Muhimbili: Familia yaomba Serikali iisamehe deni la Tsh 10m ili wapate mwili wa ndugu yao mochwari. Profesa Janabi atoa utaratibu wa kuchukua mwili

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,817
4,566
Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu A Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao mochwari.

Mzee Swalehe alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Februari 10 2023 wakati akipatiwa matibabu kutokana na utumbo wake kutoboka na hadi sasa ni siku ya tano wameshindwa kuuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi kutokana na deni wanalodaiwa la milioni Kumi ambapo wanasema wameambiwa watoe asilimia 75 ya deni ndipo wapewe mwili wa Mpendwa wao.

"Tulikuwa na Mgonjwa Muhimbili Hospitali alilazwa Kibasila wodi namba 11 akahamishiwa Mwaisela ICU namba 2 kwa ajili ya matibabu zaidi kwa sababu hali yake haikuwa nzuri hadi February 10 akafariki ambapo nikaambiwa nikafunge bili, nikakuta nadaiwa milioni kumi na laki sita lakini kutokana na hali yangu ngumu ya kiuchumi nikaambiwa nifate process ili tupate msamahama ambapo tuliandikiwa barua na Serikali ya Mtaa tukaenda hadi Muhimbili Ustawi wa Jamii ndipo tukaambiwa tulipe asilimia 75 ya pesa sawa na milioni nane".

"Uwezo wetu ni mdogo sana, kama Serikali inaweza kutupa mwili wetu tutashukuru sana lakini kama haiwezekani basi itabidi sisi tuache tuangalie taratibu nyingine maana hadi sasa tumefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja tu" amesema Stumai Mshale, Ndugu wa Marehemu.

Credit: Millard Ayo

---
Profesa Janabi atoa mwongozo wa kufuata ili kuchua mwili

Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Prof. Mohammed Janabi ameitaka familia ya marehemu Swalehe Mshale (74) kufika katika uongozi wa hospitali hiyo ili kukamilisha taratibu za kupatiwa mwili wa mpendwa wao.

Tamko hilo ni kufuatia familia ya marehemu kuiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na hospitali ya Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao toka alipofariki Februari 10, mwaka huu.

“Utaratibu upo very clear ni kurudi hapo kwa watu wa social (Ustawi) kuna barua ambayo wanatakiwa kuandika ya ‘commitment’ wataacha ID (kitambulisho) wataruhusiwa kuchukua mwili halafu baada ya hapo watakuwa na makubaliano kama ni miezi sita, kama ni mwaka kila mtu anaji-commit kivyake kwamba atakuwa analipa kidogokidogo, hivyo wakamuone Mkurugenzi wa Uuguzi,” amesema Prof. Janabi.

Ameongeza, “tatizo ni kwamba watu wa namna hii hawafuati taratibu wanazotakiwa kuzifuata, badala yake wanakimbilia kwenye jamii wakitarajia tutapata pressure, ‘we don’t get pressure’, hizi hela ni za Serikali.”
 
Familia ya Marehemu Swalehe Mshale (74) wa Mbagala Majimatitu A Wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, imeiomba Serikali kuwafutia deni la milioni 10 wanalodaiwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limefanya wasiruhusiwe kuchukua mwili wa mpendwa wao mochwari.

Mzee Swalehe alifariki katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Februari 10 2023 wakati akipatiwa matibabu kutokana na utumbo wake kutoboka na hadi sasa ni siku ya tano wameshindwa kuuchukua mwili wake kwa ajili ya mazishi kutokana na deni wanalodaiwa la milioni Kumi ambapo wanasema wameambiwa watoe asilimia 75 ya deni ndipo wapewe mwili wa Mpendwa wao.

"Tulikuwa na Mgonjwa Muhimbili Hospitali alilazwa Kibasila wodi namba 11 akahamishiwa Mwaisela ICU namba 2 kwa ajili ya matibabu zaidi kwa sababu hali yake haikuwa nzuri hadi February 10 akafariki ambapo nikaambiwa nikafunge bili, nikakuta nadaiwa milioni kumi na laki sita lakini kutokana na hali yangu ngumu ya kiuchumi nikaambiwa nifate process ili tupate msamahama ambapo tuliandikiwa barua na Serikali ya Mtaa tukaenda hadi Muhimbili Ustawi wa Jamii ndipo tukaambiwa tulipe asilimia 75 ya pesa sawa na milioni nane".

"Uwezo wetu ni mdogo sana, kama Serikali inaweza kutupa mwili wetu tutashukuru sana lakini kama haiwezekani basi itabidi sisi tuache tuangalie taratibu nyingine maana hadi sasa tumefanikiwa kukusanya shilingi milioni moja tu" amesema Stumai Mshale, Ndugu wa Marehemu.

AyoTV inaendelea kuutafuta Uongozi wa Hospitali ya Muhimbili ili kusikia kutoka upande wao. #MillardAy
FB_IMG_16764541282354115.jpg
oUPDATES
 
Kulazwa hapo ICU muhimbili kwa siku ni laki 5.

Wengi hawajui kuhusu msamaha wa matibabu kwa wazee,kama una mzee wako above 65 ni bora ufate process umuandikishe mapema serikali ya mtaa awe na barua ya exemption kutoka hapo muhimbili na pia wanamuingiza kwenye system ili siku akilazwa kuna gharama hutalipa kabisa!

Mimi sikujua umuhimu wa hii kitu adi siku bibi alilazwa hapo ICU siku 10 badala ya kulipa milioni zaidi ya 5 tulilipia kama laki 2+ kwasababu tayari yupo exempted!
 
Back
Top Bottom