Muigizaji nyota, muhusika katika filamu ya Queen of Katwe Nikita Pearl Waligwa ameaga dunia

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
5,016
9,885
Muigizaji wa kike aliyekuwa mmoja wa wahusika katika filamu ya Queen of Katwe, iliyoangazia mtu mwerevu kutoka maeneo ya makazi duni ya Uganda, aliekuwa anacheza chess, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 15, kulingana na chombo cha habari cha Uganda.

Nikita Pearl Waligwa alikuwa amepatikana na uvimbe kwenye ubongo.

Katika filamu ya Queen of Katwe, iliyotoka 2016, iliakisi simulizi ya kweli ya Phiona Mutesi, ambaye alianza kucheza chess akiwa na umri wa miaka 9 licha ya kwamba hakuwa anasoma na akashiriki mashindano hadi kufikia kiwango cha kimataifa.

Katika filamu hiyo Lupita Nyong'o aliigiza kama mama yake, huku David Oyelowo akiwa mwalimu wake wa mchezo wa chess.

Waligwa aliiigiza kama Gloria, rafiki ya Phiona ambaye alimuelezea sheria za mchezo wa chess.

2016, alipatikana na uvimbe kwenye ubongo na Mira Nair mwelekezi wa filamu ya Queen of Katwe, inasemekana kwamba alitafuta watu kuchangisha pesa ili kumsaidia katika matiba ambayo alipangiwa kupata India, huku daktari wa Uganda akinukuliwa kusema kwamba hawakuwa na vifaa stahiki kwa matibabu yake.

Inasemekana kwamba mwaka 2017 alikuwa anaendelea vizuri lakini mwaka jana akapatikana na uvimbe mwingine.

BBC
 
So sad!
15 yrs Old kweli kifo hakina huruma
RIP mamii!
 
Muigizaji wa kike, Nikita Pearl Waligwa aliyekuwa mmoja wa wahusika katika filamu ya Queen of Katwe, iliyoangazia mtu mwerevu kutoka maeneo ya makazi duni ya Uganda, mcheza chess, ameaga dunia akiwa na umri wa miaka 15, kulingana na chombo cha habari cha Uganda.

Nikita Pearl Waligwa alikuwa amepatikana na uvimbe kwenye ubongo.
Katika filamu ya Queen of Katwe, iliyotoka 2016, iliakisi simulizi ya kweli ya Phiona Mutesi, ambaye alianza kucheza chess akiwa na umri wa miaka 9 licha ya kwamba hakuwa anasoma na akashiriki mashindano hadi kufikia kiwango cha Kimataifa.

Katika filamu hiyo Lupita Nyong’o aliigiza kama mama yake, huku David Oyelowo akiwa mwalimu wake wa mchezo wa chess.

Waligwa aliiigiza kama Gloria, rafiki ya Phiona ambaye alimuelezea sheria za mchezo wa chess.

2016, alipatikana na uvimbe kwenye ubongo na Mira Nair mwelekezi wa filamu ya Queen of Katwe, inasemekana kwamba alitafuta watu kuchangisha pesa ili kumsaidia katika matibabu ambayo alipangiwa kupata India, huku daktari wa Uganda akinukuliwa kusema kwamba hawakuwa na vifaa stahiki kwa matibabu yake.

Inasemekana kwamba mwaka 2017 alikuwa anaendelea vizuri lakini mwaka jana akapatikana na uvimbe mwingine.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…