Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

JamiiForums

Official JF Response
Nov 9, 2006
6,200
4,984
Habari Wakuu,

Shukrani za dhati kwa wale wote ambao wamekuwa nasi katika safari hii toka Disemba 2016 hadi sasa.

Kuweka wepesi kwa wadau mbali mbali ambao wamekuwa wakifuatilia mienendo ya Kesi zinazowakabili Mkurugenzi Mtendaji, ndugu Maxence Melo na mwanahisa wa Jamii Media ndugu Micke William kwa madai matatu yanayoendelea, huu ni mlolongo wa yale ambayo yamekuwa yakijiri na kuwekwa JamiiForums kwa kipindi chote toka kesi zilipoanza.

1. Taarifa ya kukamatwa kwa Maxence Melo (Dec 13, 2016). Maxence alipigiwa simu Dec 13, 2016 siku ya Jumanne akiwa ofisini kwake asubuhi akitakiwa kufika kituoni Polisi na alitekeleza wito huo.

Tembelea Mkurugenzi Mtendaji wa JamiiForums, Maxence Melo anashikiliwa na Polisi, anyimwa dhamana - JamiiForums


2. Taarifa ya Ukaguzi wa Kushtukiza katika ofisi za Jamii Media na nyumbani kwa Maxence Melo. Hadi kufikia Alhamisi, Dec 15, 2016 alikuwa bado ameshikiliwa na Polisi bila dhamana na kushtukizwa kuongoza mahala ofisi za Kampuni yake zilipo.

Tembelea Yaliyojiri kwenye ukaguzi wa Polisi katika Ofisi za JamiiForums na Nyumbani kwa Mkurugenzi, Maxence - JamiiForums

3. Taarifa ya Maxence Melo kufunguliwa mashtaka Mahakama ya Kisutu na kunyimwa dhamana. Dec 16, 2016 ndipo alifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka matatu; kati ya hayo mashtaka mawili alipata dhamana ya watu wanne, ilipofika shitaka la 3 dhamana ikishughulikiwa, Maxence Melo kaondolewa kinyemela pasipo Mawakili wala ndugu zake kujua na kupelekwa gereza la Keko mida ya saa tano asubuhi Siku ya Ijumaa. Alikaa gereza la Keko kwa siku 4.

Tembelea Maxence Melo ashtakiwa kwa makosa 3, likiwemo la Kumiliki Tovuti ambayo haijasajiliwa Tanzania - JamiiForums


4. Taarifa ya Maxence Melo kupata dhamana siku ya 7, na makosa yaliyokuwa yanamkabili: Mashauri yote ya Disemba 29, 2016 yaliahirishwa mpaka tarehe 16, Januari 2017 baada ya upande wa Jamhuri kudai upelelezi haujakamilika.

Tembelea Maxence Melo ashtakiwa kwa makosa 3, likiwemo la Kumiliki Tovuti ambayo haijasajiliwa Tanzania - JamiiForums


5. Taarifa ya kuunganishwa mmoja wa Wanahisa, ndugu Micke William katika mashtaka ikiwa ni Disemba 29, 2016.

Tembelea Mwanahisa wa Jamii Media, Micke William aunganishwa katika kesi mbili zinazomkabili Maxence Melo - JamiiForums


6. Mada za mwendelezo juu ya kesi zilivyokuwa zikiendelea
6.1. Tembelea
Kesi namba 458 inayomkabili Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo kutajwa leo

6.2. Tembelea
Kesi namba 458 inayomkabili Mkurugenzi wa Jamii Media, Maxence Melo kutajwa leo

6.3. Tembelea
Kesi inayowakabili Maxence Melo na Micke William yaahirishwa tena, hakimu Simba atishia kuifuta

6.4. Tembelea
Kesi inayomkabili Maxence Melo yapigwa kalenda hadi Mei 2, 2017

6.5. Kampuni ya OILCOM yahusishwa kwenye kesi namba 456 kama chanzo.

Tembelea (Sehemu ya Kwanza)
Kesi namba 456: Jamhuri dhidi ya JamiiForums - Oilcom na Uchakachuaji/Ukwepaji kodi bandarini Dar

Tembelea (Sehemu ya Pili)
Sehemu ya II: Jamhuri vs JamiiForums kuhusu Oilcom na Uchakachuaji mafuta/Ukwepaji Kodi bandarini Dar

6.6. Tembelea
Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa Jamii Media yaanza kuunguruma Kisutu

6.7. Tembelea
KISUTU: Shahidi wa Jamhuri asababisha kuahirishwa kwa kesi (Namba 457) ya Maxence Melo

6.8. Kampuni ya CUSNA Investment na Ocean Link zahusishwa kwenye kesi namba 457 kama chanzo.

Tembelea
KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaahirishwa hadi Oktoba 17

Tembelea
‪Kesi dhidi ya JamiiForums: Shahidi adai Polisi hawana utaalamu wa kulazimisha kuingilia mawasiliano kimtandao‬

6.9. Tembelea
Kesi namba 456: Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini kufanyiwa marekebisho tena!

6.10. Tembelea
Kesi namba 458 inayowakabili Wakurugenzi wa JamiiForums imeendelea

6.11. Tembelea
Kesi namba 457 dhidi ya (Jamhuri vs JamiiForums) yapigwa kalenda hadi Novemba 15, 2017

6.12. Tembelea
KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri dhidi ya JamiiForums) yaendelea - Shahidi wa Pili atoa ushahidi wake

6.13. Tembelea
Kesi namba 456 (Jamhuri vs JamiiForums): Shahidi akiri mshtakiwa namba 2 yupo kimakosa...

6.14. Tembelea
KISUTU, DAR: Kesi namba 456 yaahirishwa hadi kesho; Hakimu asisitiza anataka iishe Ijumaa hii!

6.15. Tembelea
KISUTU, DAR: Kesi namba 457 (Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa kwa kukosekana shahidi wa Jamhuri

6.16. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidhi ya JamiiForums ya kutotumia Kikoa cha .TZ, yaahirishwa kwa mara ya mwisho

6.17. Tembelea
Kesi namba 456: Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji mafuta bandarini, yaahirishwa mpaka Machi 1

6.18. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 457 (Jamhuri Vs JamiiForums) imeahirishwa hadi Machi 13! Ni ile ya Kampuni za Cusna na Ocean Link...

6.19. Tembelea
Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Hakimu hajamaliza kuandika uamuzi mdogo(ruling)

6.20. Tembelea
Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa. Jamhuri yaomba muda wa kupitia upya jalada la kesi

6.21. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri vs JamiiForums) yaahirishwa. Hakimu abadilishwa, Jamhuri yaomba kupitia upya faili la shauri

6.22. Tembelea
Kesi namba 457: Jamhuri v JamiiForums - Serikali yafunga ushahidi, uamuzi kutolewa Mei 03, 2018

6.23. Tembelea
KISUTU, DAR: Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums) imeendelea tena leo, Jamhuri yakosa tena shahidi! Kutajwa tena Mei 03

6.24. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu ashindwa kutoa uamuzi mdogo kutokana na tatizo la kisheria

6.25. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums), Jamhuri yakosa shahidi! Kesi yaahirishwa hadi Mei 10, 2018

6.26. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) Hakimu aomba muda kusoma jalada ili kutoa uamuzi kama kuna kesi ya kujibu

6.27. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu aomba muda zaidi kutatua tatizo la kisheria kwenye jalada la kesi

6.28. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.29. Tembelea
KISUTU: Hatma ya kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums) kutolewa Mei 28, 2018

6.30. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 457(Jamhuri v JamiiForums), Hakimu apata dharura. Yapigwa kalenda mpaka Juni 01, 2018

6.31. Tembelea
Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

6.32. Tembelea
Kesi ya mmiliki wa JamiiForums yakwama tena

6.33. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.34. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.35. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.36. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.37. Tembele
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.38. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.39. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.40. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.41. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.42. Tembelea -
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.43. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6. 44. Tembelea
Kesi namba 458 ya JamiiForums kutosajiliwa TZ yaendelea. Yapigwa tena kalenda

6.45. Tembelea
Kesi dhidi ya JamiiForums(Namba 458): Jamhuri yahamia shtaka la pili. Ni kuhusu Benki ya CRDB

6.46. Tembelea
KISUTU: Kesi namba 456(Jamhuri v Maxence Melo na Micke William) yapigwa tena kalenda

6.47. Tembelea
Kesi dhidi ya JamiiForums (Kuhusu CRDB): Shahidi kutoka Makao Makuu ya Polisi Kitengo cha Upelelezi Mtandaoni ahojiwa

6.48. Tembelea
Naibu Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao kutoa ushahidi katika Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums

6.49. Tembelea
Uamuzi kesi namba 456 ya kuzuia uchunguzi wa Jeshi la Polisi inayowakabili wanahisa JamiiForums kutolewa Februari 22, 2019

6.50. Tembelea
Kesi namba 458(Jamhuri v JamiiForums): Hakimu afiwa, Naibu Mkuu wa Kitengo cha Makosa ya Mtandao ashindwa kutoa ushahidi

6.51. Tembelea
Kesi namba 456 (Jamhuri v JamiiForums): Washtakiwa wakutwa na kesi ya kujibu, kuanza kujitetea Machi 14, 2019

6.52. Tembelea
Kesi namba 456 (Jamhuri vs JamiiForums): Wakili wa Jamhuri anayehusika na kesi apata dharura, Washtakiwa washindwa kuanza kujitetea!...

6.53. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri vs JamiiForums) yapigwa kalenda tena! Jamhuri yakosa Shahidi...

6.54. Tembelea
Kesi namba 456 (Jamhuri v JamiiForums): Kwa mara nyingine Wakili anayehusika na Kesi apata dharura! Kesi yapigwa kalenda..

6.55. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri vs JamiiForums) yapigwa kalenda tena! Hakimu anayehusika na kesi apata dharura

6.56. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums): Kwa mara nyingine tena Shahidi ashindwa kufika Mahakamani! Kesi yapigwa kalenda

6.57. Tembelea
Kesi namba 456(Jamhuri v JamiiForums): Wakili wa Jamhuri abadilishwa. Shauri lapigwa kalenda...

6.58. Tembelea
Muendelezo wa Kinachojiri Kisutu: Kesi za Jamhuri dhidi ya JamiiForums

6.59. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa tena, Jamhuri yakosa Shahidi! Hakimu asita kufuta shauri

6.60. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums) Shahidi wa Jamhuri ashindwa kufika Mahakamani! Kesi yapigwa kalenda

6.61. Tembelea
Maxence Melo aanza kujitetea Kesi Namba 456 Jamhuri vs JamiiForums juu ya Oilcom na Uchakachuaji Mafuta Bandarini

6.62. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums): Shahidi kutoka CRDB akosekana, kesi kuendelea Oktoba Mosi

6.63. Tembelea
Shahidi akwamisha kesi Na. 458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kuendelea

6.64. Tembelea
Kesi ya namba 458 ya JamiiForums vs Jamhuri yakwama kuendelea, shahidi ashindwa kutokea

6.65. Tembelea
Kesi no 456 (Jamhuri v JamiiForums): Maxence na Mike wajitetea, hukumu ni Novemba 26, 2019

6.66. Tembalea
Kisutu, Dar: Kesi za JamiiForums vs Jamhuri zaendelea. Kesi namba 456 Hukumu kutolewa Desemba 06, 2019

6.67. Tembalea
Kisutu, Dar: Hukumu ya Kesi namba 456 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums kutolewa Januari 22, 2020

6.68. Tembelea
Kisutu, Dar: Kesi namba 458 ya Jamhuri dhidi ya JamiiForums yaahirishwa hadi Jan 28, 2020, Shahidi bado Kitendawili

6.69. Tembelea
Kesi Na. 456 (Jamhuri v JamiiForums): Hukumu yaahirishwa hadi Februari 19, 2020 saa sita mchana

6.70. Tembelea
Kesi namba 458 (Jamhuri v JamiiForums) yaahirishwa tena kwa kukosekana Shahidi. Mara ya mwisho kuwa na Shahidi ni Novemba 12, 2018 - JamiiForums

6.71. Tembelea Hukumu ya kesi namba 456 ya 2016 inayowakabili Maxence Melo na Mike Mushi iliyokuwa itolewe leo, imeahirishwa kwa mara ya 5 - JamiiForums

6.72. Tembelea Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru - JamiiForums

6. 73. Tembelea Kesi namba 458 (Jamhuri v Maxence Melo): Ni ile kesi ya JamiiForums kudaiwa kutotumia Kikoa cha do-tz, imepigwa tena kalenda hadi Juni 25, 2020 - JamiiForums

6. 74. Tembelea ‪Kesi namba 458 dhidi ya JamiiForums: Jamhuri yaomba Hati ya kukamatwa Shahidi, Mahakama yaridhia!‬


ANGALIZO: Si siku zote za Mahakama mada ilianzishwa. Hata hivyo mada hizi zinatoa mwanga juu ya kile kilichojiri hadi sasa.

Kwa ufupi kesi 3 zinazoendelea hadi sasa ni hizi hapa chini:-


Kesi namba 456 - Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.

Obstruction of investigations under Section 22 (2) of the Cyber Crimes Act of 2015 for not complying with an order of disclosure of data in his possession. This follows an order by the Tanzania Police Force to release data pertaining to electronic communications published on his site between May 10, 2016 and December 13, 2016.

Kesi namba 457 - Kushindwa 'kutoa ushirikiano' kwa Jeshi la Polisi kwa kuzuia taarifa binafsi za wateja wa mtandao wake.

Obstruction of investigations under Section 22 (2) of the Cyber Crimes Act of 2015 for not complying with an order to disclose data in his possession. This followed an order by the Tanzania Police Force to release data pertaining to electronic communications published on his Jamii Forums site between April 10, 2016 and December 13, 2016

Kesi namba 458 - Kuendesha mtandao ambayo haujasajiliwa nchini, yaani .tz (Tanzania domain). 2) Kesi iliahirishwa hadi Machi 9, 2017.

Management of a domain not registered in Tanzania under Section 79(c) of the Electronic and Postal Communications Act (2010).

Kufikia sasa, mahakama imeziita kesi zote tatu(appearance before the court) zaidi ya mara 60.


HUKUMU
Mnamo Juni 01, 2018 shauri moja(Namba 457) kati ya mashauri matatu lilitolewa hukumu yake.

Shauri hilo hilo ambalo lilikuwa linasikilizwa mbele ya Hakimu Godfrey Mwambapa na lilikuwa linahusiana na Kampuni za CUSNA Investment na Ocean Link.

Hakimu Mwambapa baada ya kusikiliza upande wa Jamhuri alisema Washitakiwa Maxence Melo na mwenzake Micke William hawana kesi ya kujibu na hivyo akawaachia huru

Kusoma juu ya hukumu hiyo, tembelea
Kesi namba 457: Mahakama yasema Maxence Melo na Micke William hawana Kesi ya kujibu! Yawaachia huru

Kesi namba 456 ya 2016 JamiiForums vs Jamhuri, Kisutu: Maxence Melo ahukumiwa Mwaka jela au faini ya Tsh. Mil 3. Mwenzake aachiwa huru - JamiiForums

08 APRILI 2020: HUKUMU YA KESI NAMBA 456

Mahakaka ya Hakimu Mkazi Kisutu imemhukumu, Mkurugenzi Mtendaji wa Mtandao wa JamiiForums, Maxence Melo(40) kulipa faini ya Sh3 milioni au kwenda jela mwaka mmoja, baada ya kutiwa hatiani katika shitaka moja la kuzuia jeshi la polisi kufanya uchunguzi.

Pia mahakama hiyo imemuachia huru Mike Mushi ambaye ni mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo ya jinai namba 456/2016.

Mushi ameachiwa huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuthibitisha shtaka dhidi yake.


17 NOVEMBA 2020: HUKUMU YA KESI NAMBA 458

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imemuachia kwa Masharti ya kutokufanya kosa kama hilo ndani ya Mwaka mmoja, Mkurugenzi wa JamiiForums Maxence Melo, katika Shitaka namba mbili la kuzuia Upelelezi wa Jeshi la Polisi

Aidha, Shitaka la Kwanza la kutosajili JamiiForums kwa kikoa cha Dot-TZ akikutwa hana hatia.

Mshitakiwa namba mbili amekutwa hana hatia makosa yote Mawili. Hakimu Huruma amesema, Mshitakiwa namba mbili Mike Mushi alikuwa kama Msindikizaji kwenye hii kesi namba 458 ya Mwaka 2016.

Katika shtaka la pili, Polisi ilimtaka Mkurugenzi wa JamiiForums kutoa taarifa za Wanachama wawili waliodaiwa kuandika kuhusu madai ya uhalifu uliokuwa ukiendelea CRDB, kwa kushirikiana na wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari.


Wanasheria upande wa Washtakiwa:-

Advocate Peter Kibatala
Advocate Jeremiah Mtobesya
Advocate Jebra Kambole
Advocate Benedict Ishabakaki
Advocate Hassan Kiangio
Advocate Tundu Lissu (hadi pale alipopatwa na jaribio la kuuawa)

Asanteni,


Matukio katika Picha Mahakamani (kwa uchache)
2017-12-05-PHOTO-00024352.jpg

IMG-0865.JPG

2017-10-19-PHOTO-00018710.jpg
 
Halafu unakuja kuambiwa kuwa Mlalamikaji ameamua kuachana na kesi hio....

Tutashinda na zaidi ya kushinda, hivi vita vilianza tangu miaka ile ya Jambo Forum na CCM ndio alikua kinara.....kama tulishindo 2006 tuatshinda tena na tena.

Asha D Abinallah natafuta sana t-shirt, ile imeshachakaa sasa. ile ya siku zile Ocean Road
 
Inshaallah Mwenyezi Mungu aweke wepesi... Eli, Tshirt naomba tembelea mada hii hapa - Fulana(t-shirt) za JamiiForums sasa zinapatikana kwa bei ya TZS 20,000/=, atakupa maelekezo namna ya kupata. Ina maelekezo yote. Thanks for the support.

Halafu unakuja kuambiwa kuwa Mlalamikaji ameamua kuachana na kesi hio.... Tutashinda na zaidi ya kushinda, hivi vita vilianza tangu miaka ile ya Jambo Forum na CCM ndio alikua kinara.....kama tulishindo 2006 tuatshinda tena na tena. Asha D Abinallah natafuta sana t-shirt, ile imeshachakaa sasa. ile ya siku zile Ocean Road
 
Poleni sana ofisi nzima ya Jf media, naamini Mungu atawasimamia mtashinda na yataisha tu.

Asante sana Mkuu. Inshaallah na iwe hivyo...

Hii ni kesi dhidi ya Melo & Mike(Jamii Forums), na JF ni sisi members, akishindwa Melo tumeshindwa wote humu.

Naamini tutashinda.

Umeieleza vema Mkuu. I could not have done it better myself. Shukrani...
 
25 Reactions
Reply
Back
Top Bottom