Kiharusi kinaua Watu 30 katika kila Wagonjwa 100 wanaotibiwa Muhimbili

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,377
8,121
1697439664195.png
Wagonjwa wa kiharusi (stroke) 30 kati ya 100 wanaotibiwa Hospitali ya Taifa Muhimbili hufariki dunia kutokana na kuchelewa kufikishwa hospitali.

Hayo yamesemwa leo Oktoba 13, 2023 na Mwenyekiti Chama cha Wanasayansi wa Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu Tanzania (TNA), Profesa William Matuja akizungumza mafunzo ya siku nne ya jinsi ya kukabiliana na magonjwa ya mishipa ya fahamu kwa Afrika, ukanda wa Kusini mwa Jangwa la Sahara.

Mafunzo hayo yameandaliwa na Chama cha Magonjwa ya Mishipa ya Fahamu cha Ulaya (EAN), kwa ushirikiano wa Chama cha Magonjwa ya Mfumo wa Fahamu Afrika (AFAN) na Wizara ya Afya nchini.

Amesema, Tanzania kiharusi bado hakijaelimishwa watu kuwahi hospitali, wanaenda wakiwa wamechelewa, hivyo kati ya watu 100, watu 30 hupoteza maisha Muhimbili.

Amesema, kutokana na ukubwa wa tatizo hilo wameanziasha mtandao wa kuelimisha na kutibu kiharusi kwa watumishi wa kada zote nchi nzima, jinsi ya kuhudumia mtu mwenye kiharusi kwa haraka.

Profesa Matuja amesema jamii haina uelewa wa kutosha namna ya kumhudumia mgonjwa wa kiharusi mara tatizo linapoanza.

“Mtu anapata shida ya kiharusi, kila sekunde anayocheleweshwa ndio anapokua kwenye hatari zaidi, wagonjwa wengi tunawapokea Muhimbili wakiwa wameshachelewa sana matibabu kwa wiki mbili mpaka mwezi.

“Mtu anapata shida ya kiharusi badala awahishwe hospitali anapelekwa huko kwa tiba za asili mpaka analetwa kwetu tayari kashachelewa,“ amesema.

Amesema, tatizo la kiharusi linakua kubwa nchini ambapo mpaka vijana kwa sasa wanapata tatizo hilo.

“Mtindo wa maisha, tabia bwete, ulaji wa chumvi nyingi kwenye chakula, mafuta yaliyokithiri kwenye mishipa ya damu ni miongoni mwa visababishi vya kiharusi kwa vijana na watoto,” amesema Prof Matuja.

Amesema, kwa mujibu wa takwimu za Shirika la afya Duniani (WHO), kila sekunde 40 duniani kuna watu wanapata kiharusi na kati yao watatu mpaka wanne wanapoteza maisha.
 
Back
Top Bottom