Muswada wa Katiba waondolewa kinyemela! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Muswada wa Katiba waondolewa kinyemela!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Pascal Mayalla, Apr 13, 2011.

 1. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Wana bodi,

  Hatimaye serikali imeuondoa kinyemela ule muswada Tata wa uundaji wa tume ya kukusanya maoni kuhusiana na katiba mpya. Muswada huo sasa hautawasilishwa tena kama ulivyopangwa awali na badala yake, utawasilishwa kikao cha mwezi Juni.

  Habari hizi ni kwa mujibu wa souce ya 'kuaminika'

  Hata hivyo 'source' huyo hakunipa sababu za serikali kuuondoa muswada huo ila kwa maoni yangu,
  1. Serikali yetu sasa ni serikali sikivu, hivyo imesikia kilio cha waliokwisha toa maoni na ikakubali kuyazingatia.
  2. Hivyo muswada umerudishwa ili kufanyiwa marekebisho ya muhimu kiwemo kujumuisha michango ya wadau
  3. Utakapoletwa tena hiyo mwezi Juni, utakuwa ni kwa lugha yetu adhimu ya Kiswahili.
  4. Hii inamaanisha hata zile siku mbili za bunge kuendelea kukutana mjini Dodoma, siku ya Jumatatu na Jumanne ijayo kwa ajili ya kupokea maoni ya waheshimiwa wabunge, sasa hazitakuwepo, hivyo kikao hiki cha bunge kitamalizika rasmi siku ya Ijumaa.
  5. Pia kunauwezekano serikali imesoma dalili za nyakati kwa kuangalia kama maoni ya watu wa kawaida yametoa cheche vile, jee hayo ya wabunge si ndio yangewasha kabisa moto na hata kuulipua ukumbi wa bunge?!.
  6. Uthibitisho wa kuondolewa kwa muswada huu, utawajia soon!
  Pasco.
   
 2. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160
  Dalili zilikwishaonekana mapema pale Spika Makinda na Ikulu zilizpokanusha kuwa Muswada huo haukuwasilishwa Bungeni chini ya hati ya Dharura.
   
 3. Maganga Mkweli

  Maganga Mkweli JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 14, 2009
  Messages: 2,096
  Likes Received: 70
  Trophy Points: 145
  asante kwa taarifa mkuu
   
 4. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,360
  Likes Received: 6,377
  Trophy Points: 280
  Kama umeondolewa si kwa sababu hizo Pasco; Ila hizi zifuatazo:

  a. Maandamano ya kitaifa ya Chadema ya tarehe 16 yangeporomosha juhudi zote za kujivua gamba
  b. Wametambua kuwa mswada huu ulikuwa ni miongoni mwa miswada mibovu kabisa kuwahi kuandikwa na watu wenye akili. Na binafsi naamini unapita kwa ubovu ule mswada wa gharama za uchaguzi ambao wengine tulipinga na wengine wakajaribu kuutetea.

  Vyovyote vile ile ilivyo wamesoma alama za nyakati ..
   
 5. Crashwise

  Crashwise JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 22,172
  Likes Received: 862
  Trophy Points: 280
  Wamesoma nyakati....
   
 6. Dio

  Dio JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 8, 2011
  Messages: 1,278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Kweli.
   
 7. m

  matunge JF-Expert Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 346
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 60
  Kama ni kweli, naipongeza Serikali, hasa Mh. Kikwete: kimsingi Rais anayelipenda Taifa lake hutazama mbele (miaka 200) zaidi na wala si miaka miwili. Dunia ya leo hakuna haja ya kuficha mambo.Tuwaache watu waamue namna wanavyotaka taifa lao liwe.
   
 8. M

  Marytina JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  nimeamini JK anaendesha nchi kwa kuogopa kivuli cha CDM
  wanainchi chochote tunachotaka kwa sasa tunaweza JK hana ubavu wa kukataa.

  Tukidhamiria kwa dhati hata Spika wa BUNGE ataambiwa na JK ajiuzuli.

  JK ANANIACHA HOI, kwa sasa ameweka wazi ni ufisadi uliompa 61% na sio udini kama alivyowadanganya jamaa zake -(alikuwa akimjibu Sofia Simba :source Raia mwema.)
   
 9. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Good news
   
 10. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Sababu ya kwanza nadhani ndiyo iliyowafanya waondoe ili kuua "so" wanajua Chadema wanaungwa mkono na kwa hiyo wameuondoa ili makada wao wapate majibu ya kutoa -- kwamba tayari ccm ilishaliona hilo na kuiagiza serikali iurekebishe hivyo maandamano ya chadema yaonekane kuwa hayana umuhimu
   
 11. B

  Bobby JF-Expert Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Once again binafsi naendelea kuthibitisha ni namna gani hatuna watu makini serikalini. Ni ngumu kuamini kwamba kuna watu na akili zako kabisa very sober walisoma wakajiridhisha kabisa na hiki kituko then wakatoa go ahead mswada utoke kwa ajili ya consumption. Nakumbuka Werema na Kombani walitoka mpaka mapovu kwenye TV wakitetea kituko hiki tunachoita mswada eti hauna shida. By extension hata rais naye aliusoma the so called "mswada" na akasema usonge mbele. What an embarrassing thing jamani. Mimi na"groan" kwa huu utanzania kwa kweli.

  Mimi c mwanachadema lakini nilipanga kuandamana dhidi ya watu wanaodhani Tanzania ni mali yao so wanaweza kufanya lolote na hakuna mtu wa kuwauliza. Chadema please tuambieni bado tunaandamana next jmosi?
   
 12. M

  Marytina JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  unampongeza kwa lipi?ebu weka hapa JF wapi anastahili pongezi?kwa kusingizia udini huku akijua ufisadi ndio uliompa ile 61% iliyochakachulika?
  JK hana nia ya TZ kuwa na katiba mpya inayokidhi haja za makundi yote.Hapa kabanwa na hasa anakimbia kivuli cha CDM
   
 13. LordJustice1

  LordJustice1 JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 2,264
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Haaaaa haaaa! JK ni msanii, alikuwa anatest zari! Kama ana nia njema asingepeleka watoto kuuchapa usingizi ili kukaba nafasi za watu wengine wakati wa kuchangia Muswada wa Katiba Mpya! Sasa hivi atakuja kivingine, mtapinga kisha anaondoa hoja tena, mara 2015 hii hapa Tume ya Taifa ya Uchaguzi inachakachua matokeo, then hadi 2020!
   
 14. Nyami2010

  Nyami2010 JF-Expert Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ukweli, kwa namna mambo yanavyoenda Afrika, Mhe. J.K hawezi kukubali mambo yawe mambo katika Kipindi chake.

  Unadhani yeye hakuona juzi alivyonyanyasika Mzee Bgagbo, au unadhani hajui kuwa Mzee Hosni Mubarak ni maututi hospitalini? Lazima kwa yeyoye mwenye akili za kawaida aweze kusoma alama za nyakati na kuendana na mazingira.

  Hongera sana CDM na Hongera sanaaaa Mhe. J.K.
   
 15. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,634
  Likes Received: 1,399
  Trophy Points: 280

  hebu niambie vizuri hapo kwenye red kabla sijaitafuta raia mwema:A S-omg:
   
 16. Tuko

  Tuko JF Bronze Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Jul 29, 2010
  Messages: 11,186
  Likes Received: 396
  Trophy Points: 180
  Wakithibitisha hilo, nitaiomba CDM wasitishe maandamano yao...
   
 17. engmtolera

  engmtolera Verified User

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Oct 21, 2010
  Messages: 5,081
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Safii,kwani wamejaribu kusoma alama za nyakati hii ilikuwa inakula kwao kama wangelazimisha kama walivyopanga awali,yaani katiba mpya ndani ya siku nne kweli ingewezekana hiyo?
  Ni bora wameuondowa kwani Zanzibar walishawaeleza kuwa hawakushirikishwa na hawataki kuuona mswada huo wakisema swala muhimu la muungano hawalioni ktk mchakato mzima
  CCM imeamua kujivua gamba hadi ktk mswada hehehehehehe
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,552
  Likes Received: 18,233
  Trophy Points: 280
  Mzee Mwanakijiji, siamini serikali inaogopa maandamano ya Chadema, kwa sabu ingeweza kuwanyima kibali kwa kisingizio kile kile cha yale ya Arusha, na this time, amini usiamini, Chadema wangenyimwa kibali, wasingeandamana kwani kumbukumbu ya risasi za moto za Arusha, bado ni mbichi mionyoni mwetu sisi waandamanaji, na sio wahamasishaji wa maandamano. JK ni kiburi na jeuri, hawezi kuogopa maandamano ya Chadema. Kiburi na jeuri yake mliisikia siku ile alipokuwa akizuia mgomo wa wafanyakazi akaonya watakao andamana shauri yao, vyombo vya dola vitawashughulia kwa nguvu zote (risasi za moto).
  Hata sababu ya pili kuwa imeondoa kwa sababu ya ubovu, pia sio sababu, kwa sababu serikali imekwisha pitisha miswada mingi tuu mibovu mibovu, hivyo ubovu sio sababu.

  Nakubaliana na wewe kwenye hili la kusoma alama za nyakati.
   
 19. Mohamedi Mtoi

  Mohamedi Mtoi R I P

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 3,326
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 0
  Walichofanya kujiepusha na aibu zaidi na ndio ingekuwa mwisho wa serikali ya JK maana nguvu ya umma ingeamua aina ya muswada inayotaka. sio ule ambao watu walikaa na kufikiri kwa niaba ya watanzania
   
 20. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,174
  Likes Received: 892
  Trophy Points: 280

  serikali omba-omba kama hii ya kwetu huwa hazina misimamo.

  walijua fika kuwa waTZ hawatakubaliana na hili; sasa wanataka kuwapiga changa la macho wahisani kwamba wanazingatia utawala bora kwa kuwasikiliza raia. ili wapewe mijihela ya kununulia mashangingi.
   
Loading...