tanira1
JF-Expert Member
- Nov 18, 2011
- 942
- 159
kama wewe unavyomuendesha dr na chama chake.
alafu ninavyokuona kama unabifu vile na mama yetu lakini alitakusadia babu(dr) hajawahi kuishi mombasa kwa hiyo wewe mtoto wa kiume uwezi kumpata
kama wewe unavyomuendesha dr na chama chake.
Watanzania gani wanaopiganiwa na akina Nape ili wapate maisha bora. Hamuoni hata aibu kidogo tangu mwaka 2005 mnaimba wimbo huo huo wa maisha bora kwa kila mtanzania lakini kila uchao inakuwa afadhali ya jana.
Kilicho wazi ni kuwa kinachofanywa na watawala ndani ya ccm na wapiga debe wao ni kuendeleza ukwapuaji wa rasilimali za nchi na sio kudanganya kuwa mnapigania maisha bora ya watanzania.
nchi hii haitaongozwa na wahuni hata siku moja
Nitaamini kuwa mna lengo la kuhakikisha maisha bora siku mtakapokamata wale wezi wa EPA! wale wa meremeta! na kumkamata kinana kwa ujangili. Siku mtakapomuuliza Jk kwa nini anawekeza kwa Rithiwani badala ya kujitokeza kama marais wengine! Siku mtakapokamata waliotorosha fedha zetu na kuziweka mabenki ya nje wakiwaacha watanzania masikini! siku mtakayovunja mtandao wa wauza madawa ya kulevya! siku hiyo ikitimia nitachukua kadi ya CCM!!!!!!Mimi ni mtanzania kama wewe mwenye uhuru wa kuamua itikadi gani ya kisiasa siabudu binadamu; Nape ni mwanaCCM kama mimi tunasimamia na kupigania misingi ya chama kwa lengo moja tu kuhakikisha watanzania wanapata maisha bora
Chama
Gongo la mboto DSM
Unaanza kwa risala ndefu sana wakati unajua kabisa haihusiki, inaonekana kuchonga ni aina ya burudani kwako.
Kwanza kabisa naomba unielezee undugu wetu ukoje. I am not one for undugu wa lip service katika nchi ambayo undugu unatoweka faster than the speed of light, defying the known natural speed limit. Kwa hiyo kabla ya kuni patronize na undugu, naomba unieleze undugu wetu ukoje, maana huwezi hata kusema ni ndugu katika imani ya Yesu/ mungu, kwani sina imani hiyo.
I extract exactitude. Fellow JF member? yes. Ndugu? I don't know about that. Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba".
Undugu mwingi hufuga umasikini, kwani "Mtegemea cha ndugu, hufa masikini". So let's be very clear on that, sio kila mtu anapenda undugu ndugu wa jumlajumla.
Kiranga acha hasira. Huna sababu ya kutoa povu kwa kuitwa ndugu. Kama wewe ni Mtanzania huwezi kutofahamu kuwa hiyo ni namna tulivyozoezwa (socialised) kuitana. Kila lugha/jamii ina forms of addressing kama ambavyo mfano tunapoandika kwa Kiingereza kwenye email huwa tunaanza na kivumishi 'dear'. Na kwa kuwa mwenyewe umetaja unakubali labda unaweza kuwa ndunfu kama fellow JF member, huoni kuwa ulipaswa kuuliza ni undugu gani (maana unajua upo wa aina nyingi) kabla ya kuukana?
Hata hivyo kama nimekukosea kwa kukuita ndugu.... nisamehe bure!
Mwenye kuthibitisha siku zote ni yule anayesema kitu kipo, si yule anayesema kitu hakipo.
Wewe ndio mtoa madai kwamba Mungu hayupo kwa hiyo ulipaswa kuthibitisha. Kama ulitaka kuthibitishiwa ungesema hivyo mapema ili uthibitishiwe!
Naam, na nimekupa vifungu hapo juu, na vingine zaidi vipo kama unataka. The very godhead idea in it's Abrahamic manifestation is that of a repressive regime, so if one accepts that jurisprudence, why not accept of one bestowed on a demigod on earth "by the mandate of heaven". There is a reason all the oppresive Paharaohs and Chinese dynasties used this stamp to get mass approval. Read history.
Nikisema siamini kwamba mungu yupo, siwezi kusahau kuwa hakuna utawala wowote wa mungu unaopaswa kuruhusiwa kuendeleza wizi etc.
Ntasahau vipi kitu kisichokuwapo? Kisichokuwapo au usichokiamini? Kutokuamini kwako hakufanyi uwepo wa Mungu utiliwe shaka na wengine.
Utawala wa mungu ndo upi huo? Utawala wa Mungu ni aina ya uongozi wa sheria/haki ya Mungu ya upendo kwa watu binafsi (individuals) na jamii yote ya mwanadamu. Kwa bahati mbaya hatuoni hali hii katika nchi yetu au hata duniani kwa ujumla. Viongozi kumtaja/kumsingizia Mungu, haina maana wanaongozwa na Mungu. Mungu ni nani? Ni Nafsi Kuu (supreme being) ambayo ni chanzo cha uhai na uwepo wa kila kitu ulimwenguni ukiwepo wewe.
Kama mungu hayupo kutakuwaje na utawala wa mungu? Idea nzima ya "utawala wa mungu" ni ulaghai wa kuwachota binadamu akili.
Wewe unasahau kuwa laghai yeyote anaweza kutumia zana na dhana yoyote itakayofanikisha malengo yake. Ni kama mkulima wa mahindi anavyoweza kutumia mahindi yake kupikia ugali au pombe/gongo. Hivyo haiwezi kutufanya tupuuze umuhimu wa mahindi. Ulaghai unaweza kupitishiwa katika utandawazi, biashara,elimu,utamaduni, n.k.
Ukomunisti umekufa kifo cha asili, kati yangu na wewe unayeongelea Ukomunisti nani hasomi historia sasa?
Hakuna aliyezungumzia kifo cha ukomunisti. Hii ni mada mpya unayoileta.
Do not pigeonhole atheism into the constrains of Communism. I can be a Secular Humanist atheist who deplore Communism as much as I do deplore the intrinsic sheepishm in the autocratic "democracies" flagging god and country.
From the outset I disassociated myself with communist by saying "Not to be a Red Communist or anything". Do you know what that means? I am too much of a freedom lover to embrace communism.
Halafu suala likiwa kwamba wanaoamini mungu ni rahisi kuwa cajoled na tawala dhalimu, jibu liwe wanaoamini mungu na kukosa kuwa cajoled hivyo. Ukianza kuingiza Ukomunisti uliokufa utachekesha maana huna hata numbers za kufanya a reciprocal comparison. Ukomunisti umebaki wapi sasa? Korea ya Kaskazini na Cuba (Cuba nako uko kitandani kama baba yake Castro). How could you even draw a comparison?
Maneno mengi yasiyo na sababu.
Hakuna aliyesema au kukuhusisha na ukomunisti. Narudia tena hatujadili suala la kuanguka kwa ukomunisti. Kilichoelezwa hapo ni kuwa dini kama unavyotaka kutuaminisha haisababishi au kuhalalisha udikteta!!!! Ukomunisti umetolewa kama mfano halisi wa uendeshaji wa mambo bila kuhusisha imani kwa Mungu lakini unaishia kuleta udikteta. Kwa lugha nyingine dini haisababishi udikteta. Udikteta unaweza kutumia chombo chochote iwe ni dini, siasa, utamaduni, jeshi n.k kujihalalishia uwepo wake.
Halafu usitake kuleta a shallow understanding of communism through the lens of hijacked communism. Ukienda kwenye Marxism-Leninism principles utaona jinsi watu wanavyokuwa empowered kufikiri critically na sio kufuata mkumbo tu.
Hapa pia unajichanganya. Hatujadili ukomunisti kumbuka. Hata hivyo hivyo unataka kuniambia kwa uelewa wako wa critical thinking unaishia kwenye kukana uwepo wa Mungu sio? Kama ndivyo, basi tayari umeshajiweka katika sanduku (box) la kuto -embrace elimu/mawazo na dhana nyingine mpya ambazo huna na huwezi kuzipata kwa sababu umefunga mlango wa kujifunza kitu kipya. Hapa napo dhana ya critical thinking unayoilezea inakuwa shallow.
Ukishakuwa na imani ya mungu tayari ushakuwa na utegemezi katika kiongozi kukuletea maendeleo.
Mgodi utaanguka na kufukia wachimba madini, badala ya kutafuta chanzo na kukifanyia kazi utasema kama alivyosema Kikwete "Kazi ya mungu". Tayari ushajenga imani ya kumtegemea mungu kabla ya kufanya kitu. Mambo yaende kwa kudra tu. Sasa hapo kitakachokufanya ushindwe kumtegemea kiongozi wa duniani unayemuona wakati unamtegemea mungu usiyemuona ni kipi?
Mungu ni tatizo kwa sababu imani ya mungu inapalilia utegemezi.Kwenda kwa kudra za mungu,mambo inshallah inshallah.
Mtakuwa na serikali dhalimu, badala ya kupanga kuing'oa, mtataka kuomba dua mungu aiondoe, kumbe mamimamu na mapadri ni mapandikizi wa usalama wa taifa ndo kwanza wanaanza kuwasema nani na nani analeta chokochoko.
Imani ya mungu ndo uvivu wenyewe. Ukiulizwa maswali magumu usiyojua majibu yake, badala ya kujishughulisha kuyajibu, imani ya mungu inakupa jibu rahisi la kivivu "Mungu kataka hivyo". Kwisha kazi.
Kwa nini watu wavivu wa kufikiri wasiikubali sana imani ya mungu?
Ukiikataa imani ya mungu on the other hand, huwezi kuwa mvivu, kwa sababu itabidi ukatae jibu rahisi la "Mungu kataka hivyo" na kutafuta jibu lenye kina zaidi.
Hapa unazungumza vitu vingi vya kweli lakini kwa kutumia miwani yako ya kukana uwepo wa Mungu. Kwako wewe mtu mmoja mvivu wa kufanya kazi akikuambia hafanyi kazi kwa sababu anaamini Mungu atamfanikisha utamwamini huyo bila kujali kama kuna watu wengine 9 wanaoamini Mungu lakini wanafanya kazi!
Kwako wewe huoni tofauti kutowezeshwa kielimu na kiufahamu kuwa ndio tatizo ila unadhani tatizo ni dini. Kwa hiyo unaamini wewe watu wakiacha kuamini Mungu basi automatically watapata maendeleo. Ningependa kupata mifano halisi ya nchi/jamii zilizofikia maendeleo mara tu baada ya kukana uwepo wa Mungu na nyingine zinazoshindwa kupata maendeleo kwa kuwa na imani kwa Mungu.
Vitabu vya dini ni kama methali za Kiswahili.
Hapa vinakwambia "haraka haraka haina baraka" pale "ngoja ngoja huumiza matumbo" hapa "mpende adui yako" hapa vinakwambia "jino kwa jino, jicho kwa jicho" vinaji contradict. Kwa hiyo mtu mwenye kufikiri atavisoma kama ushairi wa zamani ambao hauna consistency ya kusimama katika enzi hii.
Vitabu vya dini vinajicontradict au vinapishana kutoka imani moja na nyingine? Huvitendei haki kuvijadili kwa ujumla wake wakati unajua imani ina ufanano na utofauti kati ya moja na nyingine.
Ajabu pia, ni kitabu gani cha dini specifically kinachosema 'haraka haraka haina baraka' au 'ngoja ngoja huumiza matumbo'?
Unaposema mtu mwenye kufikiri atavisoma (vitabu vya dini )kama ushairi wa zamani ambao hauna consistency ya kusimama katika enzi hii, unakosea. Vitabu vya dini vimekuwapo miaka na miaka, enzi na enzi na haviwezi kupotea kwa ujumla katika zama hizi eti kwa sababu kuna watu kama wewe unaona havina application leo. Vitabu vinavyosisitiza kufanya kazi kwa bidii, kuacha wizi na dhulma, kuacha rushwa na ufisadi vinawezaje kukosa application katika maisha ya leo? Labda kama utaniaminisha kwamba leo hakuna dhulma, wizi, ufisadi, uzembe, na ukosefu wa maadili.
Not to be a Red comrade or anything.
Mentality nzima ya "Mungu Mlinde Dr. Slaa Aiokoe Tanzania" ina matatizo lukuki, neno kwa neno.
Ukianza kwa mungu tu una deal na a hoax. Mungu hayupo. Kwa hiyo habari nzima ya mungu kutoa ulinzi ni ushairi shayiri tu.
Tanzania ina umaskini mkubwa kwa sababu ya kukataa uchunguzi na kwenda na imani imani tu, mojawapo ya msingi kabisa inayotufanya tuwe masikini ni hii ya mungu.
Watu wanaoamini kuwapo kwa mungu ni rahisi zaidi kukubali kuwa katika utawala dhalili usioheshimu haki za msingi za binadamu, kuliko wale ambao hawaamini kuwapo kwa mungu. Mungu analeta excuses kibao za kukubali udhalili. Kuanzia "utapewa malipo peponi" mpaka "watiini watawala maana wamewekwa na mungu".
Kwa hiyo kama unataka Tanzania iendelee ondoa habari za mungu katika mawazo kwanza. Mungu ni tatizo Tanzania, si suluhisho.
Mlinde? Of course kama mungu hayupo hawezi kumlinda, lakini hata kama angekuwapo. Asipomlinda - short of against death- na kumpa majaribu zaidi ndo tutamjua kama ni kiongozi bora au anaelea kwa sababu ya hali nzuri tu. Ayubu hakuthibitisha imani yake na uthabiti kwa kulindwa na mungu, alithibitisha hayo kwa kutolindwa na mungu.
Aiokoe? Kwa nini Tanzania itake mtu wa kuiokoa? Huyu Dr. Slaa ni nani mpaka aiokoe Tanzania? Yeye ni Masiha au Mahdi gani huyu?
Uongozi wetu hauhitaji charismatic figures wa kutuokoa, hatuhitaji top down leadership. Hii ina introduce a single point of failure. We have been there, done that, bought the T-Shirt to show. It is written "Nyerere, baba wa Taifa" aka Mchonga aka Haambiliki.
Kwa nini tutake strongman mwingine badala ya kutaka a grassroots empowerment? Kwa nini tusitake ushirikishwaji wa umma zaidi? Kwa nini tusitake wabunge machachari zaidi wanaohuishwa na jumuiya thabiti zenye uelewa wa mamabo zaidi?
kiukweli dr slaa ni chaguo la mungu
Da amakweli dunia imejaa wendawazimu,walio na akili zao wa kuhesabu,tangu lini simba jike amezaa mbuzi? Dr slaa ni mwanasiasa wa Tanzania,mwenye fikira za Kitanzania,hanajipya na haitatokea akawa na jipya.Inawezekana tunatumia hisia kumuona anafaa kuliko uhalisia.Na pia sisi tumekuwa washabiki wa wanasiasa badala ya kuwa wenyenchi.Na inawezekana pia hatuna vigezo vya kupima uwezo na weledi wa wanasiasa wetu tunaishia kushabikia muonekano wa nje wa watu badala ya ukweli kuhusu wao.Kila mmoja wetu afikiri mwenyewe asimpe mtu fursa ya kufikiri kwa niaba yako hatari hiyo.Fikiri peke yako,wewe mawazo uliyo nayo yako au ya kupewa? na kwanini na mpaka lini.Tafakari
Sijawahi hona mwanamke ana halalisha mumewe hawe na wake wengi kama unavyo sema wewe kupitia mfano wako wa Suleiman.
Hii ina dhihilisha wewe huna mapenzi ya kweli kwa DR SLAA ndio maana huna wivu nae sema uko hapo kwa umaskini wako (OPPORTUNIST).
Mungu amlinde DR WA UKWELI aweze kukujua ili akutimulie mbali mnafiki wa wapenzi wewe.
mungu ondoa wezi wa wake za watu katika ardhi yako takatifu
anayechagua wazinifu amelaaniwa milele, anayeunga mkono wanaolisha watu sumu ni laana kwake na kwa mungu
Hivi huyo Jk ametubu kwa kutumia kodi za watanzania kwa vimada! je wale wanaoambukiza VVU makusudi huku wao wakibadilisha damu kwa fedha za walipa kodi wako chama gani!?Atubu kwanza kwa kuasi kanisa na kuiba mke
Kiranga Subiri Kwanza,
Uko out of context,
mleta mada anaamini Mungu yupo
ndio maana anaomba ulinzi wake,
swala la wewe kutoamini uwepo wa Mungu sio sababu ya kudai hoja haina mashiko.
unapaswa kuheshimu imani za watu na sio kukurupuka namna hii.
Maelezo yako mengine yote ukiondoa huo ujinga pekee yanazungumzika.
mkuu punguza ukali wa maneno duHivi huyo Jk ametubu kwa kutumia kodi za watanzania kwa vimada! je wale wanaoambukiza VVU makusudi huku wao wakibadilisha damu kwa fedha za walipa kodi wako chama gani!?
Kwa mtaji wa UMALAYA CCM ni CHIBOKO!! funga bakuli lako!! ama sivyo sitosita kukuorodhea mambo machungu zaidi!!
I sincerely hope you can show me how.
Na mimi siamini, how is that out of context? Unajua maana ya "out of context". Wote tunaongelea imani ya mungu, how is that out of context?
Kitu ambacho mimi nimesema ni tatizo. Unataka ulinzi over Dr. Slaa? Ajili professionals wamlinde. Habari za kutegemea mungu zimewaua watu wengi, kuanzia the Gandhis mpaka Olof Palme.
Nimeonyesha jinisi gani imani ya mungu ilivyo tegemezi na vivu, inapeleka kazi ya ulinzi kwa mungu instead ya kutaka watu waifanye wao wenyewe. Hilo ni tatizo. Next thing tutaomba mvua zinyeshe badala ya kufanya mpango wa irrigation. Matokeo yake tunakufa kwa njaa katika nchi yenye maziwa na mito ya kutosha, kisa tunakesha tukiomba mungu.
Wewe utaniambia vipi mimi napaswa kuheshimu imani za watu wakati wewe huheshimu kukosa imani kwangu? Unakuita "kukurupuka"?
Ujinga wako ni hapa ulipozungumzia yasiyozungumzika, na kuacha kuzungumzia yanayozungumzika.