Special thread: Dr. Slaa tuungane uchaguzi mkuu 2015, taifa hili linakuhitaji! Tumetoka mbali pamoja

TheDealer

JF-Expert Member
Nov 19, 2012
2,424
1,129
Kwako Dr.W.Slaa !

Utangulizi:
Dr, Slaa Kama kuna sehemu nitaandika vibaya hadi kukukwaza naomba nitangulie kuomba radhi. Nipo chini ya miguu yako. Siandiki kwa nia mbaya bali kwa nia njema ya kukusihi usitengane nasi! Tunakupenda sana, tunakuhitaji sana, tumetoka mbali sana pamoja!

Hakuna shaka kuwa wote ndani ya chadema tumefikishana hapa kwa kutegemeana. Sisi kama vijana na wazee tumekuunga mkono popote pale. Ndugu, jamaa na marafiki zetu wameuwawa, wamepoteza kazi, wamepata vilema vya kudumu tukiwa kwenye harakati za kukuunga mkono kisiasa. Tulijitokeza kwa wingi wetu, tukapambana na dola dhalimu yenye silaha kali na mabavu kwa wingi na umoja wetu. Hadi Dola dhalimu ilikuogopa kwa sababu yetu sisi vijana kwa wazee. Kila wakiangalia kundi kubwa lililo nyuma yako wanakuogopa na kurudi nyuma. Wanaogopa kukugusa kwa sababu yetu sisi na si kwa sababu yako wewe na familia yako.

Sisi ndio ngao, silaha na ulinzi wako. Dola dhalimu haikuogopi wewe Dr. Slaa bali inatuogopa sisi. Wanajua wakikugusa wewe wametugusa sisi kundi kubwa. Wanajua hili. Hata pale ulipo sema tutahakikisha nchi haitatawalika kama haki za watanzania zitaendelea kupuuzwa, yote hayo unasema kwa kujiamini kwa sababu ya kiburi tulichokujaza sisi. Unatuita sisi ni mahakama ya umma. Nao wamekuogopa kwa sababu yako sisi, na wala si kwa sababu yako wewe Dr. Slaa wala si kwa sababu ya familia yako. Ni fahari kwako kuwa na wafuasi wengi walio nyuma yako. Nakumbuka Mh. Mwakyembe aliwahi kusema kuwa kulikuwa na mkakati wa kuuliwa wewe mwaka 2010 lakini waliogopa kukuua kwa sababu yetu sisi tulio nyuma yako. Walisema nchi itayumba kwa sababu una wafuasi wengi sana nchi hii. Ni kipindi hiko shekhe maarufu alitabiri kuwa kuna mtu maarufu angefariki dunia kwenye mbio za urais!

Lakini leo kuna dalili mbaya ya wewe kujitenga nasi. Leo unajitenga nasi na kuwa karibu na familia yako zaidi kuliko sisi. Leo unajitenga nasi wakati jeshi la kuwa nyuma yako limeongezeka zaidi. Wamekuja wa CUF, NCCR, na NLD. Wanaohamia chadema wanaona ni sehemu salama. Lait kama dola ingeshakufanyia lolote baya hakika hakuna ambaye angethubutu kuhama ccm na kuja chadema. Lakini kuwa kwako salama ndani ya chadema kumewapa wengi ujasiri wa kuja ndani ya chadema. Unadhani wanamfuata nani? Wanatufuata sisi wafuasi wa chadema wazee kwa vijana. Wafuasi walioweza kukulinda bila silaha yoyote bali umoja wao na mshikamano wao. Wanaohamia hawakufuati wewe Dr. Slaa bali wanatufuata sisi jeshi kubwa la ukombozi. Sisi ni people's power! Sisi ni makamanda! Kwenye mikutano yetu tunakunja ngumi na kunyoosha mikono juu kwa ajili ya kuonyesha utayari wa kukulinda na kupambana. Tunavaa nguo ngumu magwandwa kama ishara ya uaskari na ukakamavu. Yote ni kukulinda wewe kama kiongozi wetu mkuu. Tumekufanya wakuogope kupita kiasi. Nikukumbushe kwani ulipokuwa ccm walikuwa wanakuogopa kama wanavyokuogopa sasa hivi? Mbona walikukata jina ugombea ubunge karatu? Lakini ulipojiunga nasi chadema nguvu yako ikaongezeka.

Sasa hivi unatisha. Usidhani unatisha kwa sababu umewahi kugombea urais, hapana. Hata yule mama wa PPT Maendeleo naye amegombea urais, hata Dovutwa naye amegombea urais. Na hawatishi. Unatisha kwa sabau ya sisi tulio nyuma yako. Sisi sio familia yako, lakini ni familia yako ya kisiasa tuliosimama nawe kidete mbele ya maadui zako. Ukiguswa kisiasa, ama kifamilia wametugusa sisi.

Hata nasikitika wapya waliohamia hawavai hata magwanda, Lowassa vaeni magwanga, hawasemi pipoz kwa sauti ya kuwatisha, hawasemi hadi kieleweke. Yaani hawatishi. Hawajui kuwa sisi hatuna silaha lakini tunapambana na wenye silaha. Tunapambana na jeshi, tunapambana na polisi. Tunapambana na ikulu. Tunapambana na usalama wa Taifa. Sisi hata ajira hatuna, hatuna hata uhakika wa kula, hatujui hatma yetu ya kesho. Lakini ni makamanda kwelikweli. Nawasihi makamanda wapya mvae magwanda. Magwanda ni alama ya heshima kwetu. Ni alama ya mapambano na ukombozi. Ukivaa gwanda unapata msaada popote pale nchi hii, maana unajitambulisha kuwa wewe upo mstari wa mbele kukomboa taifa. Tafadhalini vaeni magwanda. Ukionyesha alama ya V unaonekana kama nuru mpya penye giza nene. Sote hizi Dr, Slaa amefanya nasi. Hatutaki akae mbali nasi.

Dr, Slaa ni wewe peke yako ndo umeamua kujitenga nasi kwa kipindi hiki, viongozi wengine wote wapo nasi, kuanzia viongozi wakuu wa NCCR, CUF na NLD na wengine wote pamoja na wanachama wao. Wafuasi wote wa chadema wameridhia mchakato wa uchaguzi unaondelea sasa. Ispokuwa wewe kwa kuwa hatukuoni kwenye mchakato, na mengi mabaya yanaandikwa lakini upo kimya, wala hukanushi! Natamani kuandika mengi sana kukukumbusha jinsi sisi na wewe tulivyo lakini yatosha kwa leo, makamanda wengi wataendelea kuandika. Lakini nina mengi sana ya kukumbusha.

Dr, Slaa kuna wengi wafuasi wako unawaumiza sana. Ni wengi kuliko familia yako, hata naamini wamekufaa vizuri zaidi kwenye wakati mgumu zaidi kuliko hata familia yako. Leo unawatelekeza na kuwaona hawafai. Unawachunia. Maumivu yao hayatakuacha salama. Usalama wa maisha yako yana gharama ya damu zao, uhai wao, jasho lao, machozi yao, maombi yao, kilio chako. Sote hizi hazitakuacha salama, Dr Slaa! Wafuasi hawa wakikasirika umaarufu wako utapeperushwa na upepo mchana kusikokuwa na upepo!

Ni kheri ubaya wenye mwisho mzuri, kuliko wema wenye mwisho mbaya. Wewe umekuwa mwema sana kwetu nasi tumekuwa wema sana kwako, lakini leo sisi tumechagua ubaya (Lowassa kwa tafsiri ya ufisadi) wenye mwisho mzuri (kukomboa taifa).

Makamanda, na wote wanaomuhitaji Dr Slaa kwenye safari yetu ya ukombozi, tunaomba sote tuungane hapa tuhesabiwe kumwomba Dr Slaa arudishe moyo nyuma, na aungane nasi! Kuna kitu kimenikaba roho kwa uchungu mkali nashindwa kuendelea!

Ahsanteni nyote!

Last edited by a moderator:
HA HA HA fun threads. Twende na Magufuli Ikulu 2015 achana na Dr Slaa, Fisadi Lowasa na Msaliti zito, wimbo wa sasa ni Dr magufuli tu kwa ukombozi wa kweli wataifa letu
 
HA HA HA fun threads. Twende na Magufuli Ikulu 2015 achana na Dr Slaa, Fisadi Lowasa na Msaliti zito, wimbo wa sasa ni Dr magufuli tu kwa ukombozi wa kweli wataifa letu

Mmeshindwa kulikomboa kwa muda wa miaka zaidi ya 50, mtaweza sasa?
 
Mwaka huu mtaisoma namba Fisadi Kuu Lowasa na Fisadi wa ruzuku za Chadema hawapatani, Twende na Dr Magufuli anajua watanzania wanahitaji nini katika nchi yao
Mmeshindwa kulikomboa kwa muda wa miaka zaidi ya 50, mtaweza sasa?
 
Dr. Slaa, pleaase, rudisha moyo wako. Come back. Tuna imani na wewe. Let's Fight this war together. Tuliondoe Pamoja hili dudu CCM come 25th Oct, 2015.
 
The dealer...,
Umesema vyema.... Huu si wakati wa kususa..., si wakati wa kununa ni wakati wa mapambano ya kuitoa nchi ktk makucha ya waporaji.., wezi wa mchana..., walimu wa rushwa... Watu hawa wanaiangamiza jamii ya wa Tanzania kwa faida ya familia zao... Dr Slaa...., adui yetu mkubwa ni HAO..., CCM..., na sio ka mtu kamoja..., Lowassa...!
Amka huko uliko Dr..., vaa gwanda uje uikomboe nchi..., SISI ndio wenye kujua nafasi yako ktk nchi hii... Tunakupenda sana..., tafadhali usituangushe..., njoo tumalizie kazi hii pamoja...!
 
Kabisa mkuu!
 
Dr Ana Hot Deal la kwenda ACT kugombea Urais agawe vijikura vyenu. CCM Mble kwa mbele na Dr Magufuli Huyooooo Ikulu ya Magogoniiii na nape Msiye mpenda ndo atakuwa Waziri wa Habari, Chadema Mtaisoma Nambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa TCCM 2015 hiyo inaingia Ikulu
 
Slaa hawezi kuchangamana na mafisadi na wauza unga hata kdogo kwahiyo mafisadi kivyao na wasafi kivyao.
 
The dealer...,
Umesema vyema.... Huu si wakati wa kususa..., si wakati wa kununa ni wakati wa mapambano ya kuitoa nchi ktk makucha ya waporaji.., wezi wa mchana..., walimu wa rushwa... Watu hawa wanaiangamiza jamii ya wa Tanzania kwa faida ya familia zao... Dr Slaa...., adui yetu mkubwa ni HAO..., CCM..., na sio ka mtu kamoja..., Lowassa...!
Amka huko uliko Dr..., vaa gwanda uje uikomboe nchi..., SISI ndio wenye kujua nafasi yako ktk nchi hii... Tunakupenda sana..., tafadhali usituangushe..., njoo tumalizie kazi hii pamoja...!
Wakati mnamtukana hamkujua kuwa anafaa leo ndiyo mnakumbuka wakati mlimtukana matusi yote.
 
HA HA HA fun threads. Twende na Magufuli Ikulu 2015 achana na Dr Slaa, Fisadi Lowasa na Msaliti zito, wimbo wa sasa ni Dr magufuli tu kwa ukombozi wa kweli wataifa letu

Mwaka huu mtaisoma namba Fisadi Kuu Lowasa na Fisadi wa ruzuku za Chadema hawapatani, Twende na Dr Magufuli anajua watanzania wanahitaji nini katika nchi yao

Nyie makahaba mmetokea wapi huku.. Hii sio safu yenu nendeni lile jukwaa lenu mkajiuze huko.
 
CHADEMA walichomfanyia Dr Slaa kwa hali ya kawaida si kitu kirahisi. Nakumbuka wakati ENL anatangaza nia na makada wengine wa CCM wakitangaza nia kwa wingi, Dr Slaa alikuwa anazunguka majimboni kuwahamasisha wananchi wajiandikishe kwenye daftari la kudumu la wapiga kura (Tunaweza kusema ni Pre Campaign). Sasa leo eti ghafla asahau ndoto na mipango aliyoipanga kwa kipindi cha miaka mingi, pengine zaidi ya miaka 10, kisa flani kakatwa jina. Naomba kwa hili tumuelewe Dr kama mwanadamu ana kila haki ya kureact kwa swala zito kama hili. Inauma na ndio maana ENL aliona ahame akatafute urais kwingine kwa kuwa alikuwa na hayo malengo. Je, tutashangaa kuona Dr akihama kwenda kutafuta urais kwingine? Naomba tumuelewe Dr Slaa.

Nawasilisha
 
Niungane nawe kumwita Dr.Slaa kurudi kundini.....nimeandika hapa jf kuwa haijarishi ni slaa hipi tuitumie sasa kuwaondoa ccm madarakani....kwa sasa slaha inayoonekana bora ni hiyo....kuwatumia wao kujiondoa kwa mwanvuri wa ukawa.

Dr. Slaa ajue kuwa safari iliyokombele bado si nyepesi na haingekuwa lahisi kwa ukawa pasipo nguvu kutoka upande mwingine wa wao kujipinga wao tukaioona ikulu. Yamkini ikawa slaha tutakayoitumia sasa ionekane mbaya kwa mwono uliopita lakini nauona ushindi hapo mbeleni.....mengine tutalekebishana baadae mbele ya safari. Karibu Dr. Slaa tuendelee mbele.
 
Dr Ana Hot Deal la kwenda ACT kugombea Urais agawe vijikura vyenu. CCM Mble kwa mbele na Dr Magufuli Huyooooo Ikulu ya Magogoniiii na nape Msiye mpenda ndo atakuwa Waziri wa Habari, Chadema Mtaisoma Nambaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa TCCM 2015 hiyo inaingia Ikulu

hahahaha! taratibu kuu utawafanya wa andamane
 
The Dealer,

Niungane nawe kumwita Dr.Slaa kurudi kundini.....nimeandika hapa jf kuwa haijarishi ni slaa hipi tuitumie sasa kuwaondoa ccm madarakani....kwa sasa slaThe Dealer,

Niungane nawe kumwita Dr.Slaa kurudi kundini.....nimeandika hapa jf kuwa haijarishi ni slaThe Dealer,

Niungane nawe kumwita Dr.Slaa kurudi kundini.....nimeandika hapa jf kuwa haijarishi ni slaa hipi tuitumie sasa kuwaondoa ccm madarakani....kwa sasa slaThe Dealer,

Niungane nawe kumwita Dr.Slaa kurudi kundini.....nimeandika hapa jf kuwa haijarishi ni slaa hipi tuitumie sasa kuwaondoa ccm madarakani....kwa sasa slaha inayoonekana bora ni hiyo....kuwatumia wao kujiondoa kwa mwanvuri wa ukawa.

Dr. Slaa ajue kuwa safari iliyokombele bado si nyepesi na haingekuwa lahisi kwa ukawa pasipo nguvu kutoka upande mwingine wa wao kujipinga wao tukaioona ikulu. Yamkini ikawa slaha tutakayoitumia sasa ionekane mbaya kwa mwono uliopita lakini nauona ushindi hapo mbeleni.....mengine tutalekebishana baadae mbele ya safari. Karibu Dr. Slaa tuendelee mbele.

"slaa" = 'silaha"?
 
Back
Top Bottom