Mume wangu amenichunia

Mume wangu amenichunia

Habarini wapendwa wa JF

Ni matumaini yangu wote ni wazima.
Naombeni ushauri, mume wangu amenichunia yapata sasa wiki tano. Haniongeleshi na mm nmenyamaza tu maana nimeshachoka kila saa kubembeleza pale nnapochuniwa.

Nina ujauzito wa miezi sita kasoro ila huyu mwenzangu hajali hata, na ni mimba yangu ya kwanza.nateseka na haya mateso najiona kama mpweke katika ukuzaji huu wa mimba na mtu alienichunia bila sababu ya msingi. Kun wakati ninakuwa na hamu ya chakula fulani au kinywaji fulani, zamani nilikua namuomba aniletee kama nkiwa na hamu ya msos wowote na alikua analeta,kadri siku zinavyokwenda ndo hamu yangu ya kula inaongezeka nikawa namwomba alete vitu analeta kama ice cream, juice,matunda n.k
Ghafla baada ya mda kupita akaanza kunijib vbaya kila ntakachiongea naye, mara aseme namzeesha,akaacha kuniletea vyakula ninavyovipenda na kunichunia juu.
Sijui ni nn kimetokea ila inaniuma kuona nachuniwa na hana time na mm.nilishamwomba sana katika hichi kipindi cha ujauzito anijali tu na si kingine ila hana time na mm kabisa. Kwenda clinic mpka leo sijaenda nikimwomba twende ni maneno juu.
Ndugu zanguni nishaurini maana nina stress mpka wakati mwingine najuta.

Jithathmini kwanza mwenyewe kabla ya kumtuhumu mwenzio. Haiwezekani mtu akabadilika tu ghafla bila sababu ya msingi.

Ninahisi wewe ni muongeaji sana na hauchuji maneno ya kuongea na mumeo. Hauoneshi kumuheshimu. Hapo lazima akuchunie tu hakuna namna. Badilika sasa, hakuna mwanaume anapenda kuongelewa maneno ya hovyo yasiyochujwa na ukicheza atakuchunia hadi pale utakapozaa. Wanawake wa siku hizi midomo yenu haina break wala chujio, mkiambiwa kwenye majukwaa ya siasa ya kuwa mpo sawa na wanaume basi mnajiona kweli mko sawa na mnataka kuota mapembe, sasa jamaa kakuongezea mkia.
 
Jaribu kujiangalia nawe una mabadiliko gani yaliyomfanya abadilike?

Unajiachia yani hujijali tena?

Una mjibu vibaya na kua na kisirani hovyo?

Humjali wala kumuheshimu labda?

Angalia upande wako kwanza urekebishe. Jishushe na ikibidi muitie watu wazima waongee nae
Natamani ningekuwa karibu yako ningekupatia zawadi ujue. Nani alikupatia hiyo hekima, ndoa yako itakuwa na amani kweli. Unajua sisi wanaume mkeo akikuheshimu na kuonesha yupo kwa ajili yako, hata akatize mwanamke mbele yako mrembo hauwezi kumtamani.

Unastahili kuwa mke wa mume anayejitambua
 
Ila wanawake bhana, kuishi nao yataka moyo.

Ni kweli nakuwa kwenye hali kama hiyo, lakini mziki wake.

Jaribu kumwelewa na wewe kudeka mda wote kisa una mimba, hebu lifikirie hilo nalo.

Kijijini mbona hawana hayo mambo, mbona mjini mnakuwa na videko deko kisa una mimba yake.

Simtetei lakini nahisi umezidi
 
Pole sana!!!
Yaani hujaenda clinic unamsubiri huyo gubu lipungue? Jijali mwenyewe mama akati unamsubiri, ikitokea complocations za uzazi ni wewe utakae umia. Kuna watu wanapewa mimba na kukimbiwa lakinj wanajifungua vizuri.
Kama umejaribu kuunguza tatizo ni nini na hakwambii usijipe stress zaidi. We fanya yako... Ukisikia hamu ya embe, vaa viatu nenda gengeni kanunue embe lako...
Endelea kujitunza akiona humpi attention ata kwa wiki moja akili itastuka kidogo. Hali ikiendelea kamripoti kwa wazee.
Sasa hao wazee watasaidia nini. Tatizo ni yeye ajitathmini. Haiwezekani mtu over a sudden tu anabadilika bila sababu.
 
Habarini wapendwa wa JF

Ni matumaini yangu wote ni wazima.
Naombeni ushauri, mume wangu amenichunia yapata sasa wiki tano. Haniongeleshi na mm nmenyamaza tu maana nimeshachoka kila saa kubembeleza pale nnapochuniwa.

Nina ujauzito wa miezi sita kasoro ila huyu mwenzangu hajali hata, na ni mimba yangu ya kwanza.nateseka na haya mateso najiona kama mpweke katika ukuzaji huu wa mimba na mtu alienichunia bila sababu ya msingi. Kun wakati ninakuwa na hamu ya chakula fulani au kinywaji fulani, zamani nilikua namuomba aniletee kama nkiwa na hamu ya msos wowote na alikua analeta,kadri siku zinavyokwenda ndo hamu yangu ya kula inaongezeka nikawa namwomba alete vitu analeta kama ice cream, juice,matunda n.k
Ghafla baada ya mda kupita akaanza kunijib vbaya kila ntakachiongea naye, mara aseme namzeesha,akaacha kuniletea vyakula ninavyovipenda na kunichunia juu.
Sijui ni nn kimetokea ila inaniuma kuona nachuniwa na hana time na mm.nilishamwomba sana katika hichi kipindi cha ujauzito anijali tu na si kingine ila hana time na mm kabisa. Kwenda clinic mpka leo sijaenda nikimwomba twende ni maneno juu.
Ndugu zanguni nishaurini maana nina stress mpka wakati mwingine najuta.
Wahi clinic Dada,miez yote hyo hujaenda bado unasubir mumeo akubali.asipokubali itakuaje. Changamka mama n hatari kwako na kwa mtoto pia.acha uzembe.sometimes jiongeze mtoto umebeba wewe na sio yeye.chaaaaa
 
Kununiwa.... Inaboa kishenzi. Mungu awaongoze
 
Kuna wanawake wanajua kudeka bana...yani mm wa kwangu ilibidi family iingilie kati maana nilishafikia ending point....MTU kila SAA anataka uwe nyumbani,Mara niletee hki,Mara nibebe,Mara ukishangaa kakupiga Kofi nikasema eeeh...IPO cku ntachinjwa ikabidi nitoe conditions kwa familia yke...jamani kwakweli ni mtihani sana...alafu sasa akikupigia cm ukachelewa kupokea heeee....utajuta
 
Upo sahihi mkuu. Unatamani uhame nyumba. Mtu anadeka kupitiliza na mbaya zaidi akikaa na mashoga zake anawaambia namkomesha kama nini vile ,as if anafanya makusudi tu kukusumbua
 
Achana naye akafie mbali jitu zima linamchunia mtu una ujauzito wake. Kweli wanaume mabwege ni wengi sana.
 
Pole shosti lakini naomba uelewe ndio mana ukaitwa mwanamke na hizo ndio Tafran za ndoa,kipindi cha ujauzito hua kuna mikwaruzo ya hapa na pale,sisemi hujaribu kumbembeleza ila mchukulie au niseme mpuuze na muombe mungu akurudishie mumeo yule ulie mzowea na akuongeze mapenzi,bila kusahau please hospital ni muhimu usisubiri kupelekwa wewe ndio Mama mtarajiwa nilazima uhakikishe unajifungua mtoto mwenye afya njema na dr atakupa ushauri mzuri ili uweze kujifungua kwa salama,narudia tena matatizo ni moja ya maisha ya wanandoa huuu nimtihani jitahidi ushinde usikubali akakutoka kwenye mikono yako He is ur man umemjulia ndio mana amekuoa na moja ya sababu kuu niuvumilivu...
 
Kwa wakongwe wa ndoa,hapo tayari jibu wanalo!ukweli wiki5 ninyingi sana kwa wanandoa, ninaamini hapo hujajiweka wazi iliupate ushauri endelevu,kama kweli unaipenda na kuithamini ndoayako hebu funguka mpenzi iliupate majibu yenye MADINI ya nguvu,kwa uchache tu mwanamme mkewe anapokua na ujamzito hatakama alikua hana mapenzi yale ya asilimia 100 kwa mkewe agunduapo tu kunaujauzito basi hapohapo anabadilika nakuonyesha mapenzi japo hatakama yatakua ya Ku act lakini atayafanya ilimradi tu ujisikie mwenye thamani kipindi hicho kigumu kipite salama.funguka mpenzi MADINI mengi wana jmf watakujalia na tatizo lita POTELEA POLTE!
 
pole sana ila kama mwanzo alikua fresh inawezekana ww ulizidisha hamu ya kula kupita kiasi..akitoka kununua chips unamtuma akafate kachumbari akirudi unamwagiza pilau masala...
 
Muda mwingine huenda gharama za mahitaji yako zinazidi kipato chake cha siku nishauri tu labda ujaribu kuagiza aina ya chakula ambacho una hamu nacho zaidi na ambacho akileta utakila kwa kiasi na si kugusa au mtu unaleta hauli unataka tena kingine hivyo hivyo,na sio unaagiza vyakula vingi kula hauli hapo ndipo "unanizeesha" linatokea

Hayo mengine niwaachie walio oa kama walivyosema.
 
Mimba ya miezi sita hujaenda clinic? Fanya haraka uanze clinic, muende wote ili mpimwe maradhi kama HIV, muhimu sana kwenda kujua afya zenu na kiumbe kilichopo tumboni.

Huyo jamaa yako sijui nimuite vipi, huwezi kumnunia mke mwenye ujauzito, unless kwa zile imani zetu za "mimba imemkataa", otherwise hana sababu hata kama wewe ndio una makosa.
 
Habarini wapendwa wa JF

Ni matumaini yangu wote ni wazima.
Naombeni ushauri, mume wangu amenichunia yapata sasa wiki tano. Haniongeleshi na mm nmenyamaza tu maana nimeshachoka kila saa kubembeleza pale nnapochuniwa.

Nina ujauzito wa miezi sita kasoro ila huyu mwenzangu hajali hata, na ni mimba yangu ya kwanza.nateseka na haya mateso najiona kama mpweke katika ukuzaji huu wa mimba na mtu alienichunia bila sababu ya msingi. Kun wakati ninakuwa na hamu ya chakula fulani au kinywaji fulani, zamani nilikua namuomba aniletee kama nkiwa na hamu ya msos wowote na alikua analeta,kadri siku zinavyokwenda ndo hamu yangu ya kula inaongezeka nikawa namwomba alete vitu analeta kama ice cream, juice,matunda n.k
Ghafla baada ya mda kupita akaanza kunijib vbaya kila ntakachiongea naye, mara aseme namzeesha,akaacha kuniletea vyakula ninavyovipenda na kunichunia juu.
Sijui ni nn kimetokea ila inaniuma kuona nachuniwa na hana time na mm.nilishamwomba sana katika hichi kipindi cha ujauzito anijali tu na si kingine ila hana time na mm kabisa. Kwenda clinic mpka leo sijaenda nikimwomba twende ni maneno juu.
Ndugu zanguni nishaurini maana nina stress mpka wakati mwingine najuta.

Pole sana sana mamito. Hayo ni mapito tu yatapita. Ila jitahidi uende clinic aisee maana mimba ipo mwilini mwako na sio kwake. Hivi ukipatwa na tatizo lolote njiani ataisaidikaje?
Nakushauri uwazie zaidi afya yako mtoto kuliko kukaa na kumuwaza mwanaume tambua kuwa wewe sio wa kwanza kupitia hayo. Songa mbele mama ila naamini ukijifungua mambo yatakaa sawa.
 
Back
Top Bottom