Mungu Lihurumie Taifa hili na Wananchi Wako! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mungu Lihurumie Taifa hili na Wananchi Wako!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Field Marshall ES, Feb 15, 2010.

 1. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #1
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  Mungu atuhurumie sana hili taifa siku moja turudie hizi enzi za honor and dignity kwa viongozi wetu, walikuwa na heshima, walikuwa na ustaraabu kidogo, waliwaheshimu sana wananchi, waliongea kero za wananchi sio kero za mafisadi na kulindana.

  May God Bless My Nation Tanzania.

  Respect.


  FMEs!
   
 2. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2010
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Inauma sana,kwani sasa vikao vyao vyote ni kusutana na kuumbuana,hakuna lolote wanalojadili la maana, Enzi za kuheshimiana na wakati wa kuongelea kero za wananchi umeshapita sasa ni wakati wa viongozi kujifikilia wao na matumbo yao ndugu jamaa zao na marafiki kwa mbali ndo mwananchi wa kawaida anafuata.
   
 3. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,255
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Kero kubwa ya wananchi sasa ni huku kuibiwa fedha zao, karibu zote, na viongozi. Kuzungumzia ufisadi ni kuzungumzia kero za wananchi. Zamani ufisadi ulikuweko, tena kwa sana tu, lakini ulikuwa ukifumbiwa macho.

  Iweje Mzee ES leo ulaumu viongozi wabovu kuumbuana?
   
 4. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  - Labda ungeonyesha popote nilipowahi kutetea ufisadi au mafisadi, sikubaliani na siasa za majina kwa sababu siku zote ninaamini kwamba taifa letu ni bigger than majina ya baadhi ya viongozi, siku zote ninalilia ushauri wa sound policies kwa our nation wengi hapa tunalilia majina ya viongozi ndio tofauti yetu ilipo, sililii kuwatetea viongozi wa kabila moja na dini flani hata siku moja sina hizo agenda na the most important of all sifuati bendera bila ya hoja zangu binafsi za kusimamia msimamo wangu.

  - Kuzungumzia ufisadi kwa namna ya kulindana sio kuzungumzia kero za wananchi, that is my point samahani sana naona hukuelewa siwezi hata siku moja ku-support kulindana na maovu, na ni wapi viongozi wameumbuana, mkuu vipi are you sure tupo ukurasa mmoja hapa au?

  Respect.


  FMEs!
   
 5. Field Marshall ES

  Field Marshall ES JF-Expert Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 27, 2006
  Messages: 12,659
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 0
  [​IMG]

  This is how viongozi wetu wanajitafutia uongozi, huko kijijini hakuna mwenye any-idea kwamba huyu kiongozi ana shutuma za kupewa rushwa za radar, amekodisha lori na wapambe kibao anapiga kampeni na atashinda tena...lol!

  Respect.


  FMEs!
   
 6. Augustine Moshi

  Augustine Moshi JF-Expert Member

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2006
  Messages: 2,255
  Likes Received: 348
  Trophy Points: 180
  Mzee ES,

  Majina yalishatajwa na vyombo vya kisheria. SFO imemtaja Chenge. Ripoti ya Bunge imemtaja Lowasa. Na majina zaidi yametajwa Bungeni. Sasa wana CCM waache kutaja majina eti ili waheshimiane?

  Mzee ES, CCM inanuka. Juzi Sofia Simba kajaribu kusema SFO imemsafisha Chenge. Ni uozo toka kwa watu waliooza. Hawaheshimiki, lakini wewe unataka waheshimike!
   
 7. Invisible

  Invisible Admin Staff Member

  #7
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 11, 2006
  Messages: 9,100
  Likes Received: 497
  Trophy Points: 180
  Tired...!
   
 8. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #8
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,625
  Likes Received: 23,787
  Trophy Points: 280
  .
  Mzee FMEs, enzi za honor and dignity, za enzi zile, zilitokana na hali halisi ya enzi hizo kwa sababu viongozi waliwaheshimu sana wananchi, hisi sasa ni enzi za mafisadi na kulindana viongozi wetu wanawaheshimu na kuwalinda hao mafisadi, ila wanaowachagua hao viongozi ni sisi sisi wananchi ambao viongozi wetu wanatudharau.

  October ndiyo hiyo inakuja, wananchi wenyewe ndio sisi pamoja na mimi na wewe, yule na wale, sisi na wao ili mradi, tutawapa tena!.
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,196
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  It makes me sick!!!!!!!!!
   
 10. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #10
  Feb 15, 2010
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,489
  Likes Received: 189
  Trophy Points: 160
  Mwalimu Moshi,
  Ni kweli ufisadi ulikuwepo. Lakini haukufikia kasi ya ufisadi ulio"mushroom" kuanzia enzi za Mkapa. Sasa hivi fisadi anaogopwa!
   
 11. O

  Omumura JF-Expert Member

  #11
  Feb 15, 2010
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 476
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Ama kweli, siku hizi vikao vyote vya CCM vimekuwa ni malumbano utafikiri taarabu, mie huwa nawashangaa sana wanapomualika John Komba na TOT kuburudisha wajumbe wakati wao wenyewe ni Taarabu tosha, Sophia simba anaimbisha viti maalum wengine wanafuatia, ovyo sana ni mipasho kwa kwenda mbele!
   
 12. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #12
  Feb 15, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  Mimi naamini sio wapiga vita ufisadi wote wanalengo moja, hii vita inamechukua mlengo wa visasi na kukosa fursa, hii vita inapiganwa na watu ambao mwisho wa siku hawajui kwanini hasa wanapigana, na hali hii unyima uwezo wa wapambanaji kua Imara na Madhubuti katika maamuzi yao.

  Wengi hawako tayari kupoteza nafasi zao, ulaji wao, kwa kifupi watu wengi hawako tayari kujitoa Muhanga kwa faida ya taifa.

  Inapofikia wakati wakuchukua maamuzi magumu hapo ndipo unaanza kuona mpasuko wa uoga.
   
 13. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #13
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,548
  Likes Received: 1,927
  Trophy Points: 280
  Ni mkakati tu ndugu yangu. Jamaa wamehakikisha wanatengeneza hela za kufa mtu wakati sisi tunakuwa maskini wa kutupwa ili kila siku tuwe tunapiga magoti mbele zao tukiwalilia msaada wa shida zetu. Ukiona watu wachache wanataka kumiliki utajiri wa nchi nzima unategemea nini? Hatuna namna nyingine ni kumuomba mungu huku tukijitahidi kusaidia wenzetu wengi pia wapate elimu tusiingie kwenye huu mtego wa mafisadi.
   
 14. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,196
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  By the way Where and How is Commando Salmin Amour? Mwenye data atujulishe!!
   
 15. Eric Cartman

  Eric Cartman JF-Expert Member

  #15
  Feb 15, 2010
  Joined: May 21, 2009
  Messages: 6,820
  Likes Received: 1,672
  Trophy Points: 280
  hawa viongozi wetu hawana tofauti na colonial masters wote walio wai kutupitia nia ni moja kumkandamiza mtanzania na kuifilisi tanzania.

  Tatizo sio fisadi bali ni system inayo ruhusu ufisadi, mpaka tutapo jifunza kuheshimu sheria na kuanza upya watalindana milele.
   
 16. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #16
  Feb 15, 2010
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,632
  Likes Received: 634
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba hatuwapi bali wanatuibia!! CCM ni waoga na ndio maana wanafanya kila hila juu ya mahakama kuu ya nchi kuruhusu private candidates wao bado wanapinga !! Kama waliweza kubadilisha katiba kwa dharulu baada ya hukumu ya marehemu jaji Rugakingira kuruhusu private candidates kwanini washindwe kubadili hiyo hiyo katiba kwa dharula kuwaruhusu private candidates washiriki uchaguzi mwezi October?
   
 17. W

  WildCard JF-Expert Member

  #17
  Feb 15, 2010
  Joined: Apr 22, 2008
  Messages: 7,494
  Likes Received: 100
  Trophy Points: 145
  Juzi kwenye mswada wa mapesa ya kutumia kwenye kampeni alimbana Manasheria Mkuu wa sasa akubali kuingiza matumizi ya pesa kwa ajili ya watu kama hao aliojaza kwenye lori hadi akafanikiwa. Haijulikani sasa atakuwa nao wangapi. Kwani watu wa PCCB hawaruhusiwi kumwita mahakamani akaieleza jinsi alivyopata "visenti" vile?
   
 18. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #18
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 135
  Wakuu Mungu huwa anawasaidia wale wanaanza kuonesha juhudi ya kutaka kujikwamua, tukionekana seriously tunafanya hivyo then mungu atakuwa nasi. Kama nchi hatuna mwelekeo kwa hiyo hatuwezi kumwomba mtu yoyote atusaidie kutufikisha ambako wenyewe hatujui. Ukiangalia toka ameondoka mkoloni mpaka leo hakuna lolote la maana tulilofanya, ukiangalia shule alizojenga mwingereza na tulizojenga baada ya yeye kuondoka unaweza kuona za mkoloni mpaka leo ziko intact za kwetu zinatisha, barabara labda tunaweza kuhesabu lakini nyingi tunakarabati tu za mkoloni, bandari, airports, cities ni sifuri, sanasana tumeharibu zilizokuwepo.

  Systems zote walizoacha sasa hazifuction, political systems zimefkufa, political institutions corrupt, security systems zimekuwa politicized. Yaani tunaona kuwa kila kitu rotten, ni kama tunatakiwasasa tuanze upya ile tuweze kupiga hatua. Otherwise hata Mungu atatuacha.
   
 19. TzPride

  TzPride JF-Expert Member

  #19
  Feb 15, 2010
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 2,482
  Likes Received: 457
  Trophy Points: 180
  Jamani naomba kujuzwa, hivi Mwalimu alikuwa akivaa shati la kijani nyakati za vikao au shughuli za chama? Binafsi sikuwahi kuona....maaana hawa ndugu zet huwa hata shughuli za kiserikali au kitaifa wao wanatinga kijani tu!
   
 20. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #20
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,510
  Likes Received: 7,586
  Trophy Points: 280
  Wanyantuzu wanakuambia kwanza alizoiba ni chache,hahah huyo ni Ngosha,bageshi aka bagesi
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...