Miss Neddy
JF-Expert Member
- Nov 3, 2013
- 14,684
- 8,760
chagua siku akiwa ametulia ongea nae kwa kina kususa si suluhisho
hahahaaaa.. ww sio kabisaaa... uyo mwanaume atakua na matatizo. hawez kuwa mbinafsi namna hii. bibie nenda driving school uyo muache km alivyo
Tatizo nyie wanawake mnataka kuonewa huruma, wananume wengine tumepinda mkuu, kama huwezi kujiongeza itakula kwako
Una nyota ya farasi, kutembea sana
habari wana Mmu
Niko kwenye ndoa miaka 10 sasa,tumejiajiri tuna kaofisi ketu mjini,tunafanya kazi pamoja na mume wangu.
mume wangu ana gari 3,kwa kawaida yeye huwahi ofisini mapema kufungua,mm nafanya mawili matatu kwanza ili kuiacha nyumba sawa.
wakati nakwenda kibaruani humfahamisha mume wangu ambaye hunitumia usafiri wa bodaboda.Hata wakati wa kurejea home nachukua bodaboda na yy anakuja na gari yake full kiyoyozi.
Nikiomba anifundishe gari huwa hanijibu lolote(anapotezea) na ataanzisha mada nyingineeee. Maswala mengine ya nyumbani yako vizuri tatizo ni hapo tu kwenye usafiri.
Akienda na gari moja mawili yanapark hapo nyumbani yakipigwa jua na vumbi,na daily anachange analotaka.
nimechoka kutembea na bodaboda,potelea mbali,nimeamua kupiga zangu kwa mguu wakati magari yako home.
gari hizi amenunua tukiwa pamoja kwenye ndoa,wakati tunaoana hatukuwa hata na baiskeli.
Aaaghrrrrr,,,,,,,acha tu nisuse,inatia hasira sana na inanyongesha pia.
Mhhhhh! Hii kali sana, pole zako nyingi sana...Wanaume wengine wana roho mbaya kuliko hata shetani!!!! Dah!!!!
Uwe unamvizia kila akitaka kwenda kazini unamuwahi unayatoboa matairi na bisisi magari yote ili mpande bodaboda wote
wengine wana gari moja la mkopo na wanafundisha na kuwaachia hadi michepuko...huyu ana magari matatu mkewe anatembea kwa miguu...kweli kutoa ni moyo.
Miss srtong nakubaliana na wewe kuna watu wakiona familia flani mambo safi huwa wanatamani sana maisha kama hayo wakizani kuna kila raha humo ndani ya mageti kwa kweli katika familia kumi za aina hiyo ni 3 tu ndio zina enjoy life hiyo, kuna jamaa mmoja alikuwa akimwambia mmke wake kabisa wakati akitoka nyumbani na gari huna hadhi ya kupanda gari yangu kweli inasikitisha na mungu ametuma uvumilivu wanawake tupo tu mpaka lana inamkuta mwanaume anarudi hoi kukuangukia lol kweli haya mambo yanaumiza.