FIBROIDS Uvimbe Kwenye Kizazi Unaowatesa sana Wanawake Duniani

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,329
33,138
1620639_10153853121805198_1634614935_n.jpg

FIBROIDS:UVIMBE KATIKA KIZAZI UNAOWATESA WANAWAKE
Katika siku za hivi karibuni,wanawake nchini wamekuwa wakilalamika kuwa kila wanapokwenda kujifungua basi hukutwa na uvimbe katika nyumba ya uzazi.

Uvimbe huo,ambao si saratani, umekuwa ni tishio kwa maelfu ya wanawake nchini jambo linalosababisha wengi wao kuondolewa vizazi vyao.

Daktari Bigwa wa magonjwa ya uzazi wa kitengo cha Pathologia wa Chuo Kikuu Sayansi ya Tiba

Muhimbili,Henry Mwakyoma akinukuliwa na Mwandishi wa Makala haya Bi.Florence Majani,anauelezea Ugonjwa huu na kusema kuwa fibroids kwa kitaalamu ‘leimyoma’ ni uvimbe unaowapata asilimia 25 ya wanawake wa kiafrika na asilimia 50 ya Wazungu.

“Nasisitiza kuwa ,uvimbe huu si saratani,unaojitokeza ama katika ukuta wa kati, wa nje au ndani kabisa ya nyumba ya uzazi,”anasema.

Anasema; ”uvimbe huu huwa katika umbile la misuli myembamba na laini na ukua siku hadi siku,” anabainisha Dk.Mwakyoma na kuongeza kuwa,sababu kuu ya ugonjwa huu,bado haijajulikana.

Anafafanua kuwa,pamoja na kuwa sababu kuu haijajulikana,lakini zipo sababu ambazo zimehakikiwa kusababisha mwanamke kupata uvimbe wa fibroids.

“Sababu inayopewa kipaumbele zaidi ni wingi wa vichocheo vya ‘estrogen’ ambavyo vipo katika miili ya wanawake.” Anasema.

Dk.Mwakyoma anafafanua kuwa ,vichocheo hivi ndivyo hufanya kazi katika mwili wa mwanamke na kumsababishia kupata siku zake za hedhi.

“Ndiyo maana wengi wanaopata uvimbe huu,huwa ni wanawake walio katika balehe au ambao tayari wamevunja ungo,kwani ndiyo ambao huzalisha vichocheo vya estrogeni,”anabainisha mtaalamu huyo.

Lakini,pia anasema kuwa endapo inatokea mwanamke akapata matibabu ambayo yatamtaka kuongezewa vichocheo hivi,huwa katika hatari ya kupata uvimbe huu.

Aidha,daktari huyu anabainisha kuwa,ndiyo maana wanawake walio katika kikomo cha hedhi(menopause) na watoto hawawezi kupata uvimbe huu.

Anazitaja sifa kuu za ugonjwa huu na kusema ,huwa ni nyingi kwa sababu ni uvimbe ambao asili yake ni mishipa midogo midogo na inapokuwa huweza kufikia urefu wa sentimeta tano na zaidi na uzito wa kilogramu 10.

Anaongeza kuwa,uvimbe huu unaweza kutokea katika kuta zote za kizazi cha mwanamke na kumsababishia mwanamke ang’olewe kizazi chake.

“Hata hivyo, wanawake wengi hupata uvimbe huu katika ukuta wa ndani kabisa wa kizazi,”anasema.

Anataja sifa nyingine za uvimbe huu ni kuwa na tabia yake ya kubadilikabadilika sana.

Kwa mfano,fibroids huweza kubadilika rangi na kuwa ya njano,ikabadilika na kuwa katika hali ya kimiminika, baadaye kuwa ngumu au kuwa laini yenye kutomasika.

Dalili za Fibroids
Dk.Mwakyoma anazitaja sababu za ugonjwa huu na kusema kuwa,ni vigumu mwanamke kubaini au kuhisi dalili zake.

“Dalili hutegemeana na eneo ulipokaa uvimbe na ukubwa ,wengi hugundulika wakati wa kujifungua,na ujauzito au endapo mwanamke atapata uvimbe katikati ya kizazi,basi huweza kutokwa damu kwa wingi,”Anasema.

Anasema: ”Hata hivyo,asilimia 35 hadi 50 ya wanawake wanaougua maradhi haya huonyesha dalili wakati wa kujifungua,”

Dalili nyingine ni mwanamke kutokwa damu zake za hedhi kwa wingi na kwa siku nyingi.

Damu za hedhi huweza kuwa nyingi au kidogo sana zikiambatana na maumivu makali.”Asilimia 30 ya wanawake wanaopata maumivu na damu nyingi wakati wa hedhi huwa na uvimbe wa aina hii”anasema.

Anasema wakati mwingine mwanamke huweza kuhisi ana ujauzito kwani uvimbe huu huwa mkubwa na huchezacheza kana kwamba ni kiumbe.

“Nina mifano hai,wapo wanawake waliowahi kuhisi wana ujauzito,wakakosa kabisa siku zao za hedhi,wakapata dalili zote za ujauzito na kumbe walikuwa na uvimbe wa fibroids,”anasema.

Anasema,mara nyingi uvimbe unaojitokeza katika ukuta wan je wa kizazi na kuning’inia,ndiyo hucheza na kuleta dalili za ujauzito.

Mwanamke huweza kuvimba miguu kwa sababu uvimbe huu husababisha damu isitembee.

Anataja dalili nyingine kuwa ni mwanamke kupata maumivu wakati wa tendo la ndoa.

Wakati mwingine ,fibroids hukua na kuzuia mfumo wa mmeng’enyo wa chakula na kusababisha mwanamke avimbiwe.

Vile vile, uvimbe huo uweza kuzuia kibofu cha mkojo na kumfanya mwanamke apate haja ndogo kwa taabu, au akatokwa na uchafu ukeni.

“Hatari kuu ya uvimbe huu ni ugumba,asilimia 27 hadi 40 ya wanawake wanaopata uvimbe katika kuta zote za kizazi, hushindwa kupata watoto,”anafafanua DK.Mwakyoma.

Hatari nyingine ni kwa wanawake wajawazito wenye uvimbe huu ambao wengi hufanyiwa upasuaji kwani fibroids huweza kuzuia mlango wa kizazi na mwanamke kushindwa kujifungua.

Imebainishwa kuwa, asilimia 30 ya wanawake hutolewa vizazi mara baada ya kujifungua kutokana na uvimbe huu.

Mtaalamu huyo anatahadharisha kuwa, wanawake walio katika umri wa kuzaa lakini hawazai wapo katika hatari ya kupata maradhi haya.

“Hii ni kwa sababu vichocheo vya estrogen hukua kwa wingi na kusababisha misuli ya fibroids kukua, lakini vichocheo hivyo huacha kukua wakati wa ujauzito,”anasema.

Anataja walio katika hatari hii ni watawa ambao hawatakiwi kuzaa au wale wanaopitiliza umri wa kuzaa.
Matibabu ya maradhi haya mara nyingi ni kufanyiwa upasuaji na kuondoa uvimbe huu au kutolewa kabisa kizazi.

“Hii inategemea na na umri wa mgonjwa,idadi ya watoto na maamuzi yake binafsi.”anasema.

Wataalamu mbalimbali wa afya ya uzazi wanashauri wanawake kwenda kufanyiwa uchunguzi mara kwa mara ili kubaini maradhi ambayo mengine yanaweza kutibika au kuzuilika. KAMA UNATATIZO HILI BASI LIMEKWISHA NITAFUTE KWA WAKATI WAKO.
 
Maduwi wa mwanamke ni wengi
Daah nikweli nakumbuka wakati nipo chuo kila mwanamke nnayetembea nae alilalamika maumivu wakati wa tendo na wengi waliashiria dalili zote za ugonjwa huu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom