Mungu tupe akili sana sana sisi ngozi nyeusi

Nyamwage

JF-Expert Member
Oct 16, 2020
634
1,535
Habari JF

Wanadamu ni wanafiki sana tena pengine nahisi wengi tunafanya mambo hayo ya kipumbavu kwa mihemko na kufwata mkumbo kibaya zaidi kwa mfano una darasa lina wanafunzi 40 wachukue hao wanafunzi uwagawe katika makundi mawili kundi A na kundi B bila kujali dini zao wala kabila zao alafu hayo makundi uyape majina ukweli ni kwamba siku zinavyo zidi kwenda automatic tu hawa wanafunzi wa kundi A na B wataanza kuchukiana chuki za chini chini pengine bila hata sababu.

Ngoja nitoe mfano ulio hai wa unafiki wenyewe Zanzibar na Pemba ni nchi ambayo asilimia kubwa ya watu wake ni waislamu na mioyoni mwao hawajisikii vizuri kuona dini nyingine yoyote ikiingia katika aridhi yao na kuota mizizi wanataka wawe wao kama wao na dini yao moja ili wapendane na kushirikiana katika kila jambo linalohusu maendeleo ya nchi yao.

Unafiki unakuja sasa kwa huyo huyo mwislamu hataki kumpa kazi muislam mwenzie hususa ni kazi za kiufundi eti kisa mtu huyo hataimalizi hiyo kazi kwa wakati sababu atatumia muda wake mwingi kwenda kuswali swala zote tano kwa siku hivyo boss anaona atapata hasara.

Hivyo maboss wengi wa huko visiwani waarabu kwa waswahili asilimia kubwa huagiza mafundi kutoka bara kwa sababu wengi wao sio watu wa msikitini na wanachapa kazi kuliko wazawa hapo udini na ukanda wameuweka pembeni wapo katika ubinafsi.

Tuje duniani sasa likitokea tukia mtu mwenye asili nyeupe akimfanyia vitendo vya ukatili au kupoteza Masha ya mtu mweusi basi watu wote weusi duniani bila kujali dini zao wala kabila zao wataungana kulaani kitendo hicho lakini hapo hapo unasikia habari tena binadamu mweusi kamuua binadamu mwenzie mweusi sababu ya dini.

Sio hayo tu kuna vita vya kikabila unakuta watu dini ni moja lakini kabila zao ni tofauti wataanza kuchukiana mpaka kufikia hatua ya kupigana vita vita vya kikabila.

Tukija kwenye vyama vya siasa sasa humo ndio kuna unafiki mkubwa sana hasa kwa sisi ngozi nyeusi.

Dawa ya kuyashinda haya maroho ya kinafiki, kibinafsi na ya kibaguzi ni kumuomba Mungu akupe akili sababu ukiwa na akili huwezi kuendeshwa na mihemko ya kufuata mkumbo.
 
Umeandika vitu poa sana ila mi nahisi Mungu mwenyewe ndo anapenda mambo yaende hivo.... unapendekeza tumuombe Mungu atupe akili, ukiwa na maana kwamba tukiwa na akili hatutafanya hivo, ikiwa wewe tu mwanadamu umewaza kwamba tukiwa na akili hatutafanya hivo, je Mungu mwenyewe hajui hilo hadi tumuombe? Au hatoi kitu hadi aombwe!?

Mi nafikiri Amani hiyo unayotaka iwepo, Mungu haitaki maana angekuwa anaitaka angetuumba tukiwa na hulka ya kutenda hayo mema unayoyazungumzia.
 
Yaani tuombe tena kwa Mungu aluyekubali kutuumba na tabia unazotaja.UNATANIA MKUU.
 
Umeandika vitu poa sana ila mi nahisi Mungu mwenyewe ndo anapenda mambo yaende hivo.... unapendekeza tumuombe Mungu atupe akili, ukiwa na maana kwamba tukiwa na akili hatutafanya hivo, ikiwa wewe tu mwanadamu umewaza kwamba tukiwa na akili hatutafanya hivo, je Mungu mwenyewe hajui hilo hadi tumuombe? Au hatoi kitu hadi aombwe!?

Mi nafikiri Amani hiyo unayotaka iwepo, Mungu haitaki maana angekuwa anaitaka angetuumba tukiwa na hulka ya kutenda hayo mema unayoyazungumzia.
Mathinker wenzangu tu ndo watakuelewa
Ila huo ndo ukweli mchungu.
 
Pia nakukumbusha hata hao weupe wanabaguana sana ila black ndo walalamikaji sana.

Matabaka hayaepukiki kuanzia ngazi ya familia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom