Mukama: I will fight corrupt CCM leaders | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mukama: I will fight corrupt CCM leaders

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Apr 13, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,187
  Trophy Points: 280
  Mukama: I will fight corrupt CCM leaders Tuesday, 12 April 2011 21:55

  By Habel Chidawali
  The Citizen Correspondent


  Dodoma. The newly appointed secretary general of the ruling Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mr Wilson Mukama, yesterday put on notice what he termed as corrupt elements within the party’s top leadership.Mr Mukama, who succeeded Mr Yusuf Makamba in the much-anticipated changes to reinvigorate the party, which is under increasing challenge from the opposition, is a former seasoned civil servant. It did not surprise many that only a day after assuming the key office in Tanzania’s biggest party, he was out flexing his muscles.

  He warned the party members implicated in corruption scandals to either quit or be prepared to face the music. Mr Mukama, who held various government posts, including that of permanent secretary in the Ministry of Water, before he went into retirement, was speaking at the party’s headquarters in Dodoma, only a day after taking office. For the party to regain its credibility in the eyes of the public, he said, it would have to front members not tainted with corruption.

  Speaking in an interview with The Citizen shortly after holding talks with regional CCM executives, the newly appointed party boss said the toughest challenge ahead would be to restore discipline within the party.
  However, Mr Mukama did not name names, appearing keen to let the corrupt sort themselves out.

  Announcing new members of the party’s Central Committee and secretariat on Monday, the national chairman, President Jakaya Kikwete, told the members implicated in graft to cleanse themselves within three months.
  Mr Kikwete said if they would not do so, the party would be forced to take punitive measures against them. He did also not mention any names.

  Yesterday, Mr Mukama said: “Our challenge is to build a new CCM, and this can be achieved by having only clean members. We must rebuild our party.” Mr Mukama’s assent to the top party office has been received with mixed reactions from various people, including political analysts.

  “All those implicated in corruption allegations should start quitting now in order to protect our party’s credibility,” he said. He said CCM’s ideology and policies were still generally acceptable to the people, but declared that some difficult decisions would have to be made.

  Some CCM members have been implicated in high profile graft scandals, including the infamous $30.8 million Kagoda Agriculture Company, the controversial $172 million Richmond emergency power contract and the Sh221billion Bank of Tanzania Twin Towers construction rip-off.

  To restructure the party, Mr Mukama said he would oversee major decisions made by the party’s top decision-making organs, including its reorganisation of the party from grassroots.
  He pledged to protect and cherish the party’s ideology of Ujamaa and Self-reliance, saying it had been CCM’s major policy since its founding.

  He said another challenge ahead was to make sure that the party won landslide victories in forthcoming elections. “Our mission should be to ensure that the party fulfills its obligations to make the people to have trust and vote for the it in future elections,” he said. Mr Mukama noted that CCM’s has large majority in Parliament was sound political capital. CCM has 258 MPs in the Tenth Parliament against the Opposition’s 84.

  Asked to comment on the growing competition from opposition parties, he said: “The current political situation does not deny me my sleep.”The new party chief executive spent most of his time yesterday meeting with his incoming lieutenants, including the deputy secretary general for the Mainland, Captain (rtd) John Chiligati, his Zanzibar counterpart, Mr Vuai Ali Vuai, and the party’ publicity secretary, Mr Nape Nnauye.

  Mr Mukama was appointed on Monday after two days of guessing and speculation, on who would replace Mr Makamba.In the ruling party’s new line-up, Mr January Makamba, the outgoing secretary general’s son, took the post of head of foreign affairs, replacing Mr Bernard Membe, the minister for Foreign Affairs and International Co-operation.

  However, political analysts said CCM should go a step beyond the change of personalities to enable the party cope with the demands of the current competitive political environment.Besides Captain (rtd) Chiligati, who was the publicity secretary, the rest of the secretariat comprises fresh faces now tasked with the delicate duty of handling CCM’s day-to-day affairs.

  Mr Chiligati has succeeded Captain (Rtd) George Mkuchika, while Mr Vuai has taken over from Mr Saleh Ramadhan Feruz. The National Execution Committee (NEC), one of the ruling party’s top decision-making organs, also announced names of members of its Central Committee, notably dropping political heavyweights such as Igunga MP Rostam Aziz and his Bariadi West counterpart, Mr Andrew Chenge.

  The new Mainland CC members announced by President Kikwete are Mr Abdulrahman Kinana, Ms Zakia Meghji, Mr Abdallah Kigoda, Mr Steven Wassira, Ms Pindi Chana, Mr William Lukuvi and Ms Constancia Buhiye.

  The Zanzibar CC members are Dr Hussein Mwinyi, Dr Maua Daftari, Ms Samia Suluhu Hassan, Mr Shamsi Vuai Nahodha, Mr Omari Yusuf Mzee, Mr Makame Mbarawa Mnyaa and Mr Mohamed Seif Khatibu.

  The members of the party secretariat are: Mr Mukama, Mr Chiligati, Mr Vuai, Mr Makamba (Foreign Affairs), Mr Mungulu Mchemba (Finance and Economic Affairs), Ms Asha Abdallah Juma (Organisation) and Mr Nnauye (Publicity).

  President Kikwete also named the new NEC members as Ms Anna Abdallah, Mr Peter Kisumo, Mr Mchemba, Mr Makamba, Mr Ali Juma Shamhuna, Mr Emmanuel Nchimbi, Mr Mukama and Haji Omari Kheri.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  [​IMG]

  [​IMG]

  Katibu Mkuu mpya wa CCM Wilson Mukama

  Na Waandishi Wetu Dar na Dodoma

  UPEPO wa kisiasa ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM), unazidi kuvuma kwa kasi baada ya Katibu Mkuu mpya wa chama hicho, Wilson Mukama, kutangaza kiama kwa mafisadi akitaka wajiuzulu mapema, huku Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa wa Chama hicho, Makongoro Nyerere akitajwa kuchochea maamuzi magumu dhidi ya genge hilo.Kauli hizo nzito za vigogo hao dhidi ya genge la mafisadi ambalo lina nguvu za fedha ndani na nje ya chama hicho tawala, ni sehemu ya mpango mkakati wa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, wa kukivua magamba.

  Mukama ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa chama hicho aliyetangazwa mjini Dodoma usiku wa kuamkia jana, alisema ili chama hicho kiweze kurudisha heshima yake kinatakiwa kuwa na watu safi wasiotiliwa mashaka kabisa katika jamii. Akizungumza na Mwananchi ofisini kwake muda mfupi baada ya kumaliza kikao na watendaji wa mikoa wa chama hicho, Katibu huyo alisema hana jipya atakalopeleka CCM isipokuwa yeye atasimamia weledi na misingi iliyokuwapo tangu kuanzishwa kwa CCM.

  "CCM inatakiwa kujengwa upya kabisa na ili hayo yaweze kufanikiwa, kuna kila sababu za kuwa na watu safi, hivyo mimi nawataka ndugu zangu wasimame katika misingi ya zamani tuliyokuwa nayo katika chama chetu," alisema Mukama na kuongeza:

  "Nawataka wote wenye tuhuma za rushwa na ufisadi ndani ya chama waanze kujiuzulu mapema ili kulinda heshima yao, kwani tunaingia kujenga chama sio kukibomoa."

  Katibu Mkuu huyo ambaye ana kibarua kigumu cha kusafisha chama na kukirejesha katika misingi ya waasisi wake tangu enzi TANU na CCM ya mwaka 1977, alisema mwelekeo wa CCM pamoja na sera zake bado unakubalika kwa wananchi na kuongeza: "Kinachotakiwa sasa ni kuwa na usimamizi na maamuzi magumu kwa kila mtu atakayekabidhiwa dhamana hiyo".

  Akizungumzia juu ya chama kujengwa upya alisema: "Ili tuweze kufanikiwa katika hilo mimi nitasimamia maamuzi ya Kamati Kuu ya CCM ya kukirudisha chama kwa wanachama ngazi ya chini ili wao ndio wakafanye maamuzi."

  Mukama ambaye alikuwa akizungumza kwa kujiamini alisema atasimamia kikamilifu itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea, kwa kuwa ndio sera kubwa ya CCM tangu kuanzishwa kwake.

  Jambo lingine alilosisitiza kiongozi huyo ni pamoja na kukiongoza chama katika kupata ushindi ambao hautakuwa ukitiliwa mashaka na watu wengine."Jambo kubwa na la msingi hapa ni kukiongoza chama katika kufikia malengo makubwa ya kupata ushindi usiokuwa na manung'uniko, kwani mbinu za kivita hupatikana katika medani sio uwanja wa vita," alitamba Mukama. Hata hivyo, alisifia hatua ambayo imechukuliwa na chama ambayo imesaidia kukijenga hadi sasa.

  Aliyataja mafanikio ya hatua hiyo kuwa ni pamoja na kuwa viti vingi bungeni, kwani zaidi ya asilimia 78 ya wabunge wanatoka CCM.

  Abeza nguvu ya upinzani

  Akizungumzia nguvu za upinzani, Mukama alibeza na kusema hilo haliwezi kumsumbua yeye wala kumfanya asilale usingizi, kwani anatambua ni wapi panatakiwa kusimamiwa na ni wapi panatakiwa kutolewa maelekezo yake.
  "Kwenye siasa hata siku moja ni kubwa sana huwezi kuidharau. Leo tutazungumzia miaka minne ili tuingie katika Uchaguzi Mkuu mwingine, hivyo bado kuna muda mzuri na wa kutosha kufanya maandalizi, ndio maana siwezi kutaja moja kwa moja chama kinachonipa tabu bali kitajulikana mbele ya safari," alitamba Mukama

  Ofisini siku ya kwanza

  Kutwa nzima jana, Mukama akiwa na wasaidizi wake John Chiligati (Bara), Vuai Alli Vuai (Zanzibar) pamoja na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, walifanya vikao na makatibu wa mikoa na watumishi wa CCM Makao Makuu.Awali, Mwenyekiti wa CCM Taifa, Rais Kikwete, alizungumza na watumishi makao makuu na baadhi ya makada wa chama kwa lengo la kuitambulisha Sekretarieti mpya na kuweka mikakati.

  Makamba ataka aachwe

  Kwa upande wake Katibu Mkuu aliyeachia ngazi, Yusuph Makamba, alisema huu ni wakati wake wa kupumzika kwani amechoka.Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana kuhusu uamuzi mgumu wa kujiuzulu aliouchukua mjini Dodoma hivi karibuni alisema, "Naomba mniache nipumzike... Nimechoka."
  Alifafanua kwamba ametumikia nchi kwa zaidi ya miaka 50, hivyo huu ni wakati wake kupumzika na watu wengine kufanya kazi na yeye aachwe apumzike.
  "Nimetumikia nchi hii kwa miaka mingi, nimekuwa mkuu wa wilaya, mkoa na baadaye chama, sasa ni wakati wangu wa kupumzika kwani kazi niliyofanya ni kubwa," alisisitiza.

  Katibu Mkuu huyo mstaafu aliyetuhumiwa kukigawa chama, alisema kama ni chama kimepata uongozi mpya ambao anaamini utaweza kusimamia ajenda zake kwa ufanisi.

  Makongoro Nyerere amchochea JK

  Mtoto wa Baba wa Taifa ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara, Makongoro Nyerere, amemshauri Mwenyekiti wake Rais Kikwete, kuwabwaga wote wanaotuhumiwa kwa ufisadi hata kama ni maswahiba wake kisiasa.
  Habari kutoka ndani ya kikao cha Nec, zilidokeza gazeti hili kwamba Makongoro alimweleza Rais Kikwete wakati wa kikao kuwa hana budi kuchukua uamuzi utakaowaumiza marafiki zake, ili kukinusuru chama.

  "Vitabu vitakatifu vinatueleza kuwa awali Mungu alikuwa akishirikiana kwa karibu na shetani, lakini shetani alipoanza ushetani wake, Mungu akamtimua na kumtupa uwanjani. Mungu hakai na shetani," mpasha habari wetu alimnukuu Makongoro.
  Makongoro anadaiwa kumweleza Rais Kikwete kwamba, watu wa Dar es Salaam walipokwenda kuhiji katika kaburi la baba yake, walipata jibu la kuwa Kikwete ndiye anayefaa, hivyo asivurugwe na watu wachache.

  Makongoro alimtahadharisha rais kuwa kama atachukua uamuzi wa kuilipa Kampuni ya Dowans Sh94 bilioni, hakuna Mtanzania atakayemwelewa.

  Katika hatua nyingine, uamuzi wa kuvunjwa kwa Sekretarieti na Kamati Kuu ya CCM, kumechochea wanachama kudai mabadiliko yafanyike haraka katika ngazi ya mikoa.

  Mbunge wa Kinondoni (CCM), Iddi Azzan, alisema mabadiliko yaliyofanywa ndani ya chama hicho ni mazuri.

  Hata hivyo, Azzan alisema mabadiliko hayo yanatakiwa kufanyika katika ngazi za mikoa na wilaya ambako alidai kuwa kumeoza.

  Aliitaka Sekretarieti ya Mkoa wa Dar es Salaam kujiuzulu kama walivyofanya wa Sekretarieti ya Taifa.

  Sekretarieti ya CCM, Mkoa wa Dar es Salaam inaundwa na Katibu wa CCM Mkoa, Kilumbe Ng'enda, Katibu Mwenezi, Juma Simba, Katibu wa Uchumi, Abbas Tarimba, Katibu wa Wazazi, Mustafa Yakub, Katibu wa UWT, Tatu Mariaga na Katibu wa UVCCM, Omar Mwanag'alu.

  January ajiuzulu Kamati ya Bunge

  Katika tukio lingine, Katibu wa Siasa na Uhusiano wa Kimataifa wa CCM, Januari Makamba, anatakiwa kujiuzulu nafasi yake ya Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini.

  Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, John Chiligati, alisema Makamba anatakiwa kupima uzito wa kazi aliyopewa na ile ya Bunge. Anatakiwa kubaki na ubunge kwa sababu sio kazi ya kuwajibika kila siku.

  Katika mkutano wake Nec iliamua kuwa watumishi wa chama wanatakiwa kuwapo kila siku kwa ajili ya utendaji na kwamba wanatakiwa kutenganisha viongozi wa Serikali na chama.

  Habari hii imeandikwa na Habel Chidawali na Midraj Ibrahim, Dodoma, Ramadhan Semtawa, Dar.
   
 3. Pukudu

  Pukudu JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 2,970
  Likes Received: 735
  Trophy Points: 280
  hicho ni kiini macho mbona hawawazungumzii mafisadi serikalini ambao hao ndo wanatuumiza kwa sana
   
 4. TITAN

  TITAN JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 309
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Aya sasa kumekucha, wacha waendelee kukwaruzana sisi tunasonga mbele
   
 5. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #5
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Ok this should be very interesting...
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  ....kama kusikia binadamu wanaji-organise kumtafuta Mungu ili waanzishe vita ya kung'oa u-Mungu wake.
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Apr 13, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,651
  Likes Received: 35,409
  Trophy Points: 280
  I expected him to talk tough but guess what, I've heard it all before....
   
 8. Baba_Enock

  Baba_Enock JF-Expert Member

  #8
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 6,802
  Likes Received: 164
  Trophy Points: 160
  Uandishi huu si mzuri, unaharibu mtiririko mzima wa habari!

  Tukirudi kwenye MADA:

  Kwa Tanzania hizi ni hadithi za kila mtu anapopewa madaraka! Wilson MUKAMA anao uwezo gani wa kuwafanya Andrew C, Edward, Nazir K, Basil M, Daniel Y, e.t.c wa-face music? Tusidanganyane bana!
   
 9. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #9
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  Katika vikao vya CCM vya "kujivua gamba" gazeti la Raia Mwema limeandika kwamba Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake CCM Sophia Simba, alitaka uletwe ushahidi watuhuma dhidi ya RA, vinginevyo hayo yalikuwa ni maneno ambayo yasingeweza kufanyiwa kazi.

  Hatua hiyo ilikejeliwa na Mwenyekiti Kikwete aliechomekea ya kuwa ushahidi ulikuwa ni ushindi wa asilimia 61 mwaka 2010 badala ya asilimia 82 za mwaka 2005.
   
 10. Wakumwitu

  Wakumwitu JF-Expert Member

  #10
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 22, 2011
  Messages: 373
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Hii nayo kali. mwenye hela acha aitwe mwenye hela tuu. Hata akiwa kilema ataambiwa kuwa hiyo ndiyo staili yake ya kutembea. Kila mtu atambuliwe kwa uhalisia wake na kupewa heshima sawa na mwingine. Kama amefanya madudu hela zake isiwe sababu ya kuwa mwema.
   
 11. M

  Maimai Senior Member

  #11
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  kanunuliwa huyu mama
   
 12. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #12
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  it is always sofia on the funny side, I am not surprised at all
   
 13. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #13
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  JK siku hizi anapingana na washauri wake? kweli chadema inamuumiza kichwa!
   
 14. M

  Maimai Senior Member

  #14
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  huyu semtawa amenunuliwa na chenge na anaongeza chumvi kwenye stories. Acc yake ikikaguliwa utaona cheque ambazo alikuwa anamlipa
   
 15. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #15
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  source Raia Mwema
  Katika kuchangia kwenye vikao vya CCM,Bw Makongoro alitaka rais ajitenge na watuhumiwa wote wa ufisadi.
  Makongoro akasema anapokaa mwenyekiti taifa ni mahali patakatifu, na kwa ajili hiyo pasingeweza kusogelewa na shetani hata siku moja Mungu alipata kukutana na shetani barabarani.
  Akasema kule sita (kwenye eneo la ujenzi anakoshinda akichanganya yege na kupiga bati) wanasema na wanataka watuhumiwa wote wa ufisadi watoke kwenye nafasi zao.
  "Lowassa ni ndugu yangu. Sina matatizo naye. Najua ananipenda, nami nampenda. Lakini kule site wanasema hapana. Atoke. Tena nawe Mwenyekiti ulipokwenda Monduli ukainua mkono wake juu, ukasema hujapata kuona kama yeye, kule site wakauliza, sasa hii ndio nini?"
  "Rostam simfahamu vizuri. Ninokotembelea yeye hawezi kuja na mimi siwezi kwenea anakotembelea. Sina ugomvi naye. Lakini kule site wanasema naye hapana. Ulipokwenda Igunga ukamuamsha mkono ukasema ni kama timu ya mpira iliokamilika watu kwenye site wakauliza sasa hii ndiyo nini?

  "Nasikia Chenge wanamwita Mzee wa Vijisenth. Ni ndugu yangu. Sina hakika kama anavyo vijisenti kiasi hicho. Lakini kwenye site , si mimi watu wanasema naye hapana."

  "Ulikwenda pia Rombo , ukamuamsha mkono Mramba, kule site wakatuuliza hii nini?"
   
 16. M

  Maimai Senior Member

  #16
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 174
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  ha ha ha kicheko
   
 17. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #17
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Mmmmmm,
  sofia si mhuni tu,kwani kuwa mwenyekit kitu gani?ndo maana mwenyekit wake kamjibu kihuni
   
 18. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #18
  Apr 13, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  Mzimu wa nyerere unarudi...kijana jasiri kweli.tatizo jk ataishia kucheka tu,,hata sita aliwahi kumwambia awe mkali kidogo akacheka tu
   
 19. Douglas Msele

  Douglas Msele Member

  #19
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 17, 2011
  Messages: 14
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Asante sana wa kuona hizo kasoro lakini Sitegemei kama utapata majibu!!!
   
 20. M

  Marytina JF-Expert Member

  #20
  Apr 13, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,037
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  hapo red nimepapenda sana.
  ukisoma Raia mwema on the same page JK anamkejeli Sofia Simba kuwa ushahidi wa ufisadi upo kwa ile 61% .Nashangaa JK alisingizia udini kumbe ukweli unao
   
Loading...