Muhongo atoroka!

Muhongo atoroka!

Hilo ni gazeti la Mzee kutoka Machame ambaye alikuwa na bifu la muda mrefu na huyo mzee wa Kijita wakati wa awamu ya nne.

Ilipoisha awamu ile na baada ya JPM kumrudisha Mjita kwenye baraza lake, ghafla ukaanza tena urafiki wa kutotazamana moja kwa moja machoni kati ya hao wawili.

Kwa hiyo kichwa cha habari cha aina hiyo sio ajabu kuwepo kwenye gazeti la mzee kutoka Machame.
 
Nipashe ni la Mengi.. Linatumika kumchafua Muhongo
Kumchafua kivipi? Wamekuonyesha chanzo kuwa in Katibu wa Bunge. Na MTU asipoonekana bungeni bila taarifa nyaraka za bunge zinamtaja kama MTORO.
Jee mtu mtoro katenda kosa gani kama sio KUTOROKA?
Nitashangaa sana kama kuna mtu atalaumu gazeti
 
Muhongo angejifunza kwa Masilingi enzi za kubinafishwa kwa Kilimanjaro Hotel
Vurugu na Mume wa K-Lyn havijawahi kumuacha mtu salama.

Ile Mengi kuambiwa ana mtaji wa kuwekeza kwenye juice na maji ya kufunga ilimuuma sana.Muhongo atajuta,hawa Maprofesa sijui huwa wanafuata nini kwenye siasa
Nasikia aliletwa na JK enzi za awamu yake. Ile intellectual superiority complex imeshindwa kumtoka na kwenye siasa zetu za kiafrika walio wengi elimu ni za kuungaunga, hivyo kujipatia maadui ni jambo la kawaida kabisa kwake.
 
Aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo, hajaonekana bungeni jijini Dodoma bila ruhusa ya Spika tangu uteuzi wake katika baraza la mawaziri utenguliwe wiki tano zilizopita.

Mei 24, mwaka huu, Rais John Magufuli alitengua uteuzi wa Prof. Muhongo katika baraza la mawaziri, ikiwa muda mfupi baada ya kukabidhiwa ripoti ya kamati ya kwanza ya uchunguzi wa mchanga wa dhahabu (Makinikia).

Hata hivyo, uchunguzi wa Nipashe umebaini kuwa mtaalamu huyo wa Jiolojia wa kimataifa hakuwapo bungeni wakati uteuzi wake wa uwaziri ukitenguliwa, huku taarifa zikidai alirudi nyumbani kwao, Musoma mkoani Mara, kuhudhuria mazishi ya dada yake.

Simu ya Prof. Muhongo iliita bila kupokewa alipotafutwa na Nipashe kwa siku tofauti, ikiwamo jana, kuzungumza sababu za utoro bungeni.

Kutokana na kutoonekana bungeni kwa Prof. Muhongo, Nipashe jana ilizungumza na Katibu wa Bunge kwenye Viwanja vya Bunge mjini Dodoma, Dk. Thomas Kashililah, ambaye alisema ofisi yake haina taarifa za Mbunge huyo wa Musoma Vijijini (CCM) jambo ambalo ni kinyume cha utaratibu.

Kiongozi huyo wa Bunge pia alisema ofisi yake haijui aliko tangu alipoachishwa nafasi ya uwaziri mwishoni mwa mwezi uliopita.

Dk. Kashililah aliongeza kuwa kwa kawaida mbunge anapokuwa na udhuru, humwandikia Spika kumwelezea hatakuwa bungeni kwa muda fulani na ofisi ya Katibu wa Bunge hupewa nakala.

"Sijapata nakala yoyote ya udhuru wa Profesa Muhongo na wala sijui alipo tangu siku ile", alisema Dk. Kashililah.


Katibu wa Bunge huyo alisema hii ni mara ya pili kwa Muhongo kuondoka bungeni kwa muda mrefu bila ya ruhusa kwani hata alipomwandikia barua ya kujiuzulu Rais wa awamu ya nne, Dk Jakaya Kikwete, hakuhudhuria Bunge kwa muda mrefu.

Prof. Muhongo alijiuzulu nafasi ya Waziri wa Nishati na Madini Januari 24, 2015 kwa shinikizo la Bunge, kutokana na taarifa ya Kamati moja ya chombo hicho juu ya kashfa ya uchotwaji fedha katika akaunti ya Tegeta Escrow.

Chanzo: Nipashe
 
Hivi ile sheria ya degree kuwa minimum requirement kwa waandishi wa habari ilipitishwa?
Sielewi inakuwaje hiyo taarifa ina register headline kwenye gazeti kubwa kama hilo...aibu sana hii


Huu ni uandshi wa habarii wa kiwango cha chini kabisa.....upo wakati mmliki wa gazeti hili alikuwa na matatizo na muhongo kuhusu umilikii wa vitalu vya uchimbasji mafuta...sasa haya ndiyo matokeo yake....Yaani hapa ndipo mtu unapoona matatizo ya waandishi wa habari nchini mwetu....
Hivi ile sheria ya degree kuwa minimum requirement kwa waandishi wa habari ilipitishwa?
Sielewi inakuwaje hiyo taarifa ina register headline kwenye gazeti kubwa kama hilo...aibu sana hii
 
Kumchafua kivipi? Wamekuonyesha chanzo kuwa in Katibu wa Bunge. Na MTU asipoonekana bungeni bila taarifa nyaraka za bunge zinamtaja kama MTORO.
Jee mtu mtoro katenda kosa gani kama sio KUTOROKA?
Nitashangaa sana kama kuna mtu atalaumu gazeti

Pamoja na hayo gazeti linajishushia heshima kabisa...Mtu ukisoma headline hapana shaka yoyote utaungansha habari ya makinikia na siyo suala la utoro wa Bunge.....Ni kwamba mmiliki wa gazeti hili ana bifu na Muhongo kwa masuala ya vitalu vya mafuta.....
 
Hivi ile sheria ya degree kuwa minimum requirement kwa waandishi wa habari ilipitishwa?
Sielewi inakuwaje hiyo taarifa ina register headline kwenye gazeti kubwa kama hilo...aibu sana hii

Hukumbuki boss wa hilo gazeti ana issue ya viwanda vya nyanya na juice na Prof. ? Prof Muhongo amejikuta kwenye uozo ulioanza miaka mingi katika wizara hiyo kabla hajateuliwa kuwa mbunge na waziri. Naamini ni mwaminifu aliyezungukwa na mafisadi aliowakuta na kwa kuwa alikuwa nje ya nchi kwa muda mrefu hakuyaelewa mazingira mapema.
 
Mleta mada umesoma vizuri undani wa habariii!??

Umesoma vizuri hicho kichwa cha gazeti au umechukulia kama gazeti la udaku...

Unakta kichwa cha habari "AMINA CHIFUPA AFUFUKA DAR"
Unakimbilia kupost kumbe mwandishi amekumbuka siku yakuzaliwa ya marehemu amina chifupa.

Ushauri wangu kuwa makini!!
 
Back
Top Bottom