TANZIA Mume wa Rais Samia, Hafidh Ameir, afariki Dunia

TANZIA Mume wa Rais Samia, Hafidh Ameir, afariki Dunia

Attachments

  • Screenshot_2026-08-27-04-59-50-43_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    Screenshot_2026-08-27-04-59-50-43_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg
    145.9 KB · Views: 7
Makamo ndo katangaza hivyo
07 September 2026
Mume wa Rais Samia Suluhu Hassan Afariki Dunia Zanzibar kwa ugonjwa wa moyo

View: https://m.youtube.com/watch?v=Aec4PCXOY7k
KTN News

Mke Kukaa Eda Ya Kufiwa Na Mumewe​

Mwanamke mwenye kufiwa na mume kama hana mimba eda yake ni miezi minne (4) na siku kumi (10), na kama mwenye mimba eda yake mpaka azae, lakini iki wa amezaa kabla ya kupita miezi minne na siku kumi lazima akae eda hadi zipite, siku hizo.

Mwanamke mwenye eda ya kufiwa na mumewe, ni haramu kuvaa nguo za rangi; kujipamba kwa namna yo yote kwa mwili au kwa nguo kama kujitia manukato, kutia wanja machoni, mapodari, hina na kila jambo la kujipamba ni haramu kwake hata nguo nyeusi ikiwa ina nakshi au mkato wa kujipamba.

Eda huanzia siku ya kufa kwa mume ikiwa yupo hapo, na kama hayupo huanzia siku atakapopata habari hata kama kumepita muda mrefu sana. Katika muda huo wa eda hawezi kuposwa au kuolewa.

Uislamu unaamrisha unadhifu, basi wanaruhusiwa wanawake wenye eda kuoga kujisafisha na kuweka mwili safi, kukata kucha.

Anaruhusiwa kutoka nje kama ipo haja kama kununua mahitaji yake au kumwangalia jamaa au mgonjwa na kadhalika, asitoke nje paisipo na haja.

Tunaomba kwa Mola wetu atupe sote Twafiki ya kufuata maamrisho ya dini na kuepukana na yaliyoharamishwa au kufuata mambo ya Bida'a uzushi, usiona msingi.

1788770847216.png

07 September 2026
Unguja, Zanzibar

🔴#LIVE: MAZISHI YA MUME WA RAIS SAMIA MUDA HUU ZANZIBAR

View: https://m.youtube.com/watch?v=_iFKBRQDCQs

Source : Wasafi Media
 
Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir, amefariki Dunia.

Taarifa za kifo cha Hafidh Ameir, zimetangazwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kupitia Vyombo vya Habari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi akitangaza taarifa ya msiba wa Mhe. Hafidh Ameir Hassan ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Kipaumbele changu kikubwa katika huu Msiba ni kumuangalia Mstaafu Kikwete kama atalia Machozi ya Kweli au atalia yale Machozi ya Mamba tu pekee. Tafadhali sitaki kuulizwa swali lolote kwanini nimeandika hivi ila kwa wenye Akili kubwa nina uhakika wa 100% kuwa watakuwa wameshanielewa.

R.I.P Mzee na Pole kwa Mfiwa.
 
Mume wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, Hafidh Ameir, amefariki Dunia.

Taarifa za kifo cha Hafidh Ameir, zimetangazwa na Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi kupitia Vyombo vya Habari.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Deogratius Ndejembi akitangaza taarifa ya msiba wa Mhe. Hafidh Ameir Hassan ambaye ni mwenza wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Tunashukuru kwa taarifa
 
Allah amjalie mahala pema peponi, alijaalie kaburi lake liwe miongoni mwa bustani ya peponi. Atukutanishe peponi
Ampe subra Rais wetu katika kipindi kigumu.
 
Back
Top Bottom