Luis Armstrong: Musicians do not retire. They just stop playing.

Damaso

JF-Expert Member
Jul 18, 2018
1,590
2,088
Frank Sinatra, John William Coltrane, Miles Dewey Davis au Dean Martin, wengine wanaweza kusema kuwa kuna mwamba Nat King Cole, au wakati mwingine Bing Crosby ila binafsi acha nimtaje Mzee wa kazi Louis Daniel Armstrong maarufu kama Satchmo ama Pops, moja ya wanamuziki wakubwa waliotumia vyema sana talanta yao za uimbaji wa upigaji wa tarumbeta, sauti yake ni mfano wa pamba laini ya Merino kutoka Australia. leo natamani nikupitishe kwa uchache kwenye historia tamu ya Armstrong.
sinatra_wide-e82beae0454312f8aa480f138232ea2be372ba8b-s1400-c100.jpg

Kumsikiliza Armstrong akiimba ni mahaba tosha ni sawa na kufurahia mvinyo wa Masseto Toscana ukiburudisha koo lako taratibu huku ukisikiliza vibao vikali kama vile, A Kiss to Build a Dream On wimbo ambao uliandikwa na watunzi magwiji kweli Bert Kalmar, Harry Ruby pamoja na Oscar Hammerstein II huku Armstrong akileta ufundi na ustadi wake kwenye kutoa mahaba kutpitia mashairi yake;
luis.jpg
Give me a kiss to build a dream on

And my imagination will thrive upon that kiss

Sweetheart, I ask no more than this


A kiss to build a dream on………….

Louis Daniel Armstrong alizaliwa Jumamosi ya Agosti 4 mwaka 1901 huko New Orleans na ikawa ni nyota bora sana ambayo ilitoa mwanga mkubwa na njia pevu katika muziki wa Jazz, kipindi hicho kulikuwa na taita mmoja ambaye alijulikana kwa jina la Papa Jack Laine ambaye huyu ndo aliunganisha wanamuziki wazungu pamoja na wenye asili ya Afrika kwenye bendi yake, aliwapatia ujira watu kama vile George Brunies, Sharkey Bonano , mara kadhaa Papa Jack Laine alitambulika kama The Father of White Jazz.
Louis-Armstrong-and-the-Jewish-Family-730_x_411.jpg

Armstrong alitubariki wapenda jazz kwa vibao vikali sana, mfano, include "What a Wonderful World", "La Vie en Rose", "Hello, Dolly!", "On the Sunny Side of the Street", "Dream a Little Dream of Me", "When You're Smiling" pamoja na kile cha "When the Saints Go Marching In". ulikuwa ukitaka kuona moto basi mkutanishe Armstrong dhidi ya Duke Ellington, ukiweka On the Sunny Side of the Street ya Armstrong basi huku naweka Take the A Train ya mwamba Duke Ellington.
louis-armstrong-2_wide-b5d9e841d468185e26f30e2e4ba5d63a5a8116a6-s1400-c100.jpg

Asanteni sana kwa kutuletea nyota hii Mary Estelle Albert pamoja na William Armstrong, nyota yeu ni zaidi ya Sirius ukiitazama usiku tulivu kwenye fukwe za Palm Cove, Australia. Armsrong umetuacha urithi mkubwa sana Keith Jarrett, Ornette Coleman, Norah Jones, Jason Moran, Vijay Iyer pamoja na Brad Mehldau, wote hawa wamepata kuona njia kutokana na mwanga ambao uliutoa wewe ktika harakati za kuufanya muziki wa Jazz uwe sehemu ya dunia.
Louis-Armstong-Courtesy-Louis-Amstrong-House-Museum-1000x600.jpg

Armstrong mtaa ulikulea kweli, na sio kelele za kina Mwaisa, miaka ya X mtaa wa Rampart Street huko New Orleans ulikuwa ni moja ya mitaa masikini sana ambayo waliishi watu weusi, haswa upande wa kusini ambao uliitwa kwa jina The Battlefield, kwa hakika ulikuwa ni uwanja wa vita, vita dhidi ya elimu ya kibaguzi, vita dhidi ya huduma mbaya za afya, lakini kubwa ilikuwa ni vita dhidi ya mfumo wa kijamii ambao ulikuwa ni wa kipuuzi sana.

Kutoka kuishi kwenye mtaa hatari mpaka kwenda kufanya kazi katika familia ya Kiyahudi ya Karnoffskys, familia ambayo ilitoka Lithuania na kuingia Marekani na kuweka kambi huko New Orleans, hakika ulipiga kazi ukiwa na umri mdogo tu ila ulikuwa unajua kuwa Mungu yupo nawe kila hatua.
1948-Louis-and-Lucille-with-Ed-Sullivan-and-Helen-Hayes-1.png

Familia hii ya Karnoffsky ilikuwa ni familia dunia na iliona kuwa ni vyema ikaishi vizuri na Armstrong ambaye alikuwa ni kama sehemu ya familia, walimpenda sana na wakati mwingine walikaa naye pamoja na kuimba nyimbo kadhaa ili kuburudika pamoja. Kwa heshima na moyo wa shukrani, Armstrong alitunga wimbo mahususi kwa ajili ya familia hii, Russian Lullaby ambao ulikuwa ukimzungumzia kijana wa familia hii ya Karnoffsky aitwaye David alipokuwa akitaka kwenda kulala, na Armstrong mara kadhaa alionesha shukrani kwa familia hii kwa kumfundisha kuimba na kutoa mashairi moyo, huku akitumia hisia kuandika mashairi na tunzi zake kadhaa.

luia.jpg

Wengi wanaweza kushangaa je kwanini familia ya kiyahudi iliyotoka Lithuania na kuhamia Marekani tena New Orleans inawezaje kumkubali na kumpenda kijana mweusi kama Armstrong tena kwa upendo wa agape!? Ilikuwa hivi, familia ya Karnoffsky kama familia zingine za wahamiaji zilikutana na unyanyasaji na ubaguzi wa kutisha kutoka kwa wazungu, miaka ya 1907 (wakati kina Kinjekitile Ngwale, Nasr Khalfan pamoja na Hemedi Muhammad wanatembeza kichapo kwa wajerumani kwenye Maji Maji.

Hivyo hii ilitosha kuwafanya Karnoffsky kuwapenda sana watu ambao wapo nao kwenye kundi moja, waliwapenda sana watu weusi kiasi kwamba walifanya sehemu ya familia yao, Morris Karnoffsky alimpenda snaa Armstrong na mara kadhaa ndiye aliyekuwa akimpa moyo na kumfundisha mambo kadhaa kuhusu namna ya kuishi katika ubaguzi wa wazungu.

zbiography.jpg

Jumatatu ya mwisho wa mwaka 1912 yaani Disemba 31 Armstrong ukajichanganya mzee wangu, ulikamatwa na Polisi mara baada ya kuchukua bastola ya Baba yako wa kambo na kupiga risasi moja juu, ukasherekea sikukuu ya Mwaka mpya ukiwa New Orleans Juvenile Court na asubuhi ukahukumiwa kwenda Colored Waif's Home kwa ajili ya kutumikia adhabu yako, Colored Waif's Home ilikuwa ni kituo maalumu kwa ajili ya Vijana watukutu wenye rangi nyeusi (wazungu hawakutaka kuweka vijana wao kwenye vituo vya urekebishaji wa tabia pamoja na vijana wenye rangi nyeusi, jamaa walikuwa wabaguzi hatari).

Maisha ndani ya kituo cha Colored Waif's Home hayakuwa mepesi kama unavyodhania, kama Shimolatewa au Shikusa kwa Wakenya basi badi muziki wake ulikuwa ni mkubwa sana, au pale Kampiringisa kwa Mseveni. Ila ukweli ni kwamba Colored Waif's Home haikuwa sehemu salama kwa Watoto kwani hakukuwa na usimamizi makini wa Watoto, na Maisha ndani ya Colored Waif's Home yalikuwa ni kile tunachokiita Survival of the fittest, hakukuwepo na vitanda, na hakukuwepo na chakula cha kutosha, mara kadhaa walikuwa mikate tena mlo mmoja tu.

zGettyImages-91141718-5b58ef8d4cedfd004b1456dd.jpg

Kila sehemu una mtu anayefanya Maisha yawe magumu kwa kila namna, basi Colored Waif's Home walipata kuwa na kiongozi mkuu wa kituo, bwana mkubwa Captain Joseph Jones ambaye aligeuza kituo hiki na kuwa kama vile kambi ya kijeshi na mara kadhaa alitumia adhabu kali sana kwa Watoto endapo ukikosea. Akiwa kituoni hapo Armstrong alianza kujifua zaidi kwenye talanta yake ya muziki huku akiimba katika band akiwa pamoja na Peter Davis ambaye alimsaidia kumuombea ruhusa mara kadhaa Armstrong kutoka kwa Captain Jones. Kutokana na tabia njema ilikuwa ni rahisi sana kwa Captain Jones kumpatia ruhusa Armstrong kwenda kutoa burudani kwa watu, taratibu Armstrong akawa muimbaji kiongozi wa bendi akiwa na miaka 13 tu.
zLouisArmstrong.jpg

Mwamba ulikuwa unapenda sana kupiga kidogo majani, ukiwa na swahiba yako Vic Berton, mwaka 1930 mlitiwa nguvuni m=baada ya kushikwa mkiwa na majani aka Bangi, mko zenu ndani ya Cotton Club huko California basi mkajiachia we! Kumbe Polisi wanawachora tu. Uliwahi kusema kuwa “a thousand times better than whiskey”.

Sifa zake zikamfikia gwiji Kid Ory na kumsifia sana dogo kuwa anajua kucheza na ala za muziki kama vile Pele alipowatia goli tatu Ufaransa kwenye hatua ya Nusu fainali ya Kombe la Dunia la Mwaka 1958 akiwa na miaka 17 tu, Kid Ory ambaye alitupatia chuma kizito sana cha Song of the Wanderer, aisee Jazz ilikuwa ikipigwa basi lazma shughuli zisimame kwamba tuanze kucheza Cakewalk pamoja na Lindy Hop, mitindo ya kucheza ambayo wengi walikuwa wakicheza kwa ustadi na mahaba makubwa.

zzz.jpg

Kazi ya upigaji wa tarumbeta ni kazi ngumu sana na wakati mwingine huleta matatizo kwenye mdomo, ulimi, kwenye mishipa ya shingo, pamoja na taya. Vivyo hivyo kwa Armstrong ambaye ukiacha tu kutuburudisha kwa nyimbo zake na ala tamu za muziki pia alikutana na kadhia hii ya ajabu. Akiwa kwenye ziara zake za kimuziki barani Ulaya, Armstrong alipata michupuko kwenye mdomo na ilimbidi kuacha kupumzika kwa mwaka mzima, ila sasa makampuni yakaona ni sehemu ya kumtumia kujitangaza kibiashara, Armstrong akawa msemaji wa bidhaa ya Ansatz-Creme Lip Salve katikati mwa miaka ya 1950.

Mwaka 1959 Armstrong akiwa backstage na Marshall Brown ambaye pia alikuwa msanii, Armstrong alipewa ushauri wa kitabibu kutoka kwa daktarin kuwa atumie muda wake kutibu majeraha ya midomo yake kwa kutumia dawa na sio lip bam au vipodozi, ila mwamba akagoma na kusema kuwa hana muda wa kupumzika, ila taratibu hali yake ikawa mbaya zaidi kiasi kwamba madaktari walishindwa kumtibu ten ahata kwa upasuaji.

zzzzz.jpg

Mwaka 1959 Armstrong alilazwa hosptali mara baada ya kupigwa na homa ya mapafu akiwa kwenye ziara ya muziki huko Italia, madakari wakamshauri kuwa kutokana na hali dhoofu yamapafu yake pamoja na moyo ni vyema aseme imetosha na aache kufanya ziara za kimuziki na atulie ale pensheni yake, lakini mamba alipumzika kidogo tu na Juni 26 alirudi kazini.

Lilpokuja suala la kuacha kuimba kiukweli Armstrong alikuwa mithili ya Nzangamba, alikuwa hataki kusikia ushauri wa madaktari kuwa apumzike na atazame afa yake. Machi 1971 mara baada ya kuwapatia watu ladha ya muziki wa Jazz kwenye ukumbi wa Waldorf-Astoria's Empire Room, Armstrong alipata mshtuko wa moyo na kulazwa, alikaa hospitali chini ya uangalizi wa madaktari na mwezi Mei aliruhusiwa hku wakimsihi kuwa aache muziki kwa faida ya afya yake ila ajabu ni kwamba mwamba alirejea tena kazini, ila kwa bahati mbaya Jumanne asubuhi ya tarehe 6, Julai 1971 Armstrong alifariki duniani kutokana na kupata mshtuko wa moyo akiwa amelala.

zzzzzzzzzgettyimages-84999231-1024x1024.jpg

Kwa heshima yake na kazi ubwa ambayo aliifanya katika muziki, jeneza lake lilisindikwa na watu kama vile, Bing Crosby, Ella Fitzgerald, Dizzy Gillespie, Pearl Bailey, Count Basie, Harry James, Frank Sinatra, Ed Sullivan, Earl Wilson, Alan King, Johnny Carson pamoja na mzee wa kazi David Frost, kikosi kazi ambacho kilimpa heshima kubwa sana bwana mkubwa Armstrong.

zzzzzzzzzzzz716eb6e1070edcccb994942fc76559fe.1000x1000x1.jpg

Al Hibbler akiwa kwenye majonzi makubwa aliimba wimbo wa Nobody Knows the Trouble I've Seen, ambao uliwapa tumaini wanafamilia na wapenzi pamoja na mashabiki wa Armstrong, Swahiba yake mkubwa, Fred Robbins alitoa neon la shukrani na kuelezea kwa ufupi Maisha na Armstrong.

Kwa heshima ya Armstrong, 2001 Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa New Orleans ulitoa nafasi ya kuitwa jina la Armstrong na hivyo kujulikana kama Louis Armstrong New Orleans International Airport, huku sehemu ya kuingia uwanjani kukiwa na sanamu kubwa la Armstrong akiwa anapiga tarumbeta yake.


Louis-Armstrong-New-Orleans-International-Airport-MSY-1024x616.jpg

Huko New Orleans kulikuwa na sehemu inaitwa Congo Square, au Makutano ya Congo ambapo watu wenye asili ya Afrika walikutana na kucheza na kusikiliza nyimbo mbalimbali, bsi makutano hayo yamepewa jina la Louis Armstrong Park, huku pia kukiwa na sanamu kubwa la futi 12 la Armstrong akiwa ameshika tarumbeta mkononi.

Mahali abapo Armstrong aliishi kwa zaidi ya miaka 28 kwa sasa ni makumbusho, ambapo watu huenda kutazama na kujifunza namna ambavyo Armstrong aliishi na kutumia talanta yake ya muziki. Makumbusho hii inaendeshwa na Chuo cha Queens College.

usa.jpg

Hadithi ya Maisha yako ni ndefu sana, uliwahi kumkandia vya kutosha Rais Dwight D. Eisenhower juu ya ubaguzi, na wengine wakadai kuwa ulimtunga utunzi kuhusu kumchana ila baadaye ukaona ni ujinga. Asante sana kwa Jazz tamu! Asante kwa kuwafanya wazungu waipende jazz mpaka dunia tukawapata watu kama vile, Elizabeth Woolridge Grant, maarufu kama Lana Del Rey, marehemu Amy Jade Winehouse, pamoja na Joe Jackson.
Louis_Armstrong_1955-640x360.jpg
Asante sana Mpambanaji! Tumelimiss sana tabasamu lako!

“Musicians do not retire. They just stop playing”
 
Huu mziki ni kama unakufa hivi. Ukitaka kuenjoy classic jazz ni lazima urudi 20th century. Kwa sasa ni kina nani wanafanya jazz bora nijaribu kuwasikiliza
 
Huu mziki ni kama unakufa hivi. Ukitaka kuenjoy classic jazz ni lazima urudi 20th century. Kwa sasa ni kina nani wanafanya jazz bora nijaribu kuwasikiliza
Bado upo hai ila kwa uchache sana Mkuu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom