Mume wangu ana kisirani

Mume wangu ana kisirani

na ww weka kisirani , akinuna mvalie kanga ya ukinuna wenzio walaa

Akiwa bado mvalie ya bora nimpe jirani kuliko kiozee ndani

Haki ya nani atanunuka tu huyo
 
Jamani mume wangu anakisirani yani ukimkosea kitu kidogo tu anaweza kununa hata miezi sita, hatakula nyumbani, atakublock kwenye mitandao ya kijamii yote na hakuna kitu kitaendelea cha maendeleo mpaka siku ataamua kuacha kununa ndo mtaendelea kuongea.

Yani hii tabia yake nahisi kuichoka natamani mnishauri niishije na Mtu wa namna hii
Muombee kwa Mungu ili aache hiyo tabia,inawezekana...
 
hiyo miezi sita kale kahuduma ka ndoa huwa hamshiriki ? je mahitaji ya nyumban anatoa kwa kipind chote hicho \?
 
Mwanaume mzimaa ununue miezi6 tena ukute sababu ya kipuuuziiii atakapomaliza kununa mm ndo naunga mwaka mzimaa
Ebooooooooooooo
 
Nauliza je hicho kisirani alikua nacho kabla ya kukuoa au? Naomba unijibu ili nami nichangie.
 
Huko ni kumuendekeza yeye ni nani asikosewe
Selfishness ni mbaya sana sweetie! Huwezi mtesa mwenzio kusudi moyo wako upae utakacho! Huo ni unyama...
Kama kafunga na ndoa it means alikubali na kifungo "Kuishi kwa shida na raha"

Ndoa ni kujinyima dear! ukisema ujiangalie ww kama ww unadhani mwenzio ataishije? vp mumewe akijiangalia yeye kama yeye? unadhani kutakua na bond hapo? possibly NO so suluhisho hapo ni kufanya mambo yanayopendezesha pande zote!

Nadhani mama la mama anataka amuendeshe endeshe mumewe atakavyo ndio afurahi sasa mumewe kapiga chini hizo habari, mwanaume anamuendesha mwanamke! Ndio maana bible inasema "Na nyinyi wanawake muwatii waume zenu" that means order zote anazopewa na mumewe atii!
Sasa lengo la kuleta mada yake hana ni kupata sympathy basi...

Mfano mm ningekua ni huyo mume wake ningempiga chini kabisa coz sipend watu wanaojiangalia wenyewe tuu wakati upande mwingine unaumia... Maisha ni kujinyima... Hata wafanya biashara waliofika mbali kimafanikio walijinyima kula, kulala na kufanya mambo yote ya starehe ili kufika hapo walipo sasa! Egocentric kama hawa hawafiki mbali coz hawajui shida ni nn wao wanajua ndoa ni happy moment tuu shida kwao ni kifungo...
 
Jamani mume wangu anakisirani yani ukimkosea kitu kidogo tu anaweza kununa hata miezi sita, hatakula nyumbani, atakublock kwenye mitandao ya kijamii yote na hakuna kitu kitaendelea cha maendeleo mpaka siku ataamua kuacha kununa ndo mtaendelea kuongea.

Yani hii tabia yake nahisi kuichoka natamani mnishauri niishije na Mtu wa namna hii
Pole sana. Ila hicho sio kisirani bali ni hasira. Kisirani maana yake ni mikosi. Yaani huna chochote unachofanya ukafanikiwa na tatizo hilo linaondoka kwa kukutana na wataalum wa mambo hayo. Hasira sio ugonjwa wala kilema. Na dawa yake ni kusema na muhusika ili ajirekebishe tu. Na kama ni mtu msikivu anaekubali kukosolewa bila shaka atabadilika.
 
Huyo sio mume ni kigego.... achana nae.. mtu ananuna miezi sita huyo ni gogo.
 
Ha ha ha kuna sehemu nilisoma, kama mume wako ni kisirani na wewe ni kisirani mara 2
 
ase binafsi nina kisirani ila siruhusu siku ipite bila kukaa sawa...
yani ntanuna sebleni wife akiandaa chakula anaona nina stress zangu za magu anajiwahia kulala tu..njemba ntagonga movie wee..time zikisogea nampigia mama room namuomba nije kulala ..lol.. utaskia gubu limeisha..bas kitu mwakeee...
inatokeaga mara moja moja yani kitu kidogo ntafwira balaa...ila siwez lala hivyo ase ndo wife anachopendaga..nikilala anajua nimejilipua JD mwenyew
 
Huyo sio mume ni kigego.... achana nae.. mtu ananuna miezi sita huyo ni gogo.
Hata kichwani kuna shida unajua kuna watu wakili ya darasani wanazo nyingi sana lakini zamaisha yakawaida zipo zakuvukia barabara tu pale kwenye pundamilia basi
 
Ukiona hivyo hauna tabia ya kujishusha/kuomba msamaha.
 
Mwanaume mzimaa ununue miezi6 tena ukute sababu ya kipuuuziiii atakapomaliza kununa mm ndo naunga mwaka mzimaa
Ebooooooooooooo
Hilo neno yeye anamaliza leo nami naunganisha ili aone kama ni vizuri kumfanyia mwenzio, wengine huwa ni malezi mabovu na upuuzi tu ndevu uso mzima ila mambo ya kitoto
 
Ukiona hivyo hauna tabia ya kujishusha/kuomba msamaha.
Yaani hiyo ni tabia, hata kama si kujishusha ndiyo miezi 6 kweli, hapo unamimba ya miezi 6 mpaka mke anajifungua mtoto anafikisha miezi 3 ndiyo hasira zinaishi mmmmm kama sio usungura tope huo!
 
Back
Top Bottom