Mume wa Mtu ananitaka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mume wa Mtu ananitaka

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by JS, Jul 21, 2010.

 1. JS

  JS JF-Expert Member

  #1
  Jul 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Jamani wadau naombeni msaada kuna mume wa mtu kaniganda kweli kweli. Tulikutana mtaani kwenye starehe hizi tukawa tunapiga stori na mambo kama hayo mwishowe tukabadilishana namba za simu.

  Sasa kila kukicha ni simu ni text messages. ananitaka kimapenzi. nishamuambia sina hisia kwake na kwamba nina mpenzi wangu tayari na there cant be anything between us. haelewi kabisa kagoma kuelewa.

  Nimfanyeje mtu wa aina hii na tamaa zake za mwili??
   
 2. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #2
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,030
  Trophy Points: 280
  Ndio umeamua kuja kunianika hapa? Ole wangu!!
   
 3. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #3
  Jul 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Kosa ulilifanya wewe tokea. Una wa kwako na yeye ana wa kwake, kwa nini mlibadilishana namba? Mambo mengine ni ya kujitakia tu.

  Mimi nikiwa na kwangu kamwe sitoweza kubadilishana namba na shori niliyekutana naye kwenye starehe. Huna msimamo bibie.
   
 4. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #4
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,347
  Likes Received: 22,199
  Trophy Points: 280
  Muonjeshe mara moja tu, kisha mwambie kuwa hawezi kazi.
   
 5. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #5
  Jul 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  hizo sms zicje zikaleta kasheshe kwa mpenzio cku ya cku...mkanye kwanza kwa hilo, halafu mwanaue unaemwambia una mpenzi na yeye ana mke lakini bado unakazana tu huyo c mzuri, anajua hana future na wewe so kilichobaki ni uharibifu tu.....
   
 6. roselyne1

  roselyne1 JF-Expert Member

  #6
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 18, 2010
  Messages: 1,369
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  :rolleyez:mpe mwaya...
  mume wa mtu mtamu..asikwambie mtu..
  tena kila mtu ana mpenzi wake ndio inanoga zaidi,
  akikutema si unarudi tu kwa mumeo?
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jul 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Na yeye JS nini kilimfanya ampe namba mwanaume mwenye mke? Na yeye hana heshima ya ndoa ya huyo mwanaume...
   
 8. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #8
  Jul 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0

  hilo pia ni tatizo lingine, mana mngemaliza na stor pale kila mmoja aende na lake, may b mbaba alivyoona mpaka mmeweza kubadilishana no bac pia anaweza kujaribu na mengine.
   
 9. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #9
  Jul 21, 2010
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Acha kupokea simu zake na text message zake.....................nafikiri ni kitu simple sana ambacho kitapeleka ujumbe mara moja.
   
 10. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #10
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,030
  Trophy Points: 280
  Nami nilimwambia hivyo hivyo. Anionjeshe mara moja nasepa zangu. Sasa yeye hataki matokeo yake kaja kunianika hapa! Dah!

  Ngoja nikapige valuu nipunguze mawazo!
   
 11. chloe.obrain

  chloe.obrain JF-Expert Member

  #11
  Jul 21, 2010
  Joined: Feb 25, 2010
  Messages: 391
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :A S 101: Dont answer his calls, never reply his texts, au mpe mpenzi wako simu apokee akikupigia. Ila siku ingine usirudie kugawa namba ya simu hovyo hovyo sawa mama?
   
 12. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #12
  Jul 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280
  hivi wewe JS tamaa za mwili zimekupita kando?mbona unatunyanyapaa waume wa wanawake wenzio jamani?
   
 13. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #13
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,030
  Trophy Points: 280
  Rosey unaweza kuniruhusu mtumishi wako nikutafute kwenye PM kwa amani?
   
 14. Kimey

  Kimey JF-Expert Member

  #14
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 4,119
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  hapo kwenye Red inawezekana huyo jamaa hana mke wala nn, ila si unajua siku izi watu wanapenda wale walio kwenye uhusiano kuliko ma single....may be he think you lied to him as he lied to you ndo maana anakomaa na wewe!! :clap2:
   
 15. Nyamayao

  Nyamayao JF-Expert Member

  #15
  Jul 21, 2010
  Joined: Jan 22, 2009
  Messages: 6,980
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 0
  acje akakosa yote mpenzi wake atakapojua anachezewa rafu...JS gandana na mpenzi wako wachana na mtu asiye na future na wewe, kwanza mapenzi ya kuvuizia vizia ya nini kwa warembo kama nyie?
   
 16. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #16
  Jul 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Alaaaa yeye JS alikuwa anategemea nini alipompa jamaa namba yake? Kwamba jamaa ataenda kuitundika ukutani hiyo namba kama pambo? Mademu bana...mtu unampa namba yako halafu akikupigia unalalamika...what the fcuk?
   
 17. Asprin

  Asprin JF-Expert Member

  #17
  Jul 21, 2010
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 51,041
  Likes Received: 24,030
  Trophy Points: 280
  Kiongozi mara hii ushasahau mambo ya ile thread yako maridhawa. Mambo ya ONS haya!!
   
 18. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #18
  Jul 21, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,661
  Likes Received: 1,496
  Trophy Points: 280

  sio uungwana hata kidogo......kukimbia tatizo sio suluhisho....
   
 19. JS

  JS JF-Expert Member

  #19
  Jul 21, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Kubadlishana namba na mtu haina kosa kwani by the time unampa mtu namba yako unakuwa unaestablish contact na huyo mtu. besides its a only a phone number ikiwa misused kama na huyu baba ambaye anataka kuchukulia advantage ndo inakuwa tatizo.
   
 20. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #20
  Jul 21, 2010
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,652
  Likes Received: 35,412
  Trophy Points: 280
  Heheheheheee...duuuuh sijui nimeingiwa na ibilisi gani tu. Go JS go....
   
Loading...