Muswada wa Katiba waondolewa kinyemela!

Yes...hali hii ndiyo ambayo imekuwa imekuwa ikililiwa tangu 'time immemorial'...naona sasa taratibu tunaanza kubadilika.
Kama kujivua Gamba kutainclude mambo ya muhimu kama haya yanayogusa wananchi, basi bora wajikwangue Gamba lote!
 
Kama kweli umeondolewa, nadhani walioshiriki kuuandaa mswada huo ni wale wale waliosema" Lazima Deni la Dowans lilipwe haraka" baadaye ikaja kuonekana kuwa hakuku na sababu za msingi kulipa deni hilo. Kwa makosa hayo mawili tu ya kuiabisha serikali yana tosha kuwatimua kazi wahusika.

Raia Mwema Inaripoti:

...akizungumza na Kamati Kuu ya CCM, Werema alieleza kwamba hakukuwa na sababu ya kuuweka muswada huo ktk lugha ya kigeni amabayo watanzania wengi hawaijui.
Inafahamika pia kwamba Jaji Werema alisema matatizo mengi ya muswada huo yametokana na uongozi (wa kisiasa-waziri) kutokutaka kusikiliza ushauri wa wataalamu......

.....Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete, aliagiza mabadiliko kadhaa yafanyike ikiwamo lugha ya muswada wenyewe.

Maswali Yangu
1. Werema kama alijua hili alimwambia Rais
2. Kama hakumwambia kwa nini alisubiri kwenda kuongea kwenye Kamati Kuu ya CCM - je nia ni kutaka kumfedhehesha Rais?
3. Kama Rais aliambiwa alichukua hatua gani?
4. Je Rais aliona madhaifu ya muswada na akaona ni nafasi ya kucheza "Super hero"??
 
Kama mwanasheria nilikuwa najiuliza Kwanini Muswada huo upelekwe Bungeni kwa hati ya dharula?

Kwani ukizingatia Katiba hiyo ndio mhimili mkuu na ndio inaoshika mustakabali mkuu wa ustawi na maendeleo ya nchi sasa kwanini upelekwe haraka haraka huo mchakato wake.

Kwa kweli ilinisikitisha sana kwani najua fika ungekuja kuleta malalamiko mengi sana kama ulivyokuwa muungano. Kwani hata Makubaliano ya muungano wa Tanganyika na Zanzibar yalipekwa bungeni kwa hati hiyo na kuwanyima wananchi muda muafaka kuyajadili na kufikia maamuzi na athari zake mpaka leo zinaliumiza tanzania.

Ningeshauri Serikali iondoe hiyo hati ya Dharula na kuupeleka kama muswada wowote ule ili wananchi wapate nafasi kuujadili na kutoa mapendekezo yao.

Kwani huo ndio mwongozo mama na unashikilia ustawi na maendeleo ya Tanzania.

Nasriyah Saleh Al Nahdi.
Doha
 
Wana bodi,

Hatimaye serikali imeuondoa kinyemela ule muswada Tata wa uundaji wa tume ya kukusanya maoni kuhusiana na katiba mpya. Muswada huo sasa hautawasilishwa tena kama ulivyopangwa awali na badala yake, utawasilishwa kikao cha mwezi Juni.

Habari hizi ni kwa mujibu wa souce ya 'kuaminika'

Hata hivyo 'source' huyo hakunipa sababu za serikali kuuondoa muswada huo ila kwa maoni yangu,

  1. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu, hivyo imesikia kilio cha waliokwisha toa maoni na ikakubali kuyazingatia.
  2. Hivyo muswada umerudishwa ili kufanyiwa marekebisho ya muhimu kiwemo kujumuisha michango ya wadau
  3. Utakapoletwa tena hiyo mwezi Juni, utakuwa ni kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
  4. Hii inamaanisha hata zile siku mbili za bunge kuendelea kukutana mjini Dodoma, siku ya Jumatatu na Jumanne ijayo kwa ajili ya kupokea maoni ya waheshimiwa wabunge, sasa hazitakuwepo, hivyo kikao hiki cha bunge kitamalizika rasmi siku ya Ijumaa.
  5. Pia kunauwezekano serikali imesoma dalili za nyakati kwa kuangalia kama maoni ya watu wa kawaida yametoa cheche vile, jee hayo ya wabunge si ndio yangewasha kabisa moto na hata kuulipua ukumbi wa bunge?!.
  6. Uthibitisho wa kuondolewa kwa muswada huu, utawajia soon!
Pasco.

Pasco hebu fuatilia hiyo source yako vizuri kujua nini kilichoondolewa kati ya haya mawili.
1. Muswada umeondolewa bungeni kinyemela - AU
2. Hati ya dharura ndio imeondolewa ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kuudadavua muswada ili maamuzi yake yafanyike bunge la Juni na sio hili la sasa.

Please verify ili mjadala uwe mnono zaidi
 
Kwa ninavyofahamu kutokana na umuhimu wa Kupatikana kwa katiba , nafikiri wataondoa Hiyo hati ya dharula ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kuujadili mchakato mzima na sifikirii kama watauondoa muswada mzima.

Ok That is Tanzania, anything can happen.
 
Uko sawa kabisa mwanakijiji,
Lakini napendekeza CHADEMA waendelee na maandano na kuuelimisha UMA
Kwamba Katiba nzuri itapatikana kama kutakuwa na mchakato mzuri, hivyo product ya sheria hiyo ni
kiini cha Katiba waitakayo, hivyo Watanzania wote, kwa uwezo wao wote walionao, na nia yao ya katiba,
na kwa nguvu zote walizonazo waendelee kuipigia kelele serikali wakati inaedit muswada huu ili
walete muswada na hatimaye sheria na chombo cha kusimamia uandikaji wa Katiba kitakachokidhi
mahitaji yao.
 
Tatizo la kwanza kabisa lilikuwa ni serikali ya ccm kudandia hoja isiyokuwa yao. Hoja ya katiba mpya ilikuwa ya cdm, haikuwa ya ccm. Walipoidandia walifanya haraka haraka ili kujitafutia umaarufu bila kuwa na mpango mzuri ulioandaliwa kikamilifu; ndiyo maana walifanya kidharura dharura tu.
Kwa kuwa hii ilikuwa hoja ya cdm, na kwa kuwa sote tu watanzania na Tanzania ni yetu sote, itakuwa vizuri serikali ya ccm iwasiliane na cdm wawaulize -hivi wenzetu wakati mnanadi katika kampeni kuwa mtaanzisha mchakato wa katiba mpya ndani ya siku 100 mlikuwa na mkakati au mtizamo upi?. Wawape huo mkakati na serikali iweke wake then tuanze. Hakuna maana, na kwa kweli ni kupoteza raslimali za nchi (fedha, muda nk), kuandaa muswada wa aina ile ambao mtu yeyote makini atauona unakasoro nyingi.
Kuhusu kuondolewa; nina wasiwasi na hilo kwani JK alimenukuliwa akisema katika kikao cha NEC kuwa ccm ijiandae kwenda kwa wananchi kuwaeleza ukweli wa muswada na kuondoa upotoshaji unaiofanywa na wapinzani. Hivyo inawezekana muswada umecheleweshwa ili kuipa ccm muda wa kufanya hivyo!
 
Spika Makinda, ametangaza M/KITI wa Kamati ya Bunge ya Sheria na Katiba, Mhe. Pindi Chana, ameitisha kikao cha kamati yake saa 7 mchana wa leo. Japo sijajua ajenda ya kikao hicho, ajenda kuu ni kupokea taarifa ya ukusanyaji maoni ya wananchi na kupewa taarifa ya serikali, kuuondoa muswada.
 
Mzee Mwanakijiji, siamini serikali inaogopa maandamano ya Chadema, kwa sabu ingeweza kuwanyima kibali kwa kisingizio kile kile cha yale ya Arusha, na this time, amini usiamini, Chadema wangenyimwa kibali, wasingeandamana kwani kumbukumbu ya risasi za moto za Arusha, bado ni mbichi mionyoni mwetu sisi waandamanaji, na sio wahamasishaji wa maandamano. JK ni kiburi na jeuri, hawezi kuogopa maandamano ya Chadema. Kiburi na jeuri yake mliisikia siku ile alipokuwa akizuia mgomo wa wafanyakazi akaonya watakao andamana shauri yao, vyombo vya dola vitawashughulia kwa nguvu zote (risasi za moto).
Hata sababu ya pili kuwa imeondoa kwa sababu ya ubovu, pia sio sababu, kwa sababu serikali imekwisha pitisha miswada mingi tuu mibovu mibovu, hivyo ubovu sio sababu.

Nakubaliana na wewe kwenye hili la kusoma alama za nyakati.

Pasco, serikali inajaribu kwa hali na mali kurudisha imani kwa wananchi, imegua kuwa iko detached sana na wananchi wa kawaida ila hawataki kukiri hadharani. Yaliyotokea Arusha hayatokuja kutokea tena kwani serikali inaogopa yale yanayotokea kati ya viongozi wa Kenya na Ocampo, kwa sasa hivi wapo kwenye spotlight,hawawezi kurudia makosa hayo.
Cha msingi hapa ni kupata kile wananchi tunachodai na tunawashukuru hao wanaoishinikiza serikali kufuata matakwa ya wananchi, iwe ni vyama vya siasa, wanaharakati, na sisi wenyewe wanajf.
 
Pasco hebu fuatilia hiyo source yako vizuri kujua nini kilichoondolewa kati ya haya mawili.
1. Muswada umeondolewa bungeni kinyemela - AU
2. Hati ya dharura ndio imeondolewa ili kuwapa wananchi muda wa kutosha kuudadavua muswada ili maamuzi yake yafanyike bunge la Juni na sio hili la sasa.

Please verify ili mjadala uwe mnono zaidi
Kwa mujibu wa posti hii, kinyemela maana yake kuuondoa bila kutoa taarifa rasmi popote. Taarifa rasmi zikishatolewa, sio kinyemela tena.
Taarifa rasmi itatolewa. Taarifa hiyo ndio itaonyesha kuondolewa kwa hati ya dharura, utaletwa tena mwezi Juni bila hati ya dharura, wananchi watapata nafasi kuujadili.
 
Wana bodi,

Hatimaye serikali imeuondoa kinyemela ule muswada Tata wa uundaji wa tume ya kukusanya maoni kuhusiana na katiba mpya. Muswada huo sasa hautawasilishwa tena kama ulivyopangwa awali na badala yake, utawasilishwa kikao cha mwezi Juni.

Habari hizi ni kwa mujibu wa souce ya 'kuaminika'

Hata hivyo 'source' huyo hakunipa sababu za serikali kuuondoa muswada huo ila kwa maoni yangu,
  1. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu, hivyo imesikia kilio cha waliokwisha toa maoni na ikakubali kuyazingatia.
  2. Hivyo muswada umerudishwa ili kufanyiwa marekebisho ya muhimu kiwemo kujumuisha michango ya wadau
  3. Utakapoletwa tena hiyo mwezi Juni, utakuwa ni kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
  4. Hii inamaanisha hata zile siku mbili za bunge kuendelea kukutana mjini Dodoma, siku ya Jumatatu na Jumanne ijayo kwa ajili ya kupokea maoni ya waheshimiwa wabunge, sasa hazitakuwepo, hivyo kikao hiki cha bunge kitamalizika rasmi siku ya Ijumaa.
    [*]Pia kunauwezekano serikali imesoma dalili za nyakati kwa kuangalia kama maoni ya watu wa kawaida yametoa cheche vile, jee hayo ya wabunge si ndio yangewasha kabisa moto na hata kuulipua ukumbi wa bunge?!.
  5. Uthibitisho wa kuondolewa kwa muswada huu, utawajia soon!
Pasco.

Hapo kwenye redi hapo, Bunge lipi? Hili linalopiga makofi hata kama spika akijamba? Wa upinzani wanatoa hoja lakini hawana wingi. Mfano angalia Mswada wa Bodi ya Famasia ulivyopitishwa, ndivyo ambavyo huu wa kutunga katiba mpya ungepitishwa.
 
Jamani jamani jamani, muswada mzuri hauwezi kuondolewa tu kwa hisia, kinachogomba kwa watanzania ni uelewa na madhumuni ya muswada wenyewe. Tupate uzoefu wa nchi nyingine walifanyaje? Uganda wao tume iliundwa na waziri wa katiba tu, je watanzania hatuoni kuwa tumeenziwa kwa muswadakupelekwa bungeni?? Hii ni heshima pekee na lulu watanzania tusiipoteze pleeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeez
 
Mzee Mwanakijiji, siamini serikali inaogopa maandamano ya Chadema, kwa sabu ingeweza kuwanyima kibali kwa kisingizio kile kile cha yale ya Arusha, na this time, amini usiamini, Chadema wangenyimwa kibali, wasingeandamana kwani kumbukumbu ya risasi za moto za Arusha, bado ni mbichi mionyoni mwetu sisi waandamanaji, na sio wahamasishaji wa maandamano. JK ni kiburi na jeuri, hawezi kuogopa maandamano ya Chadema. Kiburi na jeuri yake mliisikia siku ile alipokuwa akizuia mgomo wa wafanyakazi akaonya watakao andamana shauri yao, vyombo vya dola vitawashughulia kwa nguvu zote (risasi za moto).
Hata sababu ya pili kuwa imeondoa kwa sababu ya ubovu, pia sio sababu, kwa sababu serikali imekwisha pitisha miswada mingi tuu mibovu mibovu, hivyo ubovu sio sababu.

Nakubaliana na wewe kwenye hili la kusoma alama za nyakati.

Pasco nadhani hujawahi kuwa katika maandamano ya Chadema. The anger from umma is greater than kumbukumbu ya risasi. Serikali isingethubutu kuwanyika kibali kwa sababu wanajua madhara ambayo yangetokea. Na chadema wasingeacha kuandamana eti kwa sababu wamenyimwa kibali

On a broader look, usisahau kwamba mabadiliko yanayotokea sasa hivi ya serikali kutii amri ya wananchi siyo kwa sababu wanapenda kuonekana wasikivu bali kwa sababu bakuli linatembezwa barabarani kwa ajili ya bajeti ijayo. Anayetembeza anarudisha bakuli jioni likiwa tupu au pungufu na walivyozoea miaka iliyopita.

Remember my words wafadhili watakapotangaza mchango wao kwenye bajeti ijayo. Impact ya Arusha is more than we think of, iko kwenye bajeti, kwenye mabadiliko yanayotokea sasa hivi ccm na serikalini, n.k
 
Mzee Mwanakijiji, siamini serikali inaogopa maandamano ya Chadema, kwa sabu ingeweza kuwanyima kibali kwa kisingizio kile kile cha yale ya Arusha, na this time, amini usiamini, Chadema wangenyimwa kibali, wasingeandamana kwani kumbukumbu ya risasi za moto za Arusha, bado ni mbichi mionyoni mwetu sisi waandamanaji, na sio wahamasishaji wa maandamano. JK ni kiburi na jeuri, hawezi kuogopa maandamano ya Chadema. Kiburi na jeuri yake mliisikia siku ile alipokuwa akizuia mgomo wa wafanyakazi akaonya watakao andamana shauri yao, vyombo vya dola vitawashughulia kwa nguvu zote (risasi za moto).
Hata sababu ya pili kuwa imeondoa kwa sababu ya ubovu, pia sio sababu, kwa sababu serikali imekwisha pitisha miswada mingi tuu mibovu mibovu, hivyo ubovu sio sababu.

Nakubaliana na wewe kwenye hili la kusoma alama za nyakati.

Alama za nyakati ni pamoja na hayo yaliyosemwa na Mzee Mwanakijiji. (1) Wewe fikiria umejivua gamba halafu chama kingine kinafanya maandamano ni kuifuta historia yako uliyoiweka siku chache tu. (2) Kumbukumbu za risasi za Arusha (machungu ya Arusha) si kwa CDM tu bali hata kwa CCM na serikali yake. Wasingejaribu kutikisa kiberiti. Kwani kwa kufanya hivyo halafu CDM wakaandamana na wakafanya yaliyotukia Arusha pia ingefuta historia ya kujivua gamba.
 
Mzee Mwanakijiji, siamini serikali inaogopa maandamano ya Chadema, kwa sabu ingeweza kuwanyima kibali kwa kisingizio kile kile cha yale ya Arusha, na this time, amini usiamini, Chadema wangenyimwa kibali, wasingeandamana kwani kumbukumbu ya risasi za moto za Arusha, bado ni mbichi mionyoni mwetu sisi waandamanaji, na sio wahamasishaji wa maandamano. JK ni kiburi na jeuri, hawezi kuogopa maandamano ya Chadema. Kiburi na jeuri yake mliisikia siku ile alipokuwa akizuia mgomo wa wafanyakazi akaonya watakao andamana shauri yao, vyombo vya dola vitawashughulia kwa nguvu zote (risasi za moto).
Hata sababu ya pili kuwa imeondoa kwa sababu ya ubovu, pia sio sababu, kwa sababu serikali imekwisha pitisha miswada mingi tuu mibovu mibovu, hivyo ubovu sio sababu.

Nakubaliana na wewe kwenye hili la kusoma alama za nyakati.

Wewe Pasco inaelekea bado hujaelewa maana ya nguvu ya umma. Jiulize kule Tunisia, Misri, Libya, Yemen na Syria kwani walipewe au wanapewe kibali cha kuandamana?
 
Back
Top Bottom