Mume wangu amenichunia

blissbaby

Member
Dec 19, 2016
5
17
Habarini wapendwa wa JF

Ni matumaini yangu wote ni wazima.
Naombeni ushauri, mume wangu amenichunia yapata sasa wiki tano. Haniongeleshi na mm nmenyamaza tu maana nimeshachoka kila saa kubembeleza pale nnapochuniwa.

Nina ujauzito wa miezi sita kasoro ila huyu mwenzangu hajali hata, na ni mimba yangu ya kwanza.nateseka na haya mateso najiona kama mpweke katika ukuzaji huu wa mimba na mtu alienichunia bila sababu ya msingi. Kun wakati ninakuwa na hamu ya chakula fulani au kinywaji fulani, zamani nilikua namuomba aniletee kama nkiwa na hamu ya msos wowote na alikua analeta,kadri siku zinavyokwenda ndo hamu yangu ya kula inaongezeka nikawa namwomba alete vitu analeta kama ice cream, juice,matunda n.k
Ghafla baada ya mda kupita akaanza kunijib vbaya kila ntakachiongea naye, mara aseme namzeesha,akaacha kuniletea vyakula ninavyovipenda na kunichunia juu.
Sijui ni nn kimetokea ila inaniuma kuona nachuniwa na hana time na mm.nilishamwomba sana katika hichi kipindi cha ujauzito anijali tu na si kingine ila hana time na mm kabisa. Kwenda clinic mpka leo sijaenda nikimwomba twende ni maneno juu.
Ndugu zanguni nishaurini maana nina stress mpka wakati mwingine najuta.
 
Duh pole sana..wiki 5 hamuongeleshani kweli? Ebu jaribu kujishusha..jifanye mjinga tu hakika atabadilika!!
Nitajishusha najua tu ila kwa sasa roho inasita. Kinachonisikitisha ni jinsi navyojitoa kwake na moyo wote lakin yy kunijali tu kwa huu ujauzito ni ngumu
 
Kuna kitu kimestand out katika maelezo yako

Kivipi hujaenda clinic mpaka leo? Kwenda clinic ni very important
Kama hataki mwende wote, we nenda hata mwenyewe for the health of your unborn child na ili umalize hiyo last trimester vizuri na ujifungue salama
 
Hilo ni kawaida kwenye mimba yabkwanza na hata ya pili. Kwanza ulivyobeba ujauzito possibly umebadilika either hujijali, ama unamjibu vibaya ama umekuwa mzembe. Na yawezekana ulikatalia kidude chake cha kuchezea, unajua sisi watoto tunapenda michezo. Na kwa vile ni mimba ya kwanza mume anakuwa hana psychological experience ya mama mwenye mimba. Hivyo mabadiliko hayo ana hisi unamfanyia makusudi, na yawezekana anagegeda nje. Hata mm ilinitokea hiyo tulikuwa tunagombana kila siku. Maana mke alikuwa mkali balaa so nikaona bora niwe narudi usiku sana
 
Nenda Clinic, uzazi ni jambo zito sana,huwezi kujua utatoka damu kiasi gani so nenda kafanye vipimo ili kama ni chache wakupe dawa ubalance. Pia mtoto anatakiwa ageuzwe. Mimi kwa uzoefu wangu clinic ni muhimu mno.

Kuhusu Mabadiliko ya mumeo mimi nadhani ni kutokana na hali yako, unajua Mwanamke mjamzito kuishi nae kunataka kujishusha sana na kujitoa ufahamu. Ila ukishamjulia tu wala hakupi taabu. Hivyo huyu Mzazi mwenzio inabidi umkutanishe na mtu anaemuheshimu sana ili amsaidie mawazo jinsi ya kwenda sawa na wewe.
 
Dada naomba ujishushe tu , maana siyo yeye ni adui tu anataka kuharibu ndoa yenu nzuri.
Jifanye mjinga wala usishindane kuchuniana, maana ndoa ni mawasiliano, bila mawasiliano ndoa inakufa live. Sasa wewe mwongeleshe tu kwa namna yoyote ile ilimradi upendo uzidi kujijenga kati yenu na mtoto aliye tumboni.
 
Duuuh ndoa ngumu, hatujui pia upande wako una mapungufu gan yanayomkera
Kama sio tabia yake ya kukuchunia hvo kaen chini muongee mbembeleze hope atabadililika
 
Pole sana ila ujitahidi tu uende clinic ni muhimu sana ili kujua kama mtoto anaendelea vizuri au la. Nashindwa kumuelewa mumeo kwa kushindwa hata kukuletea chakula ukipendacho kwa kudai kwamba utamzeesha! Baadhi ya wanaume wanashangaza sana.

Habarini wapendwa wa JF

Ni matumaini yangu wote ni wazima.
Naombeni ushauri, mume wangu amenichunia yapata sasa wiki tano. Haniongeleshi na mm nmenyamaza tu maana nimeshachoka kila saa kubembeleza pale nnapochuniwa.

Nina ujauzito wa miezi sita kasoro ila huyu mwenzangu hajali hata, na ni mimba yangu ya kwanza.nateseka na haya mateso najiona kama mpweke katika ukuzaji huu wa mimba na mtu alienichunia bila sababu ya msingi. Kun wakati ninakuwa na hamu ya chakula fulani au kinywaji fulani, zamani nilikua namuomba aniletee kama nkiwa na hamu ya msos wowote na alikua analeta,kadri siku zinavyokwenda ndo hamu yangu ya kula inaongezeka nikawa namwomba alete vitu analeta kama ice cream, juice,matunda n.k
Ghafla baada ya mda kupita akaanza kunijib vbaya kila ntakachiongea naye, mara aseme namzeesha,akaacha kuniletea vyakula ninavyovipenda na kunichunia juu.
Sijui ni nn kimetokea ila inaniuma kuona nachuniwa na hana time na mm.nilishamwomba sana katika hichi kipindi cha ujauzito anijali tu na si kingine ila hana time na mm kabisa. Kwenda clinic mpka leo sijaenda nikimwomba twende ni maneno juu.
Ndugu zanguni nishaurini maana nina stress mpka wakati mwingine najuta.
 
Vumilia tu ni suala ka muda ukifanikiwa kujifungua yote haya yataisha,wakati mwingine na nyie mkiwaga wajawazito maneno yenu duuh!mara oooh mbona hukuja na chips kwani hujui kama mimi mjamzito!!!
 
Wote mmebadilika, yeye kwa kukuchunia na wewe kwa kuombaomba vitu hivyo usimlaumu.

Cha msingi ni kuelekezana na kutambua kuwa kipindi cha ujauzito ni challenging sana na si kipindi cha kujengeana lawama
 
Huyo atakuwa mvulana mana sio bure kwa mwanaume haswa anayejua ndoa na maana ya mke hawezi kufanya yote hayo.
Clinic ndio muhimu jitahidi uende kwa ajili ya afya yako na mtoto aliyeko tumboni pia.

Ila hivyo vyake ni vituko mimba ubebe wewe kununa anune yeye daah
 
Pole sana!!!
Yaani hujaenda clinic unamsubiri huyo gubu lipungue? Jijali mwenyewe mama akati unamsubiri, ikitokea complocations za uzazi ni wewe utakae umia. Kuna watu wanapewa mimba na kukimbiwa lakinj wanajifungua vizuri.
Kama umejaribu kuunguza tatizo ni nini na hakwambii usijipe stress zaidi. We fanya yako... Ukisikia hamu ya embe, vaa viatu nenda gengeni kanunue embe lako...
Endelea kujitunza akiona humpi attention ata kwa wiki moja akili itastuka kidogo. Hali ikiendelea kamripoti kwa wazee.
 
Back
Top Bottom