Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,446
- 7,822
Majaribio ya utaratibu mpya wa maegesho ya kulipia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili yameanza wiki hii, ikiwa ni jitihada za kupunguza msongamano wa magari.
Akizungumzia utaratibu huo, Mkurugenzi Mtendaji wa hospitali hiyo, Profesa Mohammed Janabi alisema majaribio yatadumu kwa wiki mbili.
“Tutakapoanza rasmi, wanaoingia na magari watakuwa wakilipia Sh500 kwa saa na kwa wanaoingia na wagonjwa tutawapa dakika 30 za bure kwa ajili ya kushusha wagonjwa, ikizidi hapo ndipo watalipia,” alisema.
Profesa Janabi alisema mgonjwa atakayefika hospitalini akiendesha gari na ikatokea akalazwa, hatatakiwa kulipia gharama za maegesho. Kundi lingine ambalo halitahusika na malipo ya maegesho ni la wafanyakazi wa hospitali hiyo.
Alisema malipo ya maegesho siyo suala jipya katika hospitali hiyo, kwa kuwa miaka ya 1990 kulikuwa na utaratibu huo.
“Utaratibu huu wa maegesho ya kulipia unakuja na faida mbili. Moja ni kuiingizia hospitali kipato na mbili, ni kudhibiti msongamano wa magari,” alisema Profesa Janabi.
Pia, alisema utafiti uliofanyika kwa mwezi mzima ulibaini kila siku yanaingia magari kati ya 3,000 na 3,500.
Akizungumzia malipo ya maegesho, Bahati Masanika, aliyefika Muhimbili kumpeleka mgonjwa alisema ni changamoto kwao.
“Kwa mfano, mimi natokea mkoani niko hapa tangu asubuhi na sasa ni saa tisa, maana yake natakiwa kulipia muda wote ambao nimekaa hapa, kwa hiyo nitakuwa nalipia hela nyingi.”
Kwa upande wake, Daudi Mbwambo ambaye ni dereva wa teksi katika eneo hilo alisema suala hilo ni sahihi kwa kuwa watu walikuwa wanaweka magari bila mpangilio. Pia, alikiri wapo wanaoegesha magari hospitalini na kuyachukua wanapotoka kazini jioni.
Chanzo: Mwananchi
Pia soma: Wanaopaki magari Hospitali ya Muhimbili kuanza kulipia