Soka Ndio Maisha Yangu
Senior Member
- Nov 27, 2024
- 110
- 377
Mwenyekiti wa klabu ya Simba ambaye katika uongozi wake Simba imebamizwa mabao mengi kuliko wakati wowote ule Mhe Murtaza Mangungu siku ya Jumamosi Asubuhi anatarajiwa kuchukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kilwa Kaskazini.
Mangungu ambaye amewahi kuwa mbunge wa Jimbo Hilo kabla ya kuangushwa na aliyewahi kuwa mbunge wa Jimbo Hilo kwa tiketi ya CUF Bw.Vedastus Ngombale anatarajiwa kupokelewa na wananchi wanaomkubali katika Jimbo Hilo siku ya Ijumaa.
Mangungu aliwahi kushinda kura za maoni mwaka 2020 lakini Magufuli alimkata jina lake na CCM ikamweka Mhe Francis Kumba Ndulane ndipo Mangungu akatafuta kazi ya kufanya pale Simba ambapo alishinda kwenye nafasi ya uenyekiti akianza kumshinda Juma Nkamia na baada wakili mmoja hivi nimemsahau jina lake.
Mangungu hana rekodi yoyote ya kucheza mpira Wala hajawahi kuongoza mpira hata kule Kipatimu, uzoefu wa kuongoza soka ameupatia Simba.
Mangungu anakubalika sana jimboni kwake, wananchi wanamkumbuka kwa kazi nzuri alizowafanyia alipokuwa mbunge, hivyo japokuwa anashindana na mtoto wa Kingunge Ngombale Mwiru lakini sioni wa kumshinda jabali huyu kwenye Siasa za Kilwa Kaskazini.
Mangungu amewasababishia maumivu makali sana mashabiki wa Simba, wengine sisi tunaojua mpira tunajua Simba ilipeleka timu kishingo upande kwa ajili ya kumheshimisha mkuu wa nchi, lakini gemu hawakuitaka kabisa, hakukuwa na mipango Wala mikakati ya ushindi Jana ndio maana inaonekana kama Simba walikuwa katika kiwango cha chini sana, ni vile TU Yanga pia hawana ubora kwani kwa namna Simba ilivyokuwa inacheza ilistahili adhabu Kali sana Jana, Sasa kama Simba mbovu isiyokuwa na mikakati ya mchezo wa Jana imekula 2 je wangeamua kujipanga hasta ingekuwaje.
Nakutakia Kila la heri Mangungu, najua utashinda kura za maoni bila wasiwasi wowote, wananchi wanaamini 2020 hukutendewa haki, ila ombi langu nakuomba sana, Niko chini ya miguu Yako, ukiteuliwa kuwa mgombea wa ubunge achia nafasi ya uenyekiti pale Simba, watu wanaichomesha timu ifanye vibaya kwa sababu Yako, pili nakuomba wewe ni kiongozi wa muda mrefu sana na una uzoefu, angalia sana lugha zako kiongozi, una lugha ngumu sana kwa mashabiki na hata waandishi wa habari wanapokuuliza maswali.
Asante