nenda tu kanisani kaombewe, ukienda kumroga, huwezi jua unaweza kukutana na kigingi wakakumaliza ukafa kabisa. pia, kati ya waganga 10 mmoja tu ndo anaweza kuwa mkweli. sishabikii uchawi, ila unachotakiwa kujua ni kwamba, ukiamua kwenda kwa shetani unatakiwa kuwa na nguvu sana za kishetani la sivyo mashetani yenye nguvu kukuzidi hayatakucheleweza ila kukuua tu. bora ukose mume kuliko kufa. hata hao waganga wanazidiana. pia lazima tukubali, uchawi upo na wachawi wapo hadi humu maofisini. ukubali ukatae ndo hivyo. faida ya kukimbilia kwa Mungu ni kwamba, Mungu ana haki, na nguvu juu ya mashetani yooote, hivyo huna haja ya kupata shida. nenda kaokoke, umwombe Mungu, ufanye maombi ya kufarakanisha huyo mwizi wa ndoa yako. kuna mama mmoja alishafanya kama hivi ninavyokwambia, akafanya maombi, siku hiyo madawa ya mwizi wa ndoa yakashindwa nguvu na maombi kwa Mungu kwasababu Mungu alisikia maombi na kuingilia kati, mume akapata akili, alishusha kichapo hapo usiku wa manani na kubeba kila kitu, alikuwa amempangishia changudoa. saa nane usiku mke alisikia mtu anagonga, kufungua anasikia mmewe, akafunga akajua kuwa amekuja kumpiga kama kawaida, akasikia "honey nifungulie mpenzi wangu tafadhali '' kufungua akakutana na hug ya nguvu, akapigiwa magoti kuombwa msamaha wa nguvu akili si imerudiii, asubuhi na mapema akaongozana naye kukodi fuso kwenda kubeba vitu vyake kwenye nyumba aliyokuwa anaishi na mwizi wa ndoa...ilikuwa kama sinema.....icho ni kitu kidogo tu, kimbilia kwa Mungu atakutetea. ukienda kwa wachawi, labda na wewe uwe mchawi mwenzao.