Mume wa Mtu ananitaka

Mume wa Mtu ananitaka

jamani mbona mmembana sana JS!

tatizo la wanake wengi ni kuwa hawapendi kuonekana "mafedhuli, wakorofi, majeuri" hata kwa watu wasio wajua sawasawa ndio maana anajikuta hawezi kumpa ile balck and white kuwa NO.

JS shoga, si dunia ya kumuonea mtu muhali hii ....ohoooo.........liwalo na liwe mpe ukweli na ukiona huwezi usipokee simu wala msg ever
 
JS nitakupa hadithi yangu
Kulikuwa na mtoto (I call him mtoto kwa sababu he sounded like one) alikoseaga namba siku moja akapiga kwangu. Sikuwa namfahamu so nikamsalimia na kumwuliza nimsaidie nini. Akanambia anamhitaji mwenye simu nikamwambia ni mie, akajibu mbona si kama sauti ya Aunt Leila, nikamwambia basi umekosea namba. Akanijibu kistaarabu tu samahani dada yangu aksante. Akakata. Baada ya siku moja akanipigia tena- safari hii usiku wa saa tano-- akaanza na samahani dada najua nimekosea namba (eti anajua amekosea but bado akapiga!!) naomba kujua unaitwa nani na unakaa wapi? Nikamwambia samahani sasa hivi ni usiku na ningependa kupumzika. (sikuona sababu ya kumjibu naitwa nani wakati keshajua amekosea!!). Huweziamini akawa anabeep (kila dakika) kila siku usiku kuanzia saa tano sita. Mr akawa anakuja juu sana na hata nikimweleza story ilivyokuwa hakuwa anaamini nikawa naulizwa swali la Barnaba .....haiwezekani akosee namba wakati wenye simu ni wengi"... huyo ni mtu wako na mnajuana.

Ilikuwa inaniumiza kichwa sana na bahati mbaya kimeo changu hakikuwa na technologia ya kubloc so niliteseka kwa muda hadi nikafikiria sijui nimtegee nimwombe tukutane kisha nimwendee na police maana ndoa yangu ilikuwa inashake haswa kwa ajili yake (whoever he was). Maana sikuwa naweza kuzima simu usiku au kuimute -nitaambiwa nina mambo yangu ati. So nikaanza kumchunia, akibeep nakaa kinywa na Mr akirauka nakaa kimya nikaambiwa nina dharau, kiburi, jeuri na kila kisifa kilichonifaa. But alikujachoka mwenyewe akaacha yaani hadi niliicremugi ile namba!!

So what I want to write here ni kuwa usimlemaze huyo if he daa want to understand you kiutuuzima, mwaga mboga kabla hajamwaga ugali. And the more you delay ndo unarise maswali kwa Mr right wako

Yaani mwanajamiione umenikumbusha tukio kama hilo limewahi nitokea mimi pia ikiwa ndo kwanza niko kwenye mwanzo wa ndoa... kuna mtu alinipigia simu akiwa kabisa anajua na jina, cha kushtua zaidi alikuwa ni wa jinsia moja na mimi, na akawa anaandika message za mapenzi, yaani kama wewe, mwenzangu kwa nza hakuamini simjui, nikimpigia hapokei, na sikuweza mtambua, nilidhani ni rafiki zangu wananitania, lakini wapi, jamaa aliendelea nikawa na hasira, mpaka siku nikamwambia nina washikaji zangu tigo watanipa detail zake na nitampeleka polisi, ghafla akaacha.Mwenzangu alisave hiyo namba mpaka leo, lakini haipatikani... ni hatari hizi simu....
 
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.

Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.

Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??

pole sana....lakini umejifuza,ukitoa namba yako kwa stranger utegemee any strange stuff.....mkaribishe kwako na mr akiwepo....halafu mwambie aseme shida yake mbele ya mr.
rule yangu namba moja sipokei namba ya simu nisiyoijua,ndg,marafiki,jamaa wanajua hii rule[kama wana namba mpya wanatxt kuniambia]
 
Kiraka, asprin, kimey,.........kicheruko kacharuka hata anachokisema hakieleweki! Anataka atambulishwe kwa fullstop na comma
 
unatuletea ushambenga hapa jamvini, hao wote uliokwisha wapa uroda ulikuja kutuuliza hapa jamvini ? wewe mpe tu ukiamua, wewe una ala yako na yeye ana kisu chake, mpe mwanakwetuu mpe.
 
Jamani mbona mnamwonea sweetie hapa? Hakuna ubaya hata kidogo kubadilishana namba za simu si ndio connections, madili na urafiki unapoanzia? Tatizo hapa ni huyo fisi kuitumia vibaya namba aliyopewa. Ingekuwa hakuna kubadilishana simu si ingekuwa hakuna maana ya kuwa na simu basi maana kama ni kuwasiliana na nduguzo mngekutana majumbani na za kikazi mngekutana ofcn au kutulia land lines??

JS mamii huyo ni wa kumpiga stop kungali mapemaa tena asiposikia dada hebu deka kidog kwa mpenzio... mweleze taratibu kuanzia A to Z tangu mlipokutana hadi kuexchange number tena mwombe na msamaha wa kutomwambia mapema juu ya hilo (Ikibidi finya macho mpendwa ili umconvince kujutia kwako-Si ndio mapenzi yenyewe ati?)
Kisha mwombe akusaidie kuondokana na jinamizi hilo. The way I know my shem is a man enough he will know what to do lovie so dont worry

Kila la kheri

DUh...hii ni kweli MJ1, au ndio sound crafting??

Haya bana
 
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.

Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.

Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??

...m -delete tu kwenye maisha yako, unless unajiona eti wewe ndio mtatuzi wa hizo tamaa zake.
Yanini kujitafutia 'mpangaji asiyelipa kodi' kwenye mawazo na akili yako?
 
Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.

Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.

Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??

Mpatie mchezo tu, halafu baada ya hapo umwambie ukweli. Yaani kubali appointment, mpe anachotaka mkimaliza mchezo, mwonyeshe picha ya mpenzi wako. wakati wa mchezo wewe tulia tu kama mwanamke wa Kimachame, bila kujishughulisha, kuonyesha ulikuwa una mvuto naye. Atajisikia vibaya sana na harudii tena ukware. Utakuwa umeasaidia wanawake wenzako wengi na wanaume wenzetu kama hawa wenye kutaka kufunuafunua kila king'aacho mbele yao
 
Hahahah Kaizer ni kweli huwa si vema kusema kuwa umetongozwa kwanza wajua inakera na wala si sifa kwako wala kwa mpenzio lakini ukiona umemkatalia mtu kistaarabu na hasikii inapaswa kumlipua mapema kabla hajakuharibia maana hapa ni suala la kulinda interest zako ati.

Mzima lakini best? long time eeh?

mi mzima best unantia tashtiti ivo!
 
Sasa tukueleweje wewe umeshasema humtaki alafu unauliza ushari? Uko tayari kufuta ushauri wa kimapenzi ambao sio chaguo lako? Je wewe una miaka mingapi?

Kwanza jiulize hisia zako zinamkataa sababu ni mume wa mtu au sababu hujavutiwa naye kwa lolote lile?

  • Kama humtaki na anakusumbua na umekeraka kachukue mchukulie RB ya polisi . otherwise mripoti ustawi wa jamii. wamsaidie.

  • Namna gani vipi kama una "mshikaji wa karibu" wa kukusaidia mpe number ya huyo jamaa. mpe na latest script ya sms alizokutumia. Then jamaa aanze kwa kumbwatukia. Ukiona inafaaa nipe hiyo kazi mimi kama huna mshikaji wa karibu.
 
Give me a break Ngoshwe ina maana wewe hujawahi kukutana na msichana any place iwe hata kwenye starehe you had a chat mwishowe mkabadilishana namba za simu?? ina maana unakuw aunamtaka huyo msichana?? hakuna cha maswali ambayo hana majibu
Sijasema nawasiiliana naye kama umesoma between the lines
Nina simu ya kawaida haina hiyo huduma ya kublock number

Kwa wanaume JS ni kawaida kukutana na mtu na kuacha namba zako. Lakini kama mwanamke akikupa zake inakuwa ni kiashirio cha mahusiano iwe kijamii, kiuchumi, kiutamaduni au kisiasa. Pengine kwa wale waliosomea kazi za inteligensia, haishauriwi sana kuachia kontakiti zako hewani kwa mtu unaekuatana nae kwa mara ya kwanza hasa maeneo yasiyo rasmi kama klub.

Kama huwezi kublock namba yake, chomoa chip hiyo weka nyingine. vinginevyo, kama una mupenzio na unamheshimu, ukiendelea ku entertain hiyo hali itakula kwako mupenzi!.

Is better kama haupo tayari kuweka bayana tishio lako la kulipua "pentagon" yake kabla hajalipua ya kwako.

Bye.
 
Sasa tukueleweje wewe umeshasema humtaki alafu unauliza ushari? Uko tayari kufuta ushauri wa kimapenzi ambao sio chaguo lako? Je wewe una miaka mingapi?

Kwanza jiulize hisia zako zinamkataa sababu ni mume wa mtu au sababu hujavutiwa naye kwa lolote lile?

  • Kama humtaki na anakusumbua na umekeraka kachukue mchukulie RB ya polisi . otherwise mripoti ustawi wa jamii. wamsaidie.

  • Namna gani vipi kama una "mshikaji wa karibu" wa kukusaidia mpe number ya huyo jamaa. mpe na latest script ya sms alizokutumia. Then jamaa aanze kwa kumbwatukia. Ukiona inafaaa nipe hiyo kazi mimi kama huna mshikaji wa karibu.

duh! maushauri mengine yanakuja kwa kishindo!:violin::A S-coffee:
 
muweke kwenye black listed(rejected number) kwenye simu yako hapo hutapokea ujumbe wake au simu yake tabu ya nini na kwanini unajibu msg zake au nataka sitaki nini hahahahahahahahaha
 
Back
Top Bottom