Mume wangu karogwa. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume wangu karogwa.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by Kima mdogo, Oct 31, 2012.

 1. K

  Kima mdogo JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 17, 2011
  Messages: 303
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Alikua mume mwema sana,Mwenye upendo wa hali ya juu sana na mimi na mwanae,Alianza kubadilia baada ya mimi kubeba mimba,Alikua mkatili sana kwangu na hakunijali kabisa kwa kipindi chote cha ujauzito,Niliumia lakini nilijipa moyo kw huenda ni kutokana na ujauzito,...nilishtuka sana baada ya kujifungua mtoto wa kiume anayefanana naye sana akanitamkia kwa mdomo wake kuwa hamtaki huyo mtoto na ni bora ningekufa na mimba,Kwakweli iliniuma sana nikafatilia na kugundua kuwa anamwanamke anayedaiwa kazaa naye japo haina hakika km mtoto ni wake,Na inasadikika kuwa mwanamke huyo anauhusiano wa kimapenzi wa muda mrefu na mfanyakazi wa mume wangu ambaye yeye ndo alifanikisha kumtegea mume wangu dawa ili awe na uhusiano na mwanamke huyo (mwenye watoto 3) na wanashirikiana kumwendea kwa mganga ili amjengee huyo mwanamke nyumba. Nisaidieni nifanyaje jamani
   
 2. Majigo

  Majigo JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Feb 23, 2012
  Messages: 5,418
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  dawa Ya moto,Ni Kuuzima!
  Utauzima Vipi?
  Nawe Nenda Kamroge Ili Uendelee Kuongoza Majeshi!!
  MDA NDIO HUU,KIMBIA FASTA!
   
 3. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  mmmh, ipo kazi.

  Utabibu wa mapenzi si mjuzi mie.
   
 4. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  kageuzwa zuzu,Pole nawewe kamroge ngoma iwe droo
   
 5. Ennie

  Ennie JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 7,145
  Likes Received: 54
  Trophy Points: 145
  Miruzi mingi----! Wote wakishindana kuroga mwisho huyo mume atakuwa taahira kabisa kwa kuzidiwa na dawa.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,466
  Trophy Points: 280
  Ngoja aje Lara1 akushauri
  yeye ndo mjuzi wa waganga lol
   
 7. Victoire

  Victoire JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 4, 2008
  Messages: 10,453
  Likes Received: 7,217
  Trophy Points: 280
  mimi siamini katika dumba.kama zipo basi YESU ni kiboko yao,mme lazima arudi,mwite YESU mwana wa MUNGU nae ataitika na kukusaidia kumrudisha mmeo
   
 8. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #8
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Afunge na kuomba itasaidia kuondoa nguvu za giza alizofungwa nazo huyo mumeo.
   
 9. m

  muhanga JF-Expert Member

  #9
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kama una hakika na unayoyasema, basi waeleze ukweli wahusika wote watatu, hyo mwanamke, mfanyakazi na baadae mume, ukweli unamuweka mtu huru na kama huyo mwanamume atasimamia msimamo wake, muacha tu aendelee usiumie sana roho kwa ajili ya mwanamume ambeye ni binadamu mwenzako, ni kweli inauma sana lakini jipe moyo , kusanya nguvu jipange uanze maisha bila yeye, najua inawezekana kabisa, jiweke kwenye nafasi ya mjane... remember life must go on, no matter what! pole dear ndio maisha hayo
   
 10. m

  muhanga JF-Expert Member

  #10
  Oct 31, 2012
  Joined: Apr 16, 2009
  Messages: 873
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  duh Boss, hata huvalishi nguo maneno... una vituko weyeee:becky:
   
 11. Z

  Zion Daughter JF-Expert Member

  #11
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 9, 2009
  Messages: 8,936
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Kamuombee afunguliwe ndio kiboko ya wachawi... but be careful na watumishi wengine ni feki
   
 12. Angel Msoffe

  Angel Msoffe JF-Expert Member

  #12
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 21, 2011
  Messages: 6,797
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  pendekeza wazo mbadala
   
 13. T

  Tetra JF-Expert Member

  #13
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 5, 2012
  Messages: 1,523
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Kuna njia mbili,chagua ya kwenda
  (NJIA YA KWANZA)
  Funga maombi ya siri umwombee mumeo.
  Hali uliyonayo imewakuta wanawake wengi na waliofanikiwa wameshinda kwa sala.Mfungue mumeo atoke aliko ikiwemo wewe kutobishana nae,kumpenda hadi ye ashangae,onyesha mabadiliko mema yatakayoshitaki dhamira yake.KUMBUKA UTII ni silaha bora zaidi kwa sasa.USITAKE MABADILIKO YATOKEE HARAKA.
  (NJIA YA PILI)
  ni wewe kwenda kwa waganga pia umrudishe mumeo ila hasara ya njia hii ni hatari,inaongeza adui,unaweza kuzidiwa na mwezio kama kweli unaamini amerogwa.BINAFSI sikushauri utumie njia hii maana madhara yake ni kuleta huzuni zaidi kwako na wengi waliopita njia hii sasa wanajuta.
   
 14. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #14
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,325
  Likes Received: 1,792
  Trophy Points: 280
  Do you believe in superstition? I dont think the problem is with the guys who bewitch your husband. Just have a serious look who has got problems you will reliaze its your lovely husband. Kujiroga tunajiroga wenyewe
   
 15. lara 1

  lara 1 JF-Expert Member

  #15
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 10, 2012
  Messages: 15,444
  Likes Received: 10,122
  Trophy Points: 280
  Kuna njia 2 za kupitia

  1. FIGHT FOR YOU SURVIVAL
  Nenda ustawi wa jamiii kablock 75% ya Kimshahara cha mumeo ofisini ili umuhudumie mtoto,
  Mtafute huyo shankupe umpe kipondo afu mlaze ndani wiki nzima( ni haki yako kikatiba)
  Muweke vikao lukuki mumeo na wazazi wake, muaibishe kwa mchungaji na rafikize kwa kulalamika mateso

  2. Do nothing and pray!!!!! Ila jiulize je wewe ni msafi wa moyo? sala za wasiwasi hazifiki upesim.


  Ushauri wangu pambana njia za kinondoni hapo namba 1 hata mganga haoni ndani, ubabe ubabe tuuuuuu!
   
 16. epson

  epson JF-Expert Member

  #16
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  fasting coupled with persistent prayers will certainly yield exiting incredible results
   
 17. epson

  epson JF-Expert Member

  #17
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 1, 2012
  Messages: 508
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  fasting coupled with persistent prayers will certainly yield exiting incredible results
   
 18. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #18
  Oct 31, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,226
  Trophy Points: 280
  mumeo kajiroga mwenyewe kwa tamaa zake.....

  Ila kama unadhani karogwa, kaa funga omba....

  Then fuata solution namba 1 alokupa lara 1.......

  Ila kuna wanawake mna moyo isee, unamjua mwizi wako halafu umetulia.......... Baadhi Wanawake Wengine timbwili lake mwizi atahama mji na mume ndani ataishi kwa mashaka.....
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 19. HoneyBee

  HoneyBee JF-Expert Member

  #19
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 23, 2012
  Messages: 673
  Likes Received: 115
  Trophy Points: 60
  2012 hii bado tunaongelea mambo ya kurogwa? Mume wako hakuwa na mapenzi ya dhati kwako na jeuri yake itabaki pale pale ukimuachia. Yaani kimada chake na wengine unawajua lakini bado upo tu. Ongea nae, ikishindikana jipange upya au subiri aidha kufukuzwa au magonjwa.   
 20. m

  msemakwelii JF-Expert Member

  #20
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 12, 2011
  Messages: 217
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baada ya kusoma maelezo yako cjakuelewa ni kwamba jamaa anayeshea penzi na mumeo ilkuwaje yeye tena asaidie huyo dem kumroga mmeo ili ahamishie majeshi kwa mwnamke wake tena , maana umesema huyo mwanamke anatembea na mfanyakazi wa mmeo na ndiye aliyefanikisha kumuwekea libwata mmeo, Aaaah hapo Sasa, ila dawa ya moto ni moto, na wewe mtafute huyo mfanyakazi wa mmeo cheza naye dili ili upate kunako undani wa mambo then , kamtego mnaweza mnaweza fanikiwa, Kamataaaa mwizi bwanaaaa
   
Loading...