[QUOTE=fangfangjt;1849378]source Raia Mwema
Katika kuchangia kwenye vikao vya CCM,Bw Makongoro alitaka rais ajitenge na watuhumiwa wote wa ufisadi.
Makongoro akasema anapokaa mwenyekiti taifa ni mahali patakatifu, na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani hata siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabarani.
Akasema kule sita (kwenye eneo la ujenzi anakoshinda akichanganya yege na kupiga bati) wanasema na wanataka watuhumiwa wote wa ufisadi watoke kwenye nafasi zao.
"Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule site wanasema hapana. Atoke. Tena nawe Mwenyekiti ulipokwenda Monduli ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye, kule site wakauliza, sasa hii ndio nini?"
"Rostam simfahamu vizuri. Ninokotembelea yeye hawezi kuja na mimi siwezi kwenea anakotembelea. Sina ugomvi naye. Lakini kule site wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema ni kama timu ya mpira iliokamilika watu kwenye site wakauliza sasa hii ndiyo nini?
"Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenth. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye site , si mimi watu wanasema naye hapana."
"Ulikwenda pia Rombo , ukamuamsha mkono Mramba, kule site wakatuuliza hii nini?"[/QUOTE]
MAY B NIGEAMINI KAMA ANGEKUWA ANA USHAWISHI KAMA MWALIMU NYERERE,HIYO NGUVU YA SODA TU........