Vision Tanzania: Dr. Slaa Atembelea Shirika la Umeme Marekani

Vision Tanzania: Dr. Slaa Atembelea Shirika la Umeme Marekani

Rtackket

Member
Joined
Sep 24, 2013
Posts
74
Reaction score
373
Dr. Slaa anaendelea na safari yake ya kujifunza inayoitwa “Vision Tanzania” ambayo leo imemfikisha katika kituo kikubwa cha Umeme kinachoitwa Alabama Power Company ambayo inatenegenza umeme wake kutokana na jua, gesi asilia, makaa ya mawe, upepo, jua, takataka, (biomass) pamoja na nuklia

Akielezea baadhi ya shuguli za Alabama Power company, mkurugenzi wa shirika hilo linalojitegemea, ameeleza kwamba shirika hilo linawahudumia wateja million nne tu, huku ikizalisha kiasi cha megawati 48,000 (4.8GW) Tangu kuanzishwa kwa shirika hilo, hakujawahi kutokea mgao wa umeme au umeme kuzimwa hata kwa dakika 5. Panapotokea dharura, kuna kuwepo njia mbadala ya kukabiliana nayo,

Kwa upande wake, Dr. Slaa amejifunza na kugundua kitu kimoja kwamba, watanzania wanaumia kutokana na wachache kuligeuza Tanesco kuwa mradi wao. Dr. Slaa anaamini kwamba mgao tulionao Tanzania, ukosefu wa umeme tulionao ni matunda ya ufisadi wa CCM. Kiongozi huyo anaamini kwamba tatizo ni ccm na desturi yao ya kulindana. ilahali tunatengeneza 600MW huku Waziri Muhongo akidai mwakani tutauza umeme nje ya nchi. Umeme gani wa kuuza nje ya nchi wakati 80% ya watanzania hawana umeme? Huyu mtu yuko katika sayari gani? Miaka 52 ya ufisadi, kugawana vyeo kindugu, umasikini na magonjwa sasa tuseme basi. CCM hawawezi kujidai kwamba watatatua matatizo ya watanzania

Viongozi wakuu Wizarani na Tanesco wanawazuia na kuwadhalilisha wawekezaji kwa manufaa yao binafsi na makampuni yasiyokuwa na huruma na mwananchi wa kawaida. Njia pekee ya kumuokoa mtanzania, ni mtanzania mwenyewe kuamka, na kumng’oa adui CCM kupitia njia ya kura. Mtanzania asifanye kosa tena 2015. Lazima amn’goe CCM ili apate umeme na kuweza kuboresha maisha yake

Akitembelea mitambo inayopewa ulinzi wa kipekee, Dr. Slaa amejionea jinsi kampuni hiyo inavyofanya shuguli zake pamoja na kuwa na mitambo ya kisasa inayo monita njia zote za umeme kusini mwa marekani yaani, Georgia, Florida, Alabama, Mississini na South Carolina.

Mkurugenzi wa shirika hilo, amemuahidi Dr. Slaa kwamba wako tayari kuja Tanzania na kuisadia nchi hiyo kuboresha uzalishaji, usambazaji pamoja na uendeshaji ikiwa serikali itawahitaji, kwani wameisadia nchi za Philippines na Kuwait ambazo hadi sasa wanazo umeme wa uhakika.
attachment.php

Dr. Slaa na ulinzi wake wakiwasili katika ofisi za Shirika la Alabama Power Company
attachment.php

Dr. Slaa anaelekea kwenye ofisi za shirika
attachment.php

Mkurugenzi mkuu akimpokea Dr. Slaa na Mkewe
attachment.php

Mkurugenzi wa shirika akimpa maelezo Dr. Slaa jinsi shirika hilo linavyofanya kazi
attachment.php

Sehemu maalum yenye ulinzi mkali ambako gridi inakuwa monitored
attachment.php

Dr. Slaa akitizama kwa umakini mitambo hiyo ya kusisimua inayoongoza gridi kusini mwa marekani.Hata mashine moja ikiharibika watagundua maramoja na kuweza kutafuta njia mbadala
attachment.php

Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu na mwanasheria mkuu wa shirika hilo​
 

Attachments

  • Dr. Slaa Akiwasili Alabama Power.jpg
    Dr. Slaa Akiwasili Alabama Power.jpg
    60.6 KB · Views: 6,187
  • Dr. na walinzi.jpg
    Dr. na walinzi.jpg
    68.4 KB · Views: 5,855
  • Viongozi wa juu.jpg
    Viongozi wa juu.jpg
    52.4 KB · Views: 5,751
  • Maelekezo.jpg
    Maelekezo.jpg
    45.2 KB · Views: 5,908
  • High security control room.jpg
    High security control room.jpg
    35.3 KB · Views: 5,664
  • Control room.jpg
    Control room.jpg
    1.8 MB · Views: 393
  • Control room.jpg
    Control room.jpg
    49 KB · Views: 5,478
  • Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu chenye historia ya shirika hilo.jpg
    Dr. Slaa akikabidhiwa kitabu chenye historia ya shirika hilo.jpg
    52.1 KB · Views: 5,437
we talii tu na ruzuku zetu, hamna chochote, alafu misikule mingine inasema go go? ngoja arudi km utaona matunda
 
tunashukuru kwa taarifa
Labda haya mawazo mapya anayoyapata yatasaidia watanzania

maana kunawatu wako madarakani zaidi ya miaka 50, na wametembelea nchi zaidi ya 60 lakini wanakwenda huko wakirudi hakuna jipya wanalorudi nalo kuwasaidia watanzania

Tanzania tuna kila kitu tatizo tunakosa watanzania (VIONGOZI)wenye dhamira ya dhati ya kumsaidia mtanzania katika matatizo yanayomkabili
 
Padri na mitambo wapi na wapi labda alikuwa anacheki tu yale mambo yake anayoyapenda.
 
we talii tu na ruzuku zetu, hamna chochote, alafu misikule mingine inasema go go? Ngoja arudi km utaona matunda

nipe matunda ya jk ya kutembelea ulimwengu mzima hadi sasa??/

quantify gahrama alizotumia ambazo ni za walipa kodi na payee za watz, na matunda aliyoleta... ???

Haya ya kuleta wachina wauza vitunguu kariakoo, wachina wanaoibia tanesco umeme, hawa wakezezaji wa hanangi-manyara wanao wachomea nyumba wenyeji, hawa waarabu wauza madawa ya kulevya... Kuna lipi jipya jk amewaletea watanzania tangu kuanza safari zake za nje 2005..
View attachment 115213

View attachment 115214SOMA HILO BANGO KWA MAKINI
View attachment 115215
kiroba ccm.png
 
tunashukuru kwa taarifa
Labda haya mawazo mapya anayoyapata yatasaidia watanzania

maana kunawatu wako madarakani zaidi ya miaka 50, na wametembelea nchi
zaidi ya 60 lakini wanakwenda huko wakirudi hakuna jipya wanalorudi nalo
kuwasaidia watanzania

Tanzania tuna kila kitu tatizo tunakosa watanzania (VIONGOZI)wenye
dhamira ya dhati ya kumsaidia mtanzania katika matatizo
yanayomkabili

wakati dr slaa ameenda kutalii huko, rais JK amefanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano barani afrika kuwekwa kwenye mpango wa marekani wa Power Afrika ambao utaifanya Tanzania kuzalisha umeme wa ziada kwa ajili ya mataifa mengine ya Afrika
 
Anaendelea na safari yake ya kitalii ulaya kwa kodi zatu ee. Sijui atatuletea lipi la maana huyu fisadi.
 
nipe matunda ya jk ya
kutembelea ulimwengu mzima hadi sasa??/

quantify gahrama alizotumia ambazo ni za walipa kodi na payee za watz,
na matunda aliyoleta... ???

Haya ya kuleta wachina wauza vitunguu kariakoo, wachina wanaoibia
tanesco umeme, hawa wakezezaji wa hanangi-manyara wanao wachomea nyumba
wenyeji, hawa waarabu wauza madawa ya kulevya... Kuna lipi jipya jk
amewaletea watanzania tangu kuanza safari zake za nje 2005..

labda wewe ni diaspora hujui yanayojiri hapa Tanzania. nakushauri ujaribu kurudi nyumbani ili uone maendeleo tunayopiga kuanzia nishati, miundombinu, ujenzi, kukuza uchumi nk
 
wakati dr slaa ameenda kutalii huko, rais JK amefanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano barani afrika kuwekwa kwenye mpango wa marekani wa Power Afrika ambao utaifanya Tanzania kuzalisha umeme wa ziada kwa ajili ya mataifa mengine ya Afrika

umeandika uharooooo......idiot
 
Anaendelea na safari yake
ya kitalii ulaya kwa kodi zatu ee. Sijui atatuletea lipi la maana huyu
fisadi.

mkuu, hana lolote atakalokuja nalo labda tutarajie Josephine kupata deal la kupata mashine za kuzalisha umeme
 
wakati dr slaa ameenda kutalii huko, rais JK amefanikisha Tanzania kuwa miongoni mwa nchi tano barani afrika kuwekwa kwenye mpango wa marekani wa Power Afrika ambao utaifanya Tanzania kuzalisha umeme wa ziada kwa ajili ya mataifa mengine ya Afrika

Kwa hiyo kwa akili zako mpaka leo miaka 50 tunashindwa kujitegemea hata kwa umeme?? na unafurahia kuwekwa kwenye huo mpango wa marekani.. MKUU BADO UNAAKILI ZA HADI WAZUNGU WAJE KUTUSAIDIA?? UNADHANI KUNA KITU CHA BURE TOKA KWA HAO WAMAREKANI MKUU.. LAZIMA ULIPIE TU...,

JIULIZE TUNASABABU GANI YA WATOTO WETU KUKOSA MADAWATI HADI LEO>??? NAYO WAMAREKANI WAJE KUTUSAIDIA?? KWELI BADO TUNASAFARI NDEFU.... UNAUJUA HUU MSEMO.. MTEGEMEA CHA NDUGU... MIAKA 50 BADO UNAWATEGEMEA WAZUNGU.. SASA TULIWAFUKUZA WANINI???
 
Tamthilia inaendelea teh teh teh teh!.

Dr.W.Slaa, unataka kushindana na Rais wako Kikwete.

Usishindane na ndovu.....
 
Last edited by a moderator:
Kwa
hiyo kwa akili zako mpaka leo miaka 50 tunashindwa kujitegemea hata kwa
umeme?? na unafurahia kuwekwa kwenye huo mpango wa marekani.. MKUU BADO
UNAAKILI ZA HADI WAZUNGU WAJE KUTUSAIDIA?? UNADHANI KUNA KITU CHA BURE
TOKA KWA HAO WAMAREKANI MKUU.. LAZIMA ULIPIE TU...,

JIULIZE TUNASABABU GANI YA WATOTO WETU KUKOSA MADAWATI HADI LEO>???
NAYO WAMAREKANI WAJE KUTUSAIDIA?? KWELI BADO TUNASAFARI NDEFU....
UNAUJUA HUU MSEMO.. MTEGEMEA CHA NDUGU... MIAKA 50 BADO UNAWATEGEMEA
WAZUNGU.. SASA TULIWAFUKUZA WANINI???

we mbona hueleweki? hayo matusi yako huoni kuwa unamlenga dr slaa? kama wazungu hawana la maana, mbona yupo marekani kwa wiki ya pili sasa? anafanya nini kwa wazungu wasio na maana?
 
mkuu, hana lolote atakalokuja nalo labda tutarajie Josephine kupata deal la kupata mashine za kuzalisha umeme

Halafu huyu mama nammaindi sana alivyotutukana humu ndani. Sijui kiburi amepewa na nani? Mwanamke mwenyewe hajaolewa sasa akijaolewa sijui tutakomaje?
 
labda wewe ni diaspora hujui yanayojiri hapa tanzania. Nakushauri ujaribu kurudi nyumbani ili uone maendeleo tunayopiga kuanzia nishati, miundombinu, ujenzi, kukuza uchumi nk


maendeleo gani mkuu??

Haya ya watoto 85% wanaomaliza kidato cha nne kupata zero hadi serikali inaamua kurisiti mitihani?? ,
haya ya zaidi ya 75% wanaofaulu kuingia kidato cha kwanza kutokujua kusoma na kuandika ndio maendeleo unayoongea??
Haya maaendeleo ya kuua viwanda 250 vilivyokuwepo enzi za mkoloni na wakati tunapata uhuru??
Haya maendeleo ya kujenga barabara kilomita 4500 kwa kutegemea mikopo ya benk of africa na benki ya dunia
haya maendeleo ya kuwauzia kila kitu wazungu kwa 10%?? Unajua kama dhahabu imekwisha barrick wanafunga?? Unajua kama uranium ya namtumbo tayari kuna makampuni 3 yameshakuja na yameondoka na madini hata bila serikali kujua, na kulipa kodi

haya ndio maendeleo ya kuacha kukusanya kodi kwa wawekezaji na kuwakaba watumiaji wa simu

.. Unayakumbuka haya maneneo ya nyerere "serikali legelege na inayonuka rushwa haikusanyi kodi kwa mabwana wakubwa... Pole sana

nipe miradi ya ndani iliyofanyika kwa fedha zetu....

Naona unaakili kama za viongozi wako wanaoamini kuwa kuongezeka kwa foleni dar-es-salaam ni dalili ya maendeleo...
 
Back
Top Bottom