovu tayari. Wamekosa uhalali wa kuwaongoza Watanzania. Iko haja ya kurekebisha sheria za uchaguzi haraka, raisi kulivunja bunge na kuitisha uchaguzi mkuu. Patakapobakia tutamaliza wenyewe.
"Enough is Enough".
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom