Muhimbili sasa ina teknolojia ya kuyeyusha damu (blood clots) kwa watu wenye stroke pia kutibu uvimbe kwa wanawake (Fibroids) bila kufanyiwa upasuaji

Mhaya

JF-Expert Member
Aug 20, 2023
1,658
4,866
MKURUGENZI Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Profesa Mohamed Janabi amesema hospitali hiyo inatumia mtambo wa kuyeyusha damu iliyoganda kwa mtu aliyepata kiharusi.

Profesa Janabi alisema hayo Dodoma jana na akasema kwa sasa kwa wanaopata ugonjwa huo wanatibiwa kwenye kifaa hicho.

“Ukipata kiharusi sasa hivi kama uko Dar es Salaam, ukiletwa Muhimbili tuna uwezo wa kukuingiza kwenye mtambo na kutoa hiyo damu iliyoganda na ukapata nguvu na ukatembea kama zamani…haya ni maendeleo makubwa maana tutapunguza ulemavu kwa wagonjwa hao,” alisema alipozungumza na waandishi wa habari.

Profesa Janabi alisema mtambo huo pia unatumika kutibu wagonjwa watakaokuwa na tatizo la mishipa ya miguu kuziba.

“Kwa kutumia mtambo huo pia tutatibu kina mama walio na uvimbe kwenye mfuko wa uzazi hatutakuwa na haja ya kufanya upasuaji tunaweza kuyeyusha uvimbe kwenye mashine,” alisema.

Kwa wagonjwa wa saratani, Profesa Janabi alisema badala ya kupiga dawa ya saratani mwili mzima mtambo huo utagundua tatizo lilipo na kutibu.

“Ukitumia dawa za saratani mwili mzima kuna madhara pia lazima upate sasa mtambo utarahisisha madhara ya dawa itakuwa kidogo…tumeshaanza kuufanyia kazi huduma zipo zinapatikana katika hospitali yetu ya taifa,” alisema.

Imeandaliwa na Zena Chande
-
Tembelea //epaper.tsn.go.tz kusoma zaidi.
 
Itakuwa ni ukombozi kwa wanaopata kiharusi ambao idadi yao inaongezeka siku hadi siku nchini.
 
Back
Top Bottom