Soma vizuri na uelewe kichwa cha thread cha mtoa mda uone anachouliza.
Humo makanisani kuanzia anakosali mtoa mada mwenyewe kumejaa kila aina ya sanamu, kuanzia jengo analosalia lenyewe ni sanamu, mabenchi anayokalia ni sanamu, maandishi yenyewe ya kitabu anachotumia kumjua huyo Mungu (biblia) ni sanamu pia. Mambo mengi sana yanayo mzunguka mtoa mada humo kanisani kwake anakosalia na kumuabudia huyo Mungu ni sanamu, hata yeye mwenye ni kama sanamu tu mbele ya Mungu kwa sababu kaumbwa kwa sura na mfano wa Mungu hivyo mimi na wewe na mto wote ni sanamu ya Mungu.
Labda mtoa mada angeenda moja kwa moja ni sanamu zipi izo alitaka kumaanisha, ila kama ni kwenye kichwa cha uzi kinavyosema, basi si kweli kwamba kuna sanamu ya Mungu, Sanamu ya Mungu haipo kwani tangu mwanzo Mungu baba hajawahi kuonwa na mtu isipokuwa kupitia kwa mwanae ambaye watu walimwona na waliishi naye wakamfahamu na kumbe kuchonga sanamu ya kufanana naye Isingeliwezekana.