Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 85,992
- 146,309
Naomba tutoke nje ya hapa tuzungumzie swala la uwepo wa Mungu au la, ndio la msingi kwa upande wangu, nakwenda Great Thinkers forum kuanzisha, nakukaribisha.
Unaanzisha thread nyingine kwa suala lililo katika thread hii tayari.
Nani anaenda "out of context" hapa?
Unataka kulitenganisha suala la imani ya mungu na context yake katika thread hii.
Halafu wewe ndo unalalamika mimi niko out of context!
Endeleza mpira hapahapa.
Imani ya mungu ni kati ya vitu vinavyoendeleza umasikini na utegemezi Tanzania.
Kama kilimo chetu kinahitaji maji na mvua zinakosekana, suluhisho si kuomba mungu tupate mvua, suluhisho ni kuangalia mbadala kama umwagiliaji, kupanda miti etc.
Mungu ni wazo la kikandamizaji, wanamapinduzi hawatakiwi kumtegemea mungu.