Sorry
fyddell, nilikuwa mbali na majukumu mengine
nimeiona concern yako labda nianze hivi, Kweli mwanzo wa Dunia ni Mwanzo wa Ulimwengu, lakini nilichokuwa namaanisha hapo ni hiki
Kwa mujibu wa Vitabu vitakatifu kama ulivyomention hapo juu na kwa uelewa wa wana sayansi wa kale na watu wa dini ni kuwa muda halisi wa Dunia ulikuwa unabase zaidi kuanzia uumbaji wa Dunia (Earth), vitabu hivyo havikuzungumzia sana uumbaji wa Ulimwengu (Universe), vitu kama Nyota, Mwezi na Jua vilikuwa vinaonekana kama ni part ya Dunia na wala sio Ulimwengu yaani ni vitu ambayo vilikuwa duniani kama tunavyoona Bahari Milima nk.
Ni kweli Vitabu vinaposema ikawa usiku-ikawa mchana siku ya kwanza hapo ilikuwa ina refer jua na mzunguko wa Dunia kwa ujumla wake. Hivyo Kidini na hata sayansi ya Zamani/Kale inaonyesha umri wa Dunia including Nyota, Mwezi, Jua, Milima na Bahari, unaanzia na uumbaji wa siku ya kwanza kisha siku ya Sita ndio Adam akaumbwa,
So Kidini na Sayansi ya Zamani inaonesha kuwa Duniani (Nyota, Jua, Mwezi, Milima, Bahari) ni changa mno, ambayo haizidi miaka 10,000, na hili lilitokana na Hesabu zilizofanywa na wasomi wa kidini na wanasayansi wa kale kwamba walichukua siku sita za uumbaji, kisha wakaenda na umri wa Adamu mpaka Jesus, na kutoka Yesu mpaka sasa.
Maendeleo ya kisayansi ndio yamekuja kuwafamahisha watu kuwa Jua, Nyota sio "Mali" ya Dunia pekeyake bali kuna sayari nyingi ziko kwenye Mzunguko wa Jua, na kuna Sayari nyingine nyingi zaidi ya Dunia, na kuna Galaxy nyingi tu, na hizo zinazoonekana kama nyota zingine si Nyota bali ni Sayari zingine.
Radiometric Dating imekuja kuprove kuwa Dunia haina miaka chini ya 10000, bali ina 4.5Billion years, so Radiometric imekuja kutoa ile mentality ya sayansi ya kale kuwa dunia ni changa kwa kuionyesha Dunia ni Nzee.
ndio hapo niliposema kuwa radiomentric imeuvuta ule muda wa dunia uliokuwa unajulika wa chini ya 10000 na kuwa 4.5bil years sawa na Baadhi Sayari, Vimondo, Nyota, Miezi nk.
Labda kama kusingekuwepo na Radiomertic basi tungeendelea kuwa na imani ileile ya kuwa umri wa Dunia uko chini ya 10,000yrs
Hope nimejaribu kukuelezea nilichokuwa namaanisha