Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

  • Thread starter Asha D Abinallah
  • Start date

Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
38
Likes
165
Points
40
Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined Apr 5, 2015
38 165 40
Habari Wakuu,

Shukrani za dhati kwa wale wote ambao wamekuwa nasi katika safari hii toka Disemba 2016 hadi sasa.

Kuweka wepesi kwa wadau mbali mbali ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya Kesi zinazowakabili Mkurugenzi Mtendaji, ndugu Maxence Melo na mwanahisa wa Jamii Media ndugu Micke William kwa madai matatu yanayoendelea, huu ni mlolongo wa yale ambayo yamekuwa yakijiri na kuwekwa JamiiForums kwa kipindi chote toka kesi zilipoanza.

1. Taarifa ya kukamatwa kwa Maxence Melo (Dec 13, 2016). Maxence alipigiwa simu Dec 13, 2016 siku ya Jumanne akiwa ofisini kwake asubuhi akitakiwa kufika kituoni Polisi na alitekeleza wito huo.

2. Taarifa ya Ukaguzi wa Kushtukiza katika ofisi za Jamii Media na nyumbani kwa Maxence Melo. Hadi kufikia Alhamisi, Dec 15, 2016 alikuwa bado ameshikiliwa na Polisi bila dhamana na kushtukizwa kuongoza mahala ofisi za Kampuni yake zilipo.

3. Taarifa ya Maxence Melo kufunguliwa mashtaka Mahakama ya Kisutu na kunyimwa dhamana. Dec 16, 2016 ndipo alifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka matatu; kati ya hayo mashtaka mawili alipata dhamana ya watu wanne, ilipofika shitaka la 3 dhamana ikishughulikiwa, Maxence Melo kaondolewa kinyemela pasipo Mawakili wala ndugu zake kujua na kupelekwa gereza la Keko mida ya saa tano asubuhi Siku ya Ijumaa. Alikaa gereza la Keko kwa siku 4.

4. Taarifa ya Maxence Melo kupata dhamana siku ya 7, na makosa yaliyokuwa yanamkabili: Mashauri yote ya Disemba 29, 2016 yaliahirishwa mpaka tarehe 16, Januari 2017 baada ya upande wa Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika.

5. Taarifa ya kuunganishwa mmoja wa Wanahisa, ndugu Micke William katika mashtaka ikiwa ni Disemba 29, 2016.

6. Mada za mwendelezo juu ya kesi zilivyokuwa zikiendelea
6.5. Kampuni ya OILCOM yahusishwa kwenye kesi namba 456 kama chanzo.

6.8. Kampuni ya CUSNA Investment na Ocean Link zahusishwa kwenye kesi namba 457 kama chanzo.


ANGALIZO: Si siku zote za Mahakama mada ilianzishwa. Hata hivyo mada hizi zinatoa mwanga juu ya kile kilichojiri hadi sasa.​
Kwa ufupi kesi 3 zinazoendelea hadi sasa ni hizi hapa chini:-
Kesi namba 456 - Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.
Obstruction of investigations under Section 22 (2) of the Cyber Crimes Act of 2015 for not complying with an order of disclosure of data in his possession. This follows an order by the Tanzania Police Force to release data pertaining to electronic communications published on his site between May 10, 2016 and December 13, 2016.
Kesi namba 457 - Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.​
Obstruction of investigations under Section 22 (2) of the Cyber Crimes Act of 2015 for not complying with an order to disclose data in his possession. This followed an order by the Tanzania Police Force to release data pertaining to electronic communications published on his Jamii Forums site between April 10, 2016 and December 13, 2016
Kesi namba 458 - Kuendesha mtandao ambayo haujasajiliwa nchini, yaani .tz (Tanzania domain). 2) Kesi iliahirishwa hadi Machi 9, 2017.
Management of a domain not registered in Tanzania under Section 79(c) of the Electronic and Postal Communications Act (2010).


Kufikia sasa, mahakama imeziita kesi zote tatu(appearance before the court) zaidi ya mara 60.
HUKUMU

Mnamo Juni 01, 2018 shauri moja(Namba 457) kati ya mashauri matatu lilitolewa hukumu yake.

Shauri hilo hilo ambalo lilikuwa linasikilizwa mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa na lilikuwa linahusiana na Kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link.

Hakimu Mwambapa baada ya kusikiliza upande wa Jamhuri alisema Washitakiwa Maxence Melo na mwenzake Micke William hawana kesi ya kujibu na hivyo akawaachia huru

Kusoma juu ya hukumu hiyo, tembelea - KISUTU: Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Mike William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru


Wanasheria upande wa Washtakiwa:-
Advocate Peter Kibatala
Advocate Jeremiah Mtobesya
Advocate Jebra Kambole
Advocate Benedict Ishabakaki
Advocate Hassan Kiangio
Advocate Tundu Lissu (hadi pale alipopatwa na jaribio la kuuawa)Asanteni,
Matukio katika Picha Mahakamani (kwa uchache)
2017-12-05-photo-00024352-jpg.692201

img-0865-jpg.692208

2017-10-19-photo-00018710-jpg.692200
 
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2008
Messages
31,052
Likes
17,520
Points
280
Elli

Elli

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2008
31,052 17,520 280
Halafu unakuja kuambiwa kuwa Mlalamikaji ameamua kuachana na kesi hio....

Tutashinda na zaidi ya kushinda, hivi vita vilianza tangu miaka ile ya Jambo Forum na CCM ndio alikua kinara.....kama tulishindo 2006 tuatshinda tena na tena.

Asha D Abinallah natafuta sana t-shirt, ile imeshachakaa sasa. ile ya siku zile Ocean Road
 
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2017
Messages
30,476
Likes
79,689
Points
280
Age
18
Mwifwa

Mwifwa

JF-Expert Member
Joined Apr 3, 2017
30,476 79,689 280
Kuchelewesha kesi kwa madai kuwa upelelezi bado hujakamilika imekuwa ni mbinu yenye usumbufu kwa watuhumiwa jambo ambalo linakera sana.

Hii kesi JF tutashinda, tuwe na subira, Muda ni jibu
 
successor

successor

JF-Expert Member
Joined
Oct 25, 2012
Messages
3,008
Likes
5,341
Points
280
successor

successor

JF-Expert Member
Joined Oct 25, 2012
3,008 5,341 280
Asante kwa Taarifa. Ila kesi ni (Jamhuri vs JamiiForums) au (Jamhuri Vs Maxence Melo & Micke)?
Hii ni kesi dhidi ya Melo & Mike(Jamii Forums), na JF ni sisi members, akishindwa Melo tumeshindwa wote humu.

Naamini tutashinda.
 
Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
38
Likes
165
Points
40
Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined Apr 5, 2015
38 165 40
Inshaallah Mwenyezi Mungu aweke wepesi... Eli, Tshirt naomba tembelea mada hii hapa - Fulana(t-shirt) za JamiiForums sasa zinapatikana kwa bei ya TZS 20,000/=, atakupa maelekezo namna ya kupata. Ina maelekezo yote. Thanks for the support.

Halafu unakuja kuambiwa kuwa Mlalamikaji ameamua kuachana na kesi hio.... Tutashinda na zaidi ya kushinda, hivi vita vilianza tangu miaka ile ya Jambo Forum na CCM ndio alikua kinara.....kama tulishindo 2006 tuatshinda tena na tena. Asha D Abinallah natafuta sana t-shirt, ile imeshachakaa sasa. ile ya siku zile Ocean Road
 
Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined
Apr 5, 2015
Messages
38
Likes
165
Points
40
Asha D Abinallah

Asha D Abinallah

Operations
Staff member
Joined Apr 5, 2015
38 165 40
Poleni sana ofisi nzima ya Jf media, naamini Mungu atawasimamia mtashinda na yataisha tu.
Asante sana Mkuu. Inshaallah na iwe hivyo...

Hii ni kesi dhidi ya Melo & Mike(Jamii Forums), na JF ni sisi members, akishindwa Melo tumeshindwa wote humu.

Naamini tutashinda.
Umeieleza vema Mkuu. I could not have done it better myself. Shukrani...
 

Forum statistics

Threads 1,272,363
Members 489,924
Posts 30,448,844