Not to be a Red comrade or anything.
Mentality nzima ya "Mungu Mlinde Dr. Slaa Aiokoe Tanzania" ina matatizo lukuki, neno kwa neno.
Ukianza kwa mungu tu una deal na a hoax. Mungu hayupo. Kwa hiyo habari nzima ya mungu kutoa ulinzi ni ushairi shayiri tu.
Tanzania ina umaskini mkubwa kwa sababu ya kukataa uchunguzi na kwenda na imani imani tu, mojawapo ya msingi kabisa inayotufanya tuwe masikini ni hii ya mungu.
Watu wanaoamini kuwapo kwa mungu ni rahisi zaidi kukubali kuwa katika utawala dhalili usioheshimu haki za msingi za binadamu, kuliko wale ambao hawaamini kuwapo kwa mungu. Mungu analeta excuses kibao za kukubali udhalili. Kuanzia "utapewa malipo peponi" mpaka "watiini watawala maana wamewekwa na mungu".
Kwa hiyo kama unataka Tanzania iendelee ondoa habari za mungu katika mawazo kwanza. Mungu ni tatizo Tanzania, si suluhisho.
Mlinde? Of course kama mungu hayupo hawezi kumlinda, lakini hata kama angekuwapo. Asipomlinda - short of against death- na kumpa majaribu zaidi ndo tutamjua kama ni kiongozi bora au anaelea kwa sababu ya hali nzuri tu. Ayubu hakuthibitisha imani yake na uthabiti kwa kulindwa na mungu, alithibitisha hayo kwa kutolindwa na mungu.
Aiokoe? Kwa nini Tanzania itake mtu wa kuiokoa? Huyu Dr. Slaa ni nani mpaka aiokoe Tanzania? Yeye ni Masiha au Mahdi gani huyu?
Uongozi wetu hauhitaji charismatic figures wa kutuokoa, hatuhitaji top down leadership. Hii ina introduce a single point of failure. We have been there, done that, bought the T-Shirt to show. It is written "Nyerere, baba wa Taifa" aka Mchonga aka Haambiliki.
Kwa nini tutake strongman mwingine badala ya kutaka a grassroots empowerment? Kwa nini tusitake ushirikishwaji wa umma zaidi? Kwa nini tusitake wabunge machachari zaidi wanaohuishwa na jumuiya thabiti zenye uelewa wa mamabo zaidi?