Ndugu yangu argument zako nazo zimekaa kishabiki zaidi kuliko dhana nzima unayoipinga na kutaka kutuaminisha. Unaposema mungu hayupo unakosea kwa sababu kuna mungu wengi sana ambao kwa wingi wanaitwa miungu! Chochote kile mtu anachoamini, iwe ni jiwe, mti, mlima na sanamu kadha wa kadha kwake mtu huyo ni mungu. Kwa hiyo unaposema mungu hayupo (existence)sikuelewi japo najua miungu hiyo inaweza kuwa haisaidii chochote!!!
Unaanza kwa risala ndefu sana wakati unajua kabisa haihusiki, inaonekana kuchonga ni aina ya burudani kwako.
Kwanza kabisa naomba unielezee undugu wetu ukoje. I am not one for undugu wa lip service katika nchi ambayo undugu unatoweka faster than the speed of light, defying the known natural speed limit. Kwa hiyo kabla ya kuni patronize na undugu, naomba unieleze undugu wetu ukoje, maana huwezi hata kusema ni ndugu katika imani ya Yesu/ mungu, kwani sina imani hiyo.
I extract exactitude. Fellow JF member? yes. Ndugu? I don't know about that. Waswahili walisema "Mtaka nyingi nasaba, hupata mwingi msiba".
Undugu mwingi hufuga umasikini, kwani "Mtegemea cha ndugu, hufa masikini". So let's be very clear on that, sio kila mtu anapenda undugu ndugu wa jumlajumla.
Lakini dhana ya mleta uzi ni kuhusu Mungu wa mbinguni ambaye pia huwezi kutushawishi tuamini hayupo bila kutupa ushahidi kitu ambacho vilevile ni subjective. Mwishowe tutaishia kukutaka ututhibitishie kama kweli hayupo na hapo tutatumia muda mwingi kubishania facts ambazo sio lengo la uzi huu.
Mwenye kuthibitisha siku zote ni yule anayesema kitu kipo, si yule anayesema kitu hakipo.
Mapungufu mengine katika hoja zako ni kuwa watu wenye kuamini uwepo wa Mungu huishia kukubali tawala dhalimu na zisizo za kidemokrasia
Naam, na nimekupa vifungu hapo juu, na vingine zaidi vipo kama unataka. The very godhead idea in it's Abrahamic manifestation is that of a repressive regime, so if one accepts that jurisprudence, why not accept of one bestowed on a demigod on earth "by the mandate of heaven". There is a reason all the oppresive Paharaohs and Chinese dynasties used this stamp to get mass approval. Read history.
lakini unasahau kuwa hakuna utawala wowote wa Mungu unaopaswa au kuruhusiwa kuendekeza wizi, rushwa, dhulma uvivu na kadhalika kwa kuwa vitu hivyo ni dhambi.
Nikisema siamini kwamba mungu yupo, siwezi kusahau kuwa hakuna utawala wowote wa mungu unaopaswa kuruhusiwa kuendeleza wizi etc.
Ntasahau vipi kitu kisichokuwapo? Utawala wa mungu ndo upi huo? Mungu ni nani? Kama mungu hayupo kutakuwaje na utawala wa mungu? Idea nzima ya "utawala wa mungu" ni ulaghai wa kuwachota binadamu akili.
Na kuhusu demokrasia, sijui kwa nini unashindwa kusoma historia ukagundua kuwa nchi nyingi zilizokana/zinazokana uwepo wa Mungu huishia kuongozwa na udikteta mfano nchi nyingi za ukomunisti!
Ukomunisti umekufa kifo cha asili, kati yangu na wewe unayeongelea Ukomunisti nani hasomi historia sasa?
Do not pigeonhole atheism into the constrains of Communism. I can be a Secular Humanist atheist who deplore Communism as much as I do deplore the intrinsic sheepishm in the autocratic "democracies" flagging god and country.
From the outset I disassociated myself with communist by saying "Not to be a Red Communist or anything". Do you know what that means? I am too much of a freedom lover to embrace communism.
Halafu suala likiwa kwamba wanaoamini mungu ni rahisi kuwa cajoled na tawala dhalimu, jibu liwe wanaoamini mungu na kukosa kuwa cajoled hivyo. Ukianza kuingiza Ukomunisti uliokufa utachekesha maana huna hata numbers za kufanya a reciprocal comparison. Ukomunisti umebaki wapi sasa? Korea ya Kaskazini na Cuba (Cuba nako uko kitandani kama baba yake Castro). How could you even draw a comparison?
Halafu usitake kuleta a shallow understanding of communism through the lens of hijacked communism. Ukienda kwenye Marxism-Leninism principles utaona jinsi watu wanavyokuwa empowered kufikiri critically na sio kufuata mkumbo tu.
Mwisho niseme tu kama lengo lako ilikuwa ni kutaka Watanzania tusiwe na utegemezi katika viongozi kutuletea maendeleo na badala yake tuyatafute sote kwa pamoja kwa kukuza taasisi za kijamii, hilo naungana na wewe lakini usihusishe na imani ya watu kwa Mungu.
Ukishakuwa na imani ya mungu tayari ushakuwa na utegemezi katika kiongozi kukuletea maendeleo.
Mgodi utaanguka na kufukia wachimba madini, badala ya kutafuta chanzo na kukifanyia kazi utasema kama alivyosema Kikwete "Kazi ya mungu". Tayari ushajenga imani ya kumtegemea mungu kabla ya kufanya kitu. Mambo yaende kwa kudra tu. Sasa hapo kitakachokufanya ushindwe kumtegemea kiongozi wa duniani unayemuona wakati unamtegemea mungu usiyemuona ni kipi?
Kwa hiyo si kweli kwamba Mungu ni tatizo,
Mungu ni tatizo kwa sababu imani ya mungu inapalilia utegemezi.Kwenda kwa kudra za mungu,mambo inshallah inshallah.
Mtakuwa na serikali dhalimu, badala ya kupanga kuing'oa, mtataka kuomba dua mungu aiondoe, kumbe mamimamu na mapadri ni mapandikizi wa usalama wa taifa ndo kwanza wanaanza kuwasema nani na nani analeta chokochoko.
tatizo ni kutokuwepo kwa imani thabiti juu ya Mungu ambayo ingetuondolea uvivu,
Imani ya mungu ndo uvivu wenyewe. Ukiulizwa maswali magumu usiyojua majibu yake, badala ya kujishughulisha kuyajibu, imani ya mungu inakupa jibu rahisi la kivivu "Mungu kataka hivyo". Kwisha kazi.
Kwa nini watu wavivu wa kufikiri wasiikubali sana imani ya mungu?
Ukiikataa imani ya mungu on the other hand, huwezi kuwa mvivu, kwa sababu itabidi ukatae jibu rahisi la "Mungu kataka hivyo" na kutafuta jibu lenye kina zaidi.
wizi wa mali za umma, ubinafsi, rushwa, dhulma, na madudu yote ambayo katika vitabu vya dini vimetajwa kama dhambi.
Vitabu vya dini ni kama methali za Kiswahili.
Hapa vinakwambia "haraka haraka haina baraka" pale "ngoja ngoja huumiza matumbo" hapa "mpende adui yako" hapa vinakwambia "jino kwa jino, jicho kwa jicho" vinaji contradict. Kwa hiyo mtu mwenye kufikiri atavisoma kama ushairi wa zamani ambao hauna consistency ya kusimama katika enzi hii.