Muhongo atoroka!

Muhongo atoroka!

Waziri Mwiguli alisema hao watuhumiwa wa makinikia hawataruhusiwa kutoka nje ya nchi isipokuwa kwa kibali maalum sasa yeye katokaje na ameenda wapi?
Mwigulu naye ni walewale tu ccm
 
Kwa Nipashe habari ya Muhongo sidhani kama naweza kuiamini sana, nakumbuka Muhongo alimwambia mzee Mengi akawekeze kwenye juice, gesi siyo mziki wake.
...Hata gazeti la Uhuru wameandika mkuu.
 
sasa the ya nini, what are you particularizing? by the way humu ni mahali mizaha mizaha. Nikifanya hivi kwenye thesis au publication, kwenye peer reviewed journal/or any journal, then you can raise concern!
Maneno mengii lakini kosa lipo pale pale. Kwani dhambi kujisahihisha? Eti "humu ni mahali mizaha mizaha".
 
'sijapata kuona waziri muongo kama huyu prof.Muhongo..

narudia tena! ...Sijapata kuona waziri muongo kama huyu prof.Muhongo..' by Tundu Lissu
Hayo maneno hakusea lisu alisema kigwangala tena ilikua bungeni kwenye ishu ya escrow
 
Muhongo ana mishemishe nyingi za kimataifa, na hata akiondoka nchini siwezi kushangaa.
 
Nimecheka hii habari [HASHTAG]#Takukuru[/HASHTAG] kuhamia kashfa nyingine#
 
Kumchafua kivipi? Wamekuonyesha chanzo kuwa in Katibu wa Bunge. Na MTU asipoonekana bungeni bila taarifa nyaraka za bunge zinamtaja kama MTORO.
Jee mtu mtoro katenda kosa gani kama sio KUTOROKA?
Nitashangaa sana kama kuna mtu atalaumu gazeti
Kutoroka wapi? Bungeni au nchini?
 
Aliyekuwa Waziri wa nishati na madini prof. Sospeter Muhongo, hajaonekana Bungeni mjini Dodoma bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita .



Mei 24, mwaka huu, Ris John Mgufuli alitengua uteuzi wa prof. Muhongo katika baraza la mawaziri, ikiwa ni muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa machanga wa dhahabu (makinikia)



Mtaalamu huyo wa jiolojia wa kimataifa hakuwapo bungeni wakati uteuzi wake wa uwaziri ukitenguliwa, huku taarifa zikidai kuwa alirudi nyumbani kwao, Musoma Mkoani Mara, kuhudhulia mazishi ya dada yake.


Katibu wa bunge DK. Thomas Kashililah, alisema ofisi yake haina taarifa ya mbunge huyo wa Msoma Vijijini (CCM) jambo ambalo ni kinyume na utaratibu.


Kiongozi huyo wa bunge pia alisema ofisi yake haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri mwishoni mwa mwezi uliopita


DK. Kashililah aliongeza kuwa kwa kawaida mbunge anapokuwa na udhuru , humwandikia Spika kumuelezea hatakuwa bungeni kwa muda Fulani na ofisi ya KAtibu wa Bunge hupewa nakala.


“Sijapata nakala yeyote ya udhuru, wa profesa Muhongo na wala sijui alipo tangu siku ile,” alisema DK. Kashililah.


Katibu wa Bunge huyo alisema hii ni mara ya pili kwa Muhongo kuondoka Bungeni kwa muda mrefu bila ya ruhusa kwani hata alipomwandikia barua ya kujiuzulu Rais wa awamu ya nne, Jakaya Kikwete, hakuhudhulia bunge kwa muda mrefu.


Prof. Muhongo alijiuzulu nafasi ya uwaziri wa Nishati na Madini Januari 24,2015 kwa shinikizo la Bunge, kutokana na taarifa ya kamati moja ya chombo hicho juu ya kashfa ya uchotwaji wa fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.
 
Back
Top Bottom